INAUZWA Miche ya kisasa ya matunda inauzwa

Nahitaji miche 50 ya migomba, kimalindi ndefu, nipo marangu, moshi. Kama una miche mingine ya migomba inayozaa mikungu mikubwa na mirefu, nijulishe pia.
Nitumie gharama ya kununua na kusafirisha hadi njia panda ya himo
Karibu tuwasiliane kupitia namba hizi ili kupata maelekezo zaidi
0719527062
0757056472
 
Asanteni Sana wakuu Kwa kuendelea kutuamini.
Karibuni sana
 
Ndio boss, Korosho unaanza kuvuna kuanzia miaka 2-3. Bei ya mche ni 2000 Ila ukichukua kuanzia miche 50 bei ya mche ni 1500. Karibu
Machungwa na maembe yenye miti mifupi unaanza kufaidi matunda kuanzia linii??
 
Naomba ufafanuzi kidogo! GIANT PASSION inatofautianaje na za kawaida?
Ndio boss.
Tofauti ipo kwenye size,giant passion ni kubwa Sana kulinganisha na passion za kawaida.

Pia passion za kawaida zipo kwenye makundi matatu.
1.Red Passion
2.purple Passion
3.Yellow passion

Giant passion zipo za Aina moja tu
 
Machungwa na maembe yenye miti mifupi unaanza kufaidi matunda kuanzia linii??
Embe uzao wa kwanza ni baada ya miezi 7,ingawa uzao huu hauna matunda mengi,unaweza pata matunda 2-5.

Chungwa baada ya mwaka mmoja na nusu.

Karibu boss
 
Utajuaje kama mche ni dume au jike?

Kuna mtu aliniuzia jijini Mwanza, lakini katika miche zaidi ya hamsini, mijike haikufika hata kumi.

Utajuaje?
Kuhusu kujua kama mche wako ni dume au jike at early stage ni ngumu,sababu

1.Kwa muonekano mbegu zote(jike na dume) zinafanana

2. miche pia inafanana
lakini pale mche utakapo fikia hatua ya kutoa maua ndipo utagundua tofauti.
 
Utajuaje kama mche ni dume au jike?

Kuna mtu aliniuzia jijini Mwanza, lakini katika miche zaidi ya hamsini, mijike haikufika hata kumi.

Utajuaje?
Uwepo wa miche dume shambani husaidia uchavushaji,ingawa idadi ikizidi ni hasara na kero,pole Sana mkuu
 
Kuhusu kujua kama mche wako ni dume au jike at early stage ni ngumu,sababu

1.Kwa muonekano mbegu zote(jike na dume) zinafanana

2. miche pia inafanana
lakini pale mche utakapo fikia hatua ya kutoa maua ndipo utagundua tofauti.
Nifanyeje ili kuepuka hilo kujirudia? Nataka nioteshe tena michache.
 
βœ…πŸ™
 
boss apple zinastawi vizuri kwenye mikoa yenye joto kiasi,kiwango kikubwa cha mvua na baridi.
Mikoa kama Mbeya,Arusha,Iringa etc apple zinastawi vizuri.
Masasi ni pwani ,hutapata matokeo mazuri sana hasa kama unalima kibiashara
Hongera Lily Tony. Unajua unachokifanya.

Kwa kuwa umetanguliza huduma mbele badala ya hela, hutakaa ukose hela.

Hongera sana! Keep it upπŸ™
 
Hongera Lily Tony. Unajua unachokifanya.

Kwa kuwa umetanguliza huduma mbele badala ya hela, hutakaa ukose hela.

Hongera sana! Keep it upπŸ™
Asante mkuu kwa kunitia moyo,ujumbe kama huu unanipa nguvu zaidi.Umebariki moyo wangu hakika.

Ungekuwa Moro ningekupatia mche mmoja wa papai,πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…