Mifumo ya kidunia ilishaamua mwanaume aishi kwa kukandamizwa na kufanyiwa ulaghai/ udanganyifu

Nikushukuru kwa kujitahidi kufafanua, sasa tuachane na sheria inavyosema ambayo ni kandamizi kwa wanaume, chukulia wanandoa hawana mtoto na mke alikuwa mama wa nyumbani, tukiachana namlipa kwasababu gani? Kisa kupika na kunipa K? Nahuku ni majukumu yake kama mke, mlitaka hizo huduma nizipate wapi? Ninachoshauri ni kila mmoja aondoke na alichokuja nacho au alichonunua, haina mantiki kumlipa mtu nahuku alikuwa anatimiza majukumu yake kama mke, kama mimi nilivyokuwa natimiza majukumu yangu kama mume (ambayo unakwepa kuyazungumzia kana kwamba hayana umuhimu)

Halafu mke akifanya kazi, pesa zake bi ngumu kupata, anatuma kwao kimya kimya, nyie wanawake hampendani hata wenyewe kwa wenyewe, itakuwa kumpenda mwanaume?
 
Mahari siyo kumnunua mwanamke wala haina uhusiano wowote na mke kuwa mtumwa wa mume, kama hamtaki kutoa mahari basi mfute utaratibu wa watoto kutumia majina ya ukoo ya mume bali watumie majina ya koo zote mbili, maana kwa tamaduni zetu hiyo ndiyo sababu kubwa ya kutoa mahari
 
Kwani wanawake wengi hasa wa kiafrika tena hawa mabinti wa kileo sio omba omba ?
Siyo omba omba ni mgawanyo wa majukumu tu, siku wanaume mkianza kuyachukulia majukumu ya wanawake kama yenu, basi hata nao wataanza kuyachukulia majukumu yenu kama ya kwao
 
Nguvu ya mwanaume ipo katika kuoa wake wengi. Mila ya kiafrika iliyoachwa
 
Tamaduni zenu wewe na nani ?
 
Siyo omba omba ni mgawanyo wa majukumu tu, siku wanaume mkianza kuyachukulia majukumu ya wanawake kama yenu, basi hata nao wataanza kuyachukulia majukumu yenu kama ya kwao
Majukumu gani hayo yanayo fanya kuwa ombaomba ?
 
Mkuu mbona nimeshakuelezea kwamba katika mazingira ambayo mke ni mama wa nyumbani na hamna watoto, mkiachana mke atapewa mali kwa hicho kigezo cha kufidia muda wake ambao alitakiwa atafute pesa kama wewe lakini akawa anatimiza hayo majukumu, sawa ni majukumu yake lakini ndio ukubali sasa kwamba siku mkiachana lazima mtagawana mali kwa hicho kigezo

Vinginevyo msiachane au usifanye makosa makubwa ya kumfanya yeye atake muachane, wangesema kila mtu aondoke na alichokuja nacho ingekuwa ni uonevu kwa wanawake ambao ni wamama wa nyumbani, kwa sababu huwezi kumkataza mtu asitafute pesa akae nyumbani akuhudumie halafu eti mkiachana usimpe chochote wakati ni wewe ndio ulimzuia asitafute pesa

Hayo ya mke kufanya kazi halafu asichangie pato la familia nalo haliwezi kuwa utetezi wa kuaminika, kwa sababu mwanaume yeyote tu anaweza akatumia huo utetezi hata kama ni uongo ili mradi tu mkewe asipate chochote, huwa wanaamini haiwezekani katika muda wote ambao mmeishi na huyo mke eti awe hajawahi kuchangia chochote kwenye familia lazima tu kuna sehemu naye alichangia

Kuhusu hayo ya wanawake kutokupendana nazo ni propaganda kama propaganda nyingine kwa sababu ukiangalia hali halisi mazingira ambayo yanafanya wanawake waonekane hawapendani, utakuta ni mazingira ambayo hata ingekuwa ni wanaume nao wangefanya hayo hayo ambayo wakifanya wanawake wanaonekana hawapendani, labda wewe uniambie ni katika mazingira gani ambayo wanawake hawapendani na ni kwa sababu ya kufanya vitu gani

Halafu siyo kwamba majukumu ya mwanaume hayahesabiki au hayana umuhimu ila kumbuka jukumu lenu pekee hasa wanaume wa kiafrika ni kutafuta pesa tu, sasa niambie ni pesa kiasi gani inayoweza kulingana na majukumu ya kufanya kazi za nyumbani, kutii mume, kubeba mimba, kuzaa, kunyonyesha, kulea watoto nk sasa hata kama utakuwa unamhudumia utakuwa unampa pesa kiasi gani ya kufidia majukumu yote hayo
 
Tamaduni za kiafrika

Majukumu ya mwanamke ni yapi
Sidhani hata unajua unacho tetea au wajiandikia tu.

Tamaduni za kiafrika una generalize tu mambo.

Hebu tuliza kichwa na ujibu nacho kuuliza
 
Mwanaume kama huna akili timamu na ya kiume ndo utayumbishwa......tofauti na hapo hakuna la kunitisha...
 
Kama umeshindwa hoja sema acha hizi porojo za kusema napenda ligi, wewe ungekuwa hupendi ligi tusingefika hapa ungeshaacha kunijibu tangu mwanzo, kufika hapa maana yake wote tumebishana by the way kwani niliyoyaandika ni uwongo
Haya umeshinda mkuu
 
Sidhani hata unajua unacho tetea au wajiandikia tu.

Tamaduni za kiafrika una generalize tu mambo.

Hebu tuliza kichwa na ujibu nacho kuuliza
Ndio hivyo kwa tamaduni za jamii nyingi za kiafrika mahari ni kama fidia kwa familia ya mke kwa kulose ilihali ya mwanaume imegain, unaweza kuamua tu kukataa ila wewe kukataa haibadilishi ukweli wa hilo jambo, mahari siyo kumnunua mwanamke wala haihusiani na mwanamke kuwa mtumwa wa mumewe
 
Hajui anasupport nini uyo jamaa. Yeye anachotaka ni kuoneshana umwamba tu tu ndani ya nyumba
 
Kwahiyo kutolewa mahari ndo unarejea utamaduni, ila mke kuwa submissive kwa mume pmj na kufanya kazi za ndani, tukikwambia kuwa nao ni utamaduni wa kiafrika unapinga, unahoji eti ni nani anayeamua kuwa gender roles za mwanamke ni hizi na za mwanaume ni hizi.
 
Hatushindani tunajadili hoja
Wewe unataka mashindano. Ndio maana nimeona nikuache labda hao wengine wanaweza kukuelewesha. Hivi unajua kwann hata wanawake hawajitokezi kwenye comments? Wanajua hoja imewapiga kwenye mshono hawana cha kuchangia vinginevyo wangeshakuja kutapika hapa.
 
Ndo ujibu sasa huo muda wa kumlipa mwanamke kama fidia una mantiki gani nahuku kiutamaduni ni jukumu lake kufanya kazi za nyumbani? Mbona umesema vzr tu jukumu letu ni kutafuta pesa, basi jukumu