Midahalo ya wagombea urais kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Membe mtoe hapo maana atamwunga mkono TAL! UNG'ENG'E haiwezekani sisi wengine siyo lugha yetu!

Baba wa Taifa Mwl. Nyerere(RIP) aliwahi kusema, "KIINGEREZA NDIYO KISWAHILI CHA DUNIA LAZIMA TUJIFUNZE"
Huwezi kuwasiliana na Dunia usipojua UNG'ENG'E la sivyo utapata Taabu sana kama Rais Magufuli anavopata taabu sahivi. Haiwezekani Rais ukae Ikulu miaka yote 5 hujawahi kanyaga hata nji 1 ya kigeni...!!Huu Ni udhaifu mkubwa sana kwa Kiongozi yeyote wa Kitaifa duniani...!!!Tusirudie makosa.
 
Mwishoni mwa juma lililopita nilileta mada hapa jukwaani kuhusu Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Bw. Thabo Mbeki, alivyomkumbuka hayati Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Kwenye bandiko hilo, nami nikatoa maneno mawili matatu kumhusu Rais huyo mstaafu Mkapa, kwa jinsi nilivyomjua mimi, kiumbali.

Moja ya mambo niliyoyakumbuka ni ule mdahalo wa wagombea urais wa mwaka 1995 ambapo ndo ulikuwa uchaguzi wa kwanza katika kurudi kwenye mfumo wa vyama vingi.

Nilisema hivi kuhusu ushiriki wa Rais Mkapa kwenye huo mdahalo:
View attachment 1522615

Hilo bandiko linapatikana hapa.

Siku chache baadaye, mwenzetu Bw. Pascal Mayalla akaleta makala ya January Makamba, ya kumkumbuka marehemu rais huyo mstaafu.

Moja ya mambo ambayo Bw. Makamba aliyazungumzia, ulikuwa ni ule mdahalo wa wagombea urais wa mwaka 1995, mdahalo ambao nadhani ndiyo uliomtambulisha vizuri Rais Mkapa kwa umma wa Watanzania.

Katika kumbukumbu yangu, mimi nilisema Rais Mkapa alifanya vizuri sana kwenye huo mdahalo. Licha ya kwamba hakuna kipimo sahihi cha kupima na kuona yupi alishinda, kwa maoni yangu, Rais Mkapa alishinda mdahalo ule.

Na kwa maoni pia ya January Makamba, nadhani ni sahihi pia nikisema hata yeye January aliona kuwa Mkapa alishinda.

Yeye Bw. Makamba alisema hivi:

View attachment 1522626

Kusoma zaidi alichokiandika Bw. Makamba, bofya hapa.

Tokea mwaka huo wa ‘95, nadhani hatujawahi tena kuwa na mdahalo wa kitaifa wa wagombea urais.

Ningependa sana mwaka huu wa uchaguzi tuwe na mdahalo wa wagombea hiyo nafasi. Ila, sitashikilia pumzi yangu kusubiri hilo kutokea.

Lakini pia, nimeona si vibaya kuleta ombi/ wazo hili hapa.

Ombi ama wazo lenyewe ni kuipata video ya mdahalo wa ‘95.

Nimezunguka sana mtandaoni na huko YouTube, lakini nimeambulia patupu.

Pascal Mayalla wewe ni mwandishi wa habari wa muda mrefu. Naamini bado una uhusiano na watu waliomo kwenye vyumba vya habari vya vyombo vya habari hapa.

Sikumbuki vizuri ni stesheni zipi za runinga ambazo zilirusha matangazo ya ule mdahalo. CTN? ITV? DTV? Radio One labda?

Sasa Bw. Mayalla, unaweza kutumia uzoefu na nyenzo zako ulizonazo kututafutia video [au hata audio] ya huo mdahalo?

Mimi si muangaliaji sana wala si mfuatiliaji sana wa stesheni za runinga za hapa Tanzania. Ila kama kuna stesheni ambazo labda zina chaneli huko kwenye YouTube, zinaweza kuipandisha video ya huo mdahalo kwa faida ya umma.

Kama inawezekana, tusaidie Bw. Mayalla...

Shukran jazilan na ahlan wa sahlan.
Salaam.
Ombi limepokelewa.

1. Video za Mdahalo zipo, na video za matangazo yoyote yanayorushwa na TV zote, miaka yote, zipo. Kila kinachotangazwa na TV kinahifadhiwa katika Mifumo miwili ya on air na off air. Anayerekodi on air ni TCRA na makampuni ya monitoring kama Steadman, na wanaorekodi off Air ni TV zilizotusha.
2. Changamoto ya 1 kwa on air recordings ni to find out nani alirekodi besides TCRA?.
3. Changamoto ya pili ni ya kitekinolojia. Ile 1995 Tanzania tulikuwa bado kwenye mfumo wa analogue hivyo kipindi kilirekodiwa kwenye tapes za analogue na whoever mwenye kipindi kimehifadhiwa kwe analogue, kwanza kukipata tuu na kukiona ni issue.
4. Changamoto ya tatu ni jee bado zipo au walifuta. Kama zipo, we can do something, kama hazipo, there is nothing we can do.
5. Ikitokea nikakipata kitakuwa kwenye format ya beta cam SP, kukitransfer into digital format ili kiwe uploaded ni muziki mwingine.
6. Kwa vile nothing is impossible under the sun, let me take up this challenge halafu nita toa progress report from time to time.

Thanks again for thinking of me that I can do this.
P
 
Shukran tena Pascal.

Kama tapes zipo, basi kuzihamishia kwenye mfumo wa kidijitali si shida. Inawezekana.

Naamini unaukumbuka ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Press Club uliofanyika mwaka huo huo wa ‘95.

Kama sijakosea, huo mkutano ulifanyika Kilimanjaro hotel.

Ukiingia YouTube video za huo mkutano zipo. Kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho.

Kama video za huo mkutano wa Nyerere zipo huko YouTube, basi naamini kabisa hata za mdahalo zikipatikana, zinaweza kabisa kuwa formatted kidijitali.

Subutuuuu. Sisi tunatoa orders. Tena mje mtubane na maswali zenyu !!
 
Asante Paskali. Ukiweza kuupata basi utakuwa umetupa zawadi nzuri sana.
 
Shukran tena Pascal.

Kama tapes zipo, basi kuzihamishia kwenye mfumo wa kidijitali si shida. Inawezekana.

Naamini unaukumbuka ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Press Club uliofanyika mwaka huo huo wa ‘95.

Kama sijakosea, huo mkutano ulifanyika Kilimanjaro hotel.

Ukiingia YouTube video za huo mkutano zipo. Kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho.

Kama video za huo mkutano wa Nyerere zipo huko YouTube, basi naamini kabisa hata za mdahalo zikipatikana, zinaweza kabisa kuwa formatted kidijitali.

Ule mdahalo ulimwangusha kwa kiasi kikubwa Mrema. Hakuweza kujenga hoja zozote. BTW midahalo kama huo kila uchaguzi unapofika CCM ndiyo wanakataa kushiriki. Nakumbuka wakati Kikwete anagombea mara zote yalikuwepo mapendekezo ya mdahalo lakini CCM wakakataa. Labda ni wakati wa kuingiza hili jambo kwenye sheria ili kila anayegombea urais asikwepe mdahalo, japo najua litapata upinzani mkubwa kutoka CCM. Mdahalo ni moja ya njia nzuri sana ya kumpima mgombea. Sitaki kufikiria kama kungekuwa na sheria ya kulazimisha mdahalo ufanyike jinsi ambavyo ungekuwa na mvuto wa kipekee kipindi hiki. Na kama ungefanyika kwa kiingereza naweza kuona mtu mmoja ambaye angeshangaza watu sana. Labda kama mdahalo ungekuwa wa kuulizwa swali moja tu la ''what is catalyst?''.
 
CCM hawawezi kukubali presidential debate...Magu atakuwa amejimaliza siku hiyo...maswli kama ya mzee Tido anaweza kutukana kabisa
 
Ule mdahalo ulimwangusha kwa kiasi kikubwa Mrema. Hakuweza kujenga hoja zozote. BTW midahalo kama huo kila uchaguzi unapofika CCM ndiyo wanakataa kushiriki. Nakumbuka wakati Kikwete anagombea mara zote yalikuwepo mapendekezo ya mdahalo lakini CCM wakakataa. Labda ni wakati wa kuingiza hili jambo kwenye sheria ili kila anayegombea urais asikwepe mdahalo, japo najua litapata upinzani mkubwa kutoka CCM. Mdahalo ni moja ya njia nzuri sana ya kumpima mgombea. Sitaki kufikiria kama kungekuwa na sheria ya kulazimisha mdahalo ufanyike jinsi ambavyo ungekuwa na mvuto wa kipekee kipindi hiki. Na kama ungefanyika kwa kiingereza naweza kuona mtu mmoja ambaye angeshangaza watu sana. Labda kama mdahalo ungekuwa wa kuulizwa swali moja tu la ''what is catalyst?''.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huu Mdahalo wa mwaka 2015, Chief Lutayosa Yemba aliuweza vyema. Sijui sasa yupo wapi na sijui kama anaendelea na harakati za kisiasa.
 
Itapendeza pia hata kama mgombea wa CCM hatoshiriki mdahalo [endapo utakuwepo], wagombea wengine wote washiriki na kumzodoa huyo mgombea wa CCM kwa kuogopa kushiriki.
 
Back
Top Bottom