Miezi 30 ya Rais Samia madarakani: Pamoja na kujikwaa kwenye Bandari, bado ni Rais mwenye record bora ya kukuza uchumi wa Tanzania kwa kipindi kifupi

Miezi 30 ya Rais Samia madarakani: Pamoja na kujikwaa kwenye Bandari, bado ni Rais mwenye record bora ya kukuza uchumi wa Tanzania kwa kipindi kifupi

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Unapozungumzia masuala ya kiuchumi, huwa mara zote tunaangalia Zaidi ‘numbers’.
Hongera kwa upembuzi yakinifu kwa takwimu. Tatizo ni kuwa chuki imetamalaki juu ya Dk Samia hutaona watu wakikosoa takwimu linganishi ulizotoa. Utaambulia kejeli kama tulivyoanza kuona kutokana na chuki kwa kiongozi aliyeko madarakani..purely pathetic!
 
Sikibaliani na kusema Rais kajikwaa kwenye bandari na kama.amejikwaa basi amejikwaa Ili kuleta Neema zaidi Tanzania.

Pili sio tuu kwenye uchumi Bali sekta zote hakuna Rais aliyefanya vizuri kama Samia kila.sekta unayoijua wewe rekodi zimembeba mbele zaidi ya watangulizi wake tena Kwa mda mfupi na ndani ya Dunia ya Changamoto.

Yeye Rais binafsi alisema Ukiwa inaongoza Nchi inayoamini mfumo Dume,mwanamke hawezi nk unalazimika kufanya mara mbili zaiis ya waliotangulia Ili kuwajengea Imani wa Sasa na kuwapa Msukumo wanawake siku za baadae.

Mimi binafsi Rais Samia ndio my best president ukitoa Nyerere ambae nae alifeli sana kwenye uchumi ila namheshimu kwa mkujenga Taifa.
 
Vitu vingi Samia alivyofanya alikuwa anamalizia pale alipoishia hayati, kwahiyo hamna jipya atoke tu MADARAKANI.
Wewe ni mjinga sana na hujui unachoongea,nakupa mfano maeneo 2 tuu ,
1.Maelfu ya miradi ya maji Nchi nzima alikuwa anamalizia wapi?

2.Mamia ya miradi ya umwagiliaji Nchi nzima alikuwa anamalizia sehemu gani?

Mwisho anaemalizia anaweza kufanya mara 2 Kwa miaka 2 kushinda aliyekaa labda miaka 5 au 10?

Unajua Samia anajema shule ngapi kuanzia Primary Hadi A level? Unajua anajenga Veta ngapi Tanzania hii? Unajua anajenga universities ngapi Nchini?

Hiyo ni Kati ya mifano Mingi sana nayoweza kukujazia seva za jf Bure.

Hakuna Rais wa kumlinganisha na Samia kwenye delivery kwa.waliopita hayupo Kwa taarifa Yako.
 
Uzi wako ni mrefu.

SWALI: Unadhani ni kwa nini yule muhalifu mmoja aliyesulubiwa pamoja na Yesu pale Golgota,alipoomba akumbukwe kwenye ufalme, tena siku ya mwisho baada ya kufanya uhalifu mwingi, aliahidiwa kuuona huo ufalme wa mbinguni? Tuliza akili na uelewe swali.
 
Vitu vingi Samia alivyofanya alikuwa anamalizia pale alipoishia hayati, kwahiyo hamna jipya atoke tu MADARAKANI.
Huwa najaribu sana kuangalia logic ya hicho ulichosema. Kwa taarifa yako, nimefanya utafiti mwingi sana wa kuchambua uchumi wa Tanzania.

Ila nasikitika kwamba, conclusion ambayo huwa naipata ni kwamba Magufuli hakuwa mzuri sana kwenye private sector.

Nimekwepa kumsema Magufuli kweny uzi kwasababu namba zinaongea wazi. Usilazimishe kunilisha mihemko, wewe kama unasema mtangulizi wa Samia alifanya maajabu. Leta takwimu tupambane.

Mi sio mtu wa siasa na maneno, lata namba.
 
Ila bahati mbaya ni kwamba Watu hapa Africa Huwa hawachagui Viongozi Kwa hoja na matokeo ya msingi Bali bila sababu za msingi na ujinga ujinga mwingine.

Ndio maana vyombo vyeti vinatakiwa kumlinda Rais Samia Kwa gharama yeyote hadi 2030 ataivusha Nchi.

Rais Samia sio mtu wa porojo na maneno meengi ya propaganda Bali ni mtu wa matokeo yaani aina ya Viongozi wa mbele huko ambao wanazungumzia issues zaidi badala ya porojo na propaganda za Kiafrika.

Muulize mbunge yeyote au sehemu yeyote kwamba Kuna kipindi kumewahi kuwa na miradi Mingi kama awamu ya 6 ,watakupeni majibu.
 
Ktk hili hata Yeye mwenyewe aweza kukubishia!!!

Pesa ni MTU, ameamua kuficha dollar!!

Twende KAZI!!!
Ukisoma uzi mpaka mwisho utapata picha ni kwanini dola imeadimika. Napinga hii hoja ya kusema Rais kaficha dola.

Kama wewe ni great thinker, achana na fikra za namna hii. Usichangie tu kwa sababu una bando, angalia na maana ya unachokichangia kwenye mada.
 
Ukisoma uzi mpaka mwisho utapata picha ni kwanini dola imeadimika. Napinga hii hoja ya kusema Rais kaficha dola.

Kama wewe ni great thinker, achana na fikra za namna hii. Usichangie tu kwa sababu una bando, angalia na maana ya unachokichangia kwenye mada.
Rudia kusoma, usikurupuke!!!

Nimesema pesa/Fedha ni Mtu, Mtu huyo ameficha dollar!!!

Uliza tena nikujibu Fedha ni Mtu kivipi!!!
 
Back
Top Bottom