INAUZWA Miche ya kisasa ya matunda inauzwa

Hongera kwa kazi nzuri,

1) Ni dawa gani zinatumika wakati wa kukuuza hii miche lets say kama Papai ,strawbery,maembe,Pasion,Parachichi na mingineyo?

2) Ni matunda ya aina gani hushambuliwa na wadudu mara kwa mara hivyo kuhitaji uangalizi maalum?

3) Je kwa maeneo kama Bagamoyo na Kigamboni unashauri matunda ya aina gani yenye kustawi kwa 100% ukianzia na Ya muda mfupi na muda mrefu?

Nawasilisha
 
Pia ningeomba picha unazoweka ziwe na Name Tag ili iwe rahisi kujua ni tunda la aina gani wengine huku tunaona chengachenga kwa baadhi ya matunda.


#Black passion
 
Safi sana hii.
 
Pia ningeomba picha unazoweka ziwe na Name Tag ili iwe rahisi kujua ni tunda la aina gani wengine huku tunaona chengachenga kwa baadhi ya matunda.


#Black passionView attachment 1673930
Asante kwa ombi lako mkuu,nitalifanyia kazi.Lakini pia kama kuna picha umeshindwa kuelewa naomba uniqoute kwenye picha na page husika ili nikitajie jina sasa
 
1.Dawa ambayo tumekuwa tukiwashauri wateja wetu waitumie kuboost na kuua wadudu inaitwa FARM GUARD,na wamekuwa wakitupa feedback kuwa inafanya vizuri.Lakini pia zipo dawa ambazo pia mkulima anapaswa kuzipiga kwenye miche ili kuondoa ukungu ,ukungu hujitokeza kipindi cha mvua nyingi.
 
2.Hapa naweza kusema miche ya aina zote za matunda,inahitaji unangalizi.Kila mche kwa aina yake unahitaji matunzo na huduma nzuri ili kuleta matokeo yaliyotarajiwa huku ukifuata ushauri tutakao kupa tangu siku ya kwanza unaponunua miche kwetu.Mche wowote utahitaji
a.Mbolea
b.kumwagiliwa
c.kutoa magugu
d.Mwanga wa jua
e.Dawa,pale unaposhambuliwa na wadudu
f.kupunguza machipukizi na kufanya prunning kwa baadhi ya miche n.k
 

3.Asilimia kubwa ya miche yetu ni ya kisasa(zaidi ya 90%),nikiwa na maana kuwa imefanyiwa budding na mingine grafting, ni miche michache sana ambayo ni ya asili mfano,Ukwaju,Zaituni,Tende n.k
Hivyo basi,kigezo cha kwanza tunachokitumia kujua kama Mche wetu wa kisasa aina ya Muembe(mfano)utastawi,tunaangalia je, Bagamoyo ipo.miembe ya asili inayostawi?.Kama jibu ni ndio,basi mche wetu wa muembe uliofanyiwa grafting nao pia utaleta matokeo mazuri.
Sababu grafting ni muunganiko wa mche wa asili na mche wa kisasa.
Hivyo basi,kwa Bagamoyo miche ambayo itakuletea matokeo ni kama Embe,Minazi,Citrus zote(chungwa,chenza,ndimu,limao,balungi),Parachichi,Papai,passion
 
karibu mkuu kwa maswali zaidi
 
karibu mkuu kwa maswali zaidi
Nashukuru kwa kunijibu maswali yangu yote matatu pamoja na nyongeza yake Naona uko serious na kazi yako na unaijua vyema!

Swali : Je strawbery inakubali maeneo ya pwani? Hizo sehemu mbili yani Bagamoyo na kigamboni?
 
Nashukuru kwa kunijibu maswali yangu yote matatu pamoja na nyongeza yake Naona uko serious na kazi yako na unaijua vyema!

Swali : Je strawbery inakubali maeneo ya pwani? Hizo sehemu mbili yani Bagamoyo na kigamboni?
Hii ndio inanipa mkate wa kila siku mkuu,inabidi niwe serious leo kuliko jana😁😁.
Kuhusu strawberry Bagamoyo na Kigamboni zinakubali mkuu.
Strawberry zinastawi zaidi kwenye maeneo yenye joto la wastani,udongo wa tifutifu na wenye rutuba na muhimu zaidi ni upatikanaji wa maji.Hii miche inahitaji sana maji,unashauriwa kumwagilia mara 3 mpaka mara 4 kwa siku
 
Ok fine. Ngoja niandae miundo mbinu then order yangu itakuwa kama ifuatavyo
Papai
Limao
Chenza
Chungwa
Embe
Strawbery.

Je unafahamu ni wapi naweza kupata miti/mimea yenye dawa asili (Siifahamu kwa majina ) Mfano kama Mwarobaini, Mkaratusi, Chaichai and the like coz hii Corona imenipa funzo kubwa sana kwamba hii mimea Ina chakula na dawa za kila aina na muda muafaka wa kuachana na hizi dawa za kizungu.
 
Nashukuru kwa kunijibu maswali yangu yote matatu pamoja na nyongeza yake Naona uko serious na kazi yako na unaijua vyema!

Swali : Je strawbery inakubali maeneo ya pwani? Hizo sehemu mbili yani Bagamoyo na kigamboni?

Karibu sana boss muda na saa yoyote nikuhudumie,niko available 24/7 kupitia Pm na namba zangu za simu.
Mchaichai tunayo pia,kuhusu hiyo miche mingine uliyonitaji usijali inapatikana TTSA(wakala wa mbegu za misitu) huku Morogoro.Ukiwa tayari tutawasiliana ili nikakuchukulie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…