Michano/Hiphop/Freestyle

Michano/Hiphop/Freestyle

Nikichana ngumu naishia kuskika geto, mabishoo wanalaumu mistari imewazidi uwezo.../

Mara Scars acha ndumu ufanye commercial, ili uweze kudumu kwenye soko la kesho.../

Njia imejaa visiki na vigingi, ukiwa peku haupiti.../

hata hao wabana pua mtaani hawana shilingi, hali tight nishafanya utafiti.../

Bongo bila kiki mziki hauskiki, kubali kuitwa chawa kwa celebreties uta hit.../

Nakomaa na game, wala sitaki inilipe../

Mi ni rapper sitaki fame, na kwenye magazeti ikibidi msiniandike.../
 
Kuchana nikizididisha watasema nabahatisha,
mademu wananipisha wakiona nimedindis*a,
hawataki nianze waliasha eti nitawavimbisha,
iramba naiwakilisha mpaka chuga natisha, wanasema me ni noma cha ajabu hata sijasoma,
haters wananitazama wanapata tu trakoma.
Hiki kipaji ni kama kifo hakuna wa kukizuia
Nina mistari kama maandiko shauri yako unayepuuzia,
Wao wnakazakaza jamii foram tunakazana
Leo wanawazawaza sisi tumeamua jana.
 
Nikishuka wanastuka kama wamemwona masih/
marapa wenu vipusa kwenye game wanaanguka, course hawana plan b/

Fungua roho upokee flow za uzima, mc wengi much know mithili ya Gwajima/
kutwa wanahit na kiki wakati pikipiki za kuazima/
Ulivyo sema Much know mithili ya Gwajima nimeona niweke na mdhamini Gwaji boy.

 
Nyani ngedere na kima wote jamii moja,naona mnakuja wima wima mmesahau mna mguu mmoja"

Niite king wa hizi Mambo,Mambo mkangaja,mtatubu wote watoto wadogo Ben mwaipaja"

Kata keki tule how old are you now,watoto wadogo washule hizi anga za mafarao"

Chini ardhini juu ardhini pateni idhini,keti kitini simamia ulimi kalia mpini"

Vina utata na mwanzo mwisho,ngumu za haja mipasho mwiko"karibu barza shekhee,imeingia ikitoka iwekee"""

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni Ngumu kwa warembo, hawaitaki kama magendo/
njooni kinondoni kati muone mizengo/
wazee wa mapank na mapedo milegezo wanamegwa na madoni kama mengo/
Niko fresh kamiligado,natema verse zaidi ya kado/
Mi ni goat kama ronaldo, kwenye battle ni vichapo na visago marapa wenu wapeni panaldo/
 
Sikia King nimerudi, baba mwenye mji,
Kuachia kipaza hamna budi, fake msio vipaji,
Siwajaji, mila na desturi tufate itikadi,
Wanyoa viduku, wavaa vikuku,
Nna ugwadu Kama mjela nawanyonya Kama chuchu,
Kichwa full ma power, Uhuru ni dawa,
Demu unamwita baby hujawahi mwaga shahawa,




Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Haya maisha bila pesa, utateswa kama mtumwa../
Nilikotoka nilisota, ila sikutazama nyuma../
watu waliona nimemoka kwakua biashara zilibuma/nikashindia nguna na mboga nilizovuna../
maskini sikuwa na kipato, mademu hawakunithamini kutokana hali ya geto../ nikakosa kujiamini nikaishia kupga nyeto../
now chek life lipo gado, benk zikijaa/kiroho mbaya/nazi-burn na fire kama pablo../
 
Sura ya mbuzi na chunusi kila angle, wananiita buzi aka mzee wa migegedo/

Mafisadi hawana upendo, wanaiba mpaka katiba coz hawaina haiba ya uzalendo/
Nchi imeshauzwa zimebaki screpa, Viongozi wanatupuuza, upinzani wanatekwa/wengine wanatoweka, spika anacheka/bungeni ni vitimbwi na vibweka/
Nani wakuilinda nchi, kama sio sisi wananchi../
Inapaswa tuungane bila kujari vyama vyetu, ili tulilinde keki ya taifa letu isiliwe na mafisi../
 
Kwanza nawapa salamu, nazingatia itifaki/
Nadhani Mvumbo mnamfahamu, kwenye mistari mimi ndiye chaki/
Naandika zaidi ya kalamu, mwana Hip hop kindaki ndaki/
Ma mc's wa Jamii Forum, karibuni nyuma msibaki/
Leo mitandaoni ukisema usome, habari zimejaa ukakasi/
Huku Kiba anasema UNIKOME, huku Idriss akaripoti Polisi/
Huku Kigwa kavunja ngome, Le M'bebez kapiga pasi/
Haya yasikufanye ulale ukorome, pambana watoto wasile nyasi.
Ni kama hujui unapokwenda kwaiyo ulipo utaona kama umefika

