Zohaan
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 268
- 273
Upendo hakuna wameweka pesa mbele..//Upendo umefika mwisho, wapendanao wanajinyonga/
Wengine ni vitisho, kama mikwara ya Mandonga/
Hakuna upatanisho, kila mmoja anachonga/
Kifo ndio hitimisho, hata kama alikukonga/
Unaempenda hakupendi kama uteja wa unga/
Usiye mpenda haendi kama kamba umemfunga/
Dharau haijengi siyo tofari la nyumba/
Mapenzi yana mengi bwana mdogo chunga/
Mnunulie simu wenzako wampe vocha/
Jifanye mwalimu ajifanye kocha/
Mpe za kujikimu akakufanye ndondocha/
Yanakata stimu mapenzi ulofa/
Hiyo bastola unayonunua, haitaua kabisa vibaka/
Bali mwenyewe utajiua, utakapokuta mkeo wamempakata/
Wachache wana mapenzi ila tenzi kuwapata/ hauwezi bila Mwenyezi utadata/ kindezi kisa penzi atakukamata/
Kwa mwenye Benz atakuacha/ hauna malezi linavuja pakacha/ hata uwe mbezi na pesa ya kutakata/ bado utafanyiwa ushenzi kwa muuza kashata/
Ule muda unasaka mahitaji, ili Family njaa isijelala/
Wife yupo kifuani kwa mshikaji, huku akikuita fala/
Mapenzi hayana Falsafa, hata uwe umesoma sana/
Mapenzi yanaleta maafa, sio Tarime mpaka Tanga wanauwana/
Mke ana nuna ukiacha pesa ya tembele..//
Maisha utaftaji hawajui tunayoyapitia..//
Wao kazi udangaji na kugeuka viruka njiaa..//
Tumuombe MANANI arudishe upendo na amani..//
Hekima nidhamu tuishi kama Zamani..//
Amani furaha zitawale majumbani..//
Mola hatotuacha me nakiri abadani..//