Michano/Hiphop/Freestyle

Michano/Hiphop/Freestyle

Wananiita mkuu/ na ukifoka/ nakumeza/

Mvumbo nipo juu/ nachoka/ kuwaelekeza/

Town kitambo/ kama ma bus ya Uda/

Kabla Mambo jambo/ hawajajua msuba/

Kabla ya Rambo/ nini tamthilia ya Huba/

Nafanya mambo/ nazichanga fuba/

Nishavaa suti/ nishavaa Gucci/ mitaa nishafunga/

Kuhusu papuchi/ nazijua nyuchi/ zaidi ya Mkunga/

Watoto beki hazikabi, wakijaribu wanafichwa/

Niite Mvumbo Alshabab, nawakata vichwa/
 
Siwaelewi Ma Mc's/Hasa wa siku hz/

Hawajui hz ladha Zina utamu Zaid ya kupiz/

Ona wanaficha sura/ wanaona aibu ka mama mwenye fistula/

Wanashindwa chakata medulla/Hawafanyi kazi vp tuwaruhusu Kula/

Wanfunika mdomo/ wakisahau matundu nyuma ya kaptula/

Leo nawapa somo/ waache uvivu Hawa chura/

Kaza shingo nikuvunje kwa hz iron monkey bars/

You ain't scare me with baby face ryhmes/
 
Nimepiga jiwe mgodi noti imepiga hodi/
Namshukuru God silipi kodi navimba road/
Sisukumi Bm wala Verossa/ liwanza Gadem kuna kitu nitakosa/
Nikaagiza kichwa cha Semi/ nikaki pimp full utemi/
Muziki mnene na mwendo hatudemi/
Namwaga mapene madem hawasemi/
Jicho jekundu kama Remmy/ tunakunywa za kizungu minazi hatugemi/
Kuna siku nipo Club akaja babu/akanipa salamu ya kiarabu/
Akasema anaishi maisha ya tabu/ nimsaidie akanunue japo kababu/ hali mbaya njaa ndio sababu/
Nikamwambia mzee huna ustaarabu/ huu ni muda wa pombe na makushabu/
Unaniletea michongo ya ajabu/
Utavishwa nikabu/ kama kina Maajabu/
Akaniambia sina adabu/ atanipa adhabu kisha akasepa kwa ghadhabu/
Siku kadhaa nyani akatema bungo/
Mali na chapaa TRA wakapiga mtungo/
Madem vifaa wakasema nanuka uvundo/
Sasa hivi jamaa napiga debe Ubungo/
 
Mvumbo mademu wa siku hiz niku hit then una run,ukifwata mkumbo watakuchuna pesa hadi utalani/
shida yao nikushibisha matumbo na mapenzi kwao kama utani/ ukiwa na pesa watakuonyesha upendo usio na kifani/
ila hawana true love wengi wao ni makahaba, bila ela hupewi kitu zaidi ya mabusu tu labda/
Kula mzigo kama kawa/ kisha kula kona/ usipende kizungu/

Hawakawii kukufanya dawa/ wakishapona/ wanasema ni chungu/

Wachache wapo sawa/ ukiwapata mbona/ hawatakupa machungu/

Ila wengi wameshapagawa/ na wamenona/ nyuma wana nundu/

Oa ujinyonge/ wahonge/ unyang'anywe tonge/ ufanywe mnyonge/ wamgonge/

Unajitamba unamjali, mpaka kwa mabest/

Kumbe watu wanaramba asali, kama Government/
 
Mbona kimya, mbona Kama mnajinyima,

Ma Mc's wote deki au mmeishiwa vina,

Nagaagaa na upwa ndio maana sili wali mkavu,

Ni Nani Kama mmanaeweza stand above,
Misokoto inafanya watoto mnapagawa/

Si unajoto, basi leo umekutana na popobawa/

Ungekuwa ugonjwa , basi mi ndio dawa/

Jaribu kwengine, mi ni mashine nimekuzidi pawa/
 
Kula mzigo kama kawa/ kisha kula kona/ usipende kizungu/

Hawakawii kukufanya dawa/ wakishapona/ wanasema ni chungu/

Wachache wapo sawa/ ukiwapata mbona/ hawatakupa machungu/

Ila wengi wameshapagawa/ na wamenona/ nyuma wana nundu/

Oa ujinyonge/ wahonge/ unyang'anywe tonge/ ufanywe mnyonge/ wamgonge/

Unajitamba unamjali, mpaka kwa mabest/

Kumbe watu wanaramba asali, kama Government/
Tangu nimetoswa na zuwena, mademu sina hamu nao tena/

Nafahamu makosa tumeumbiwa binadamu, ila nimechoshwa na masinema/

Ukiwa na pesa utawatekenya, zikishatoweka watakuacha dilema/
 
Mwamba niko moto sijapoa/

Ma mc watoto wanaboa, halafu wepesi kama nyoya/

hawana changamoto, hata
kwa mkono wa kushoto nawazoa/
 
Freestyle session 1.

Niko imara kama mjeshi vitani./
Tangu zamani, Humu ndani sina mpinzani./

Naflow faya mpaka maik inabani./
Ma mc uchwara
nimewaficha kwapani./

Sikia kayafa, elimu ya darasa ina mwisho..|
Hip-pop sio rasta, naheshimu kacha kama mrisho..|

Hata nipewe kesi ya siasa, ntaiskep kama petrol..|
 
Freestyle session 2

Huwezi kuwa dingi, kama huna misingi imara..|

Wapinzani wamekata lingi, daima ntabaki mshindi kama cheguevara..|

Jf mi ni freestyle king, nyie mapimbi mjipange..|
Siwezi toa shilingi, ili nipambwe..|

Najulikana kila pande, kama connection ya afande..|

Mi na hip pop, ni sawa na umbea na mange..|
Pusha na bange, au Masikini na maharage.||

Natema madini utasema ruge..|
sijapagawa na udini, ntakufa kirasta kama dube..|
 
Leo Rap naifanyia uovu/ ma Mc kwenye nyuzi za povu/ hapa wanaogopa kovu/ ila mkonga wangu haunishindi ndovu/

Mvumbo namba bovu/ Media nawasikia wachovu/ wakipewa mashavu na Mchomvu/ halafu wanaleta utovu/

Siendekezi jina, kama haiongezi flusi/
Japo natema vina, ka' nimemeza kamusi/

Mistari yao ya ki China, hapa hawagusi/
Kwenye vita ya milima, wanaleta kifusi/

Kichwa changu ni River, mashairi kama samaki/

Nasimama kama Shiva, kutetea haki/

Walioleta za ki Diva, na battle za kiwaki/

Waambie mawe yameiva, na kuni zimebaki/
 
Hakuleta za kishost wala u sister duu/

Hakuomba noti japo sio matawi ya juu/

Alikuwa na love hot moto wa kifuu/

Anawaka She got A gwan East zoo/

Nimemjua tu last wiki/ ila moyoni kawa topic/ sijui kaniteka vipi/

Hakunipa style ipi?/ moto kwenye miti/ mtoto gademiti/ kwenye pipi ya kijiti/

Anachezea kila engo/ akiondoka naliona pengo/ nikampeleka kwenye mijengo/

Tukapanga malengo/ nikamwambia hapa pesa haina mwendo/ akanikanya mwanangu Mazengo/

Nisiuze ramani kwa upendo/ asijue dili zetu za unga na magendo/ wala meno ya tembo/

Nikamwambia mtoto anazijua nyendo/ aache za Omary Nyembo/ na wivu kwa mrembo/ kumbe haikuwa skendo/ leo nagundua mtoto ni Kitengo/ na Defender ipo kwenye mwendo/

Kidume nimekamatwa kama jambazi/ nimefyata japo nina vijana wa kazi/
Maafande watata wamejaa shazi/
Pesa haijamata ishu ipo juu ya ngazi/
 
Nimepiga jiwe mgodi noti imepiga hodi/
Namshukuru God silipi kodi navimba road/
Sisukumi Bm wala Verossa/ liwanza Gadem kuna kitu nitakosa/
Nikaagiza kichwa cha Semi/ nikaki pimp full utemi/
Muziki mnene na mwendo hatudemi/
Namwaga mapene madem hawasemi/
Jicho jekundu kama Remmy/ tunakunywa za kizungu minazi hatugemi/
Kuna siku nipo Club akaja babu/akanipa salamu ya kiarabu/
Akasema anaishi maisha ya tabu/ nimsaidie akanunue japo kababu/ hali mbaya njaa ndio sababu/
Nikamwambia mzee huna ustaarabu/ huu ni muda wa pombe na makushabu/
Unaniletea michongo ya ajabu/
Utavishwa nikabu/ kama kina Maajabu/
Akaniambia sina adabu/ atanipa adhabu kisha akasepa kwa ghadhabu/
Siku kadhaa nyani akatema bungo/
Mali na chapaa TRA wakapiga mtungo/
Madem vifaa wakasema nanuka uvundo/
Sasa hivi jamaa napiga debe Ubungo/
Hapo kati ume flow kam JCB Makala.
Bigup Mvumbo
 
Natoka shamba nishapiga noti za mahindi/

Naingia Dar kutamba kutumia shilingi/

Kila kona wameuramba sijui yupi Queen yupi King/

Na wote wanachamba eti wanaupiga mwingi/

Dume limesuka, chini viatu vya kina mama/

Suruali inaanguka, ukiuliza anasema ni unyama/

Hana kazi wala duka, anashinda skani na wana/

Jioni anasukuma chupa, na meza inajaa sana/

Ukishindana nae utakufa njaa, hujui pesa anatoa wapi/

Ila haina kushangaa, inazingatiwa itifaki/

Watoto wanaotembea tembea, ni wa kufinya na kukanya/

Huku wanaogopewa, Road wanaitwa Panya/
 
Dume limesuka, chini viatu vya kimama
Suruali inaanguka, ukiuliza anasema ni unyama"

Mistari imenyoka.
 
Usiulize mi ni nani..|
Mi ndio yule naepinga muafrika kuitwa nyani..|

Duniani hakuna amani, popote unapotimba hakikisha kiunoni upo na gun..|

Maisha mafupi kama suti ya zakayo..|
Ukiona mjini nuksi, mfwate goerge bush mlime mazao..|

Sikurupuki uwezo ninao..|
Haters wanaleta chuki, bada ya kuona nimevaa buti za cowboy..|
 
mkuu we ni mbayaaaaaaaaaaaa salute [emoji119]
 
Usiulize mi ni nani..|
Mi ndio yule naepinga muafrika kuitwa nyani..|

Duniani hakuna amani, popote unapotimba hakikisha kiunoni upo na gun..|

Maisha mafupi kama suti ya zakayo..|
Ukiona mjini nuksi, mfwate goerge bush mlime mazao..|

Sikurupuki uwezo ninao..|
Haters wanaleta chuki, bada ya kuona nimevaa buti za cowboy..|

Sina haja ya kukujua man
Kwanini upinge bila hoja evolution is real kama huamini jiulize kwanini mabinti wa karne hii wanapevuka mapema sana yan.../

Vipi unaishi somalia? Mbona sisi wa hazarbe tunaishi tu hakuna machafuko wala shida
Mkononi buyu la maziwa au mbege kiaina../

Maisha mafupi ni kweli maradhi yamezidi
Watu hawana furaha mawazo hasi yamejaa n.k
Hapo kurudi bush ni uhakika tukawape mkono bibi na babu../

Uwezo unao una uhakika? Au
Unahisi unachukiwa, cow boy ni stallion hayumbi kwa vitu vidogo vidogo sasa inabidi uache alama kama cowbama../
 
Tupa biti, nidondoshe mistari..|
Upate ladha ya mziki, kutoka kwa mc hodari..|

Maisha ni safari ya hatari..|
Ukidondoka inuka, ila kumbuka adui yako hatoki mbali..|

Ukipenda vitu vya ghali, jitume..|
Wanaume usiku hatulali, pochi itune..|
Sasa we Legeza suruali, ukunwe..|
mqaxy
 
yo yo yoh
yote nayopitia ni kwasababu sina noti
maadui wamekua wengi kuliko machizi boti

mi husubiri tajiri ale ndipo nikombe sahani
Fid alisema bila hela hupati rafiki maishani

na ghetto sina taa mwezi ndo hunipa nuru
najilinda nisilale njaa kwa uji wa sukari guru

wadeni wangu wameniziba mdomo ili nisiwadai
watesi wangu wameziba promo nionekane sifai
Ila haina noma! haina homa! sikia

nipeni nafasi niendelee kupaza kwenye microphone
mistari yangu ni ya kipekee Ka mtende jangwani
 
Back
Top Bottom