MSODOKI
 
Mimi ni mhuni japo Sometime nageuka pastor, nauza imani ya mbinguni kisha nakomba sadaka../
Mtaani kwetu hakuna matabaka wala siri, tunapeana madili then we move faster../
Maisha ya sasa bila mkwanjwa utadata,huu ni muda wa ma' master wagumu tunapeta/ wakuda wamekatwa../
Hii ni ngumu sio easy, vichwa panzi hawawezi elewa thats why hawakatizi pande hizi/
ni uduwanzi kusema zama hizi, hakuna rapa kama fid na ngwair../
wakati street kuna watu wanaflow kichizi hawafiki mbele, au mpaka watumie irizi kama mzee kagere../
 
Mgumu na roho ngumu zaidi ya paka, mi ni rasta ila nakula bata mpaka pasaka/
Sina shaka niko huru navuka mipaka, niko africa chaka la vibaka wa siasa/
Nasaka vumba sina time nawachumba, nikizpata sitazitumbua kama idris na kayumba/
Npo fit siwezi kuyumba, masnitch wamekosa info wanatia huruma/
 
Bunju,kunduchi,mkuki au bunduki/
Nawatoa nduki kama hasira za nyuki/
Mkuki haunikuti na moyoni sibabuki/
Na hata mkinichoma Kwa Hilo Jani la kuti.......
Maji,biskuti kamanda natinga buti/
Mkononi na bunduki, naanza duty/ Naanza kuruka futi adui anakunja goti.......

I'm poison killer akasome
Tito magoti/

Ghost
Dumas the terrible!
 
Nipo kwenye uzi wa mvumbo na flow bila mdundo/
Mabishoo nimewapoteza kwenye ulingo, nalinda culture kama umbwa chindo/
Natema mistari heavy,ni mizigo kwa mandezi wanaofake/
wananiita mbobezi cause napanga tenzi zaidi drake/
sometime nanuna sicheki, nageuka maimuma napata blood thirsty/
masnitch hawanajipya wanakuna kichwa, info zimefichwa hawapati picha nawadondosha utadhani hitler/
 
Imeandika utakula kwa jasho na utazaa kwa uchungu, najidai nanilicho nacho maana riziki mafungu/
Siachi kuhaso mpaka nipate pesa kama bakhresa/kutesa kwa zamu na hii ndio zamu ya walioteswa/
bongo joto money makers hatuna presha tunakesha kama popo/
sitegemei ndugu kwangu wa kwanza ni mungu, wa pili ni alienizaa kwa uchungu japo nilikua mtundu bado alinithamini na kunilea kizungu/
 
Mwaka wa tano niko ndani ya mjengo, ID fake najificha kama bidhaa ya magendo.../

Kama JF imetupa uhuru wa kuhoji, kwanini tujifiche nyuma ya keyboard?.../

Ona mpaka maisha tunalazimika kufoji, yani mtu yuko bongo ila utaskia niko abroad.../

Naskia humu kuna wapelelezi hatari, wanafatilia wakosoaji wa serikali.../

Kuwa makini na ukae kwa tahadhari, wakikunasa utajuta kuzaliwa hii sayari.../
 
Mi ni dokta usinichagulie bega, nina diploma ya punda mpaka lawama nabeba.../

Hata bila mnyororo mi nitachanga peda, huu ni msala kama umefumwa na mke wa mjeda.../

Baada ya battle na mimi kibonde hoi, alijidai real kumbe fake kama views za konde boy.../
 
Viongozi tuliowachagua wanatutesa nakututia doa, wanakomba pesa hawaachi hata nyoya/
Nchi inaendeshwa kiboya, bungeni wamejaa mabogas/ hawana hoja wala umoja mda wote wamepoa/
Polisi wanatufilisi badala ya kulinda nchi/
Wanyonge wanazidi kunyongeka, biashara za madawa na umalaya zinadidi kuongezeka/
 
Viongozi tuliowachagua wanatutesa nakututia doa, wanakomba pesa hawaachi hata nyoya/
Nchi inaendeshwa kiboya, bungeni wamejaa mabogas/ hawana hoja wala umoja mda wote wamepoa/
Polisi wanatufilisi badala ya kulinda nchi/
Wanyonge wanazidi kunyongeka, biashara za madawa na umalaya zinadidi kuongezeka/
Hii nchi bado inaujinga mwingi, vitu bei juu afu eti mama anaupiga mwingi.../

Viongozi wengi bado ni walowezi, kutoka ngazi ya kata hadi wakurugenzi.../

Ni mafisadi kiufupi ni wezi, kodi za wanachi wanazila bure kila ifikapo mwisho wa mwezi.../

Mgao wa umeme naskia umewekewa ratiba, aisee huu uongozi hautufai ebu tupeni katiba.../

Tozo za miamala zimeongezewa riba, uamuzi ni wako kukaa na govi au kumfata ngariba.../
 
Back
Top Bottom