#Miss valentine challenge
Hapendi pombe, ingawa anaguu la bia..|
Bonge la shombe, anajua kujitupia..|
Hahitaji wapambe, mahitaji yote namtimizia..|
Hataki niwe mnyonge, yuko radhi agongwe ili nivuke njia..|
Sina wenge, na magenge yanayomvizia..|
Moyo kaugeza ngome, mi mfalme yeye ndio malkia..|
Penzi lake tamu, haikati hamu/ napenda kuona lake tabasamu..|
Mambo ya umbea hayapi taimu, anajua kukosea ni tabia ya binadamu..|
Ananipa denda, ili niache kupenda sigara..|
Nikikosea tunayajenga, hanaga papara..|
Kutuachanisha, ni kupanda mchicha kwenye jangwa la sahara..|
maji ya gundu Mvumbo Scars