Miezi mitatu nimetotolesha vifaranga 500 vya kuku wa kienyeji

Asante sana kwa darasa, naomba kujifunza utaalamu wa kuchanganya chakula kwa kuku wa kienyeji ili kupunguza gharama
 
Nzuri sanaa mali inapatikana shambani hii ndo maana yake.
 
Hongera Sana Mkuu Haya ndo mambo nayopenda kuyasikia Usisahau Tu Kumrudishia Mungu Kadiri ya Wema alokutendea kwa Mwaka ulopita
 
Kuku wa kienyeji jau sana
Mara wanakula mayai
Wanagombania sehemu ya kutaga na nimetenga sehemu nyingi

Majogoo yanapigana
Mara vifaranga kukanyagwa

Dawa ni mashine tuu ya kutotoleshea
 
Bila picha na video sasa sisi tutaamini vipi huu ufugaji wa pdf?
 
Nifanyaje nitoboe?
Kuna kuku ambao ni maalumu kwa ajili ya utotoleshaji vifaranga (PARENTAL STOCK) sasa Hawa kuwapata huwa ni issue, kuku wakwanza akishatotoa , nahuyo kifaranga akija kua mkubwa nae akaanza kutaga akitotoa vifaranga mara nyingi huwa haviwi imara, Kinga yao ya mwili inakua dhaifu natural.

Tafuta parental stock ndio wawe maalumu kwa ajili kutaga mayai kisha utotoleshe vifaranga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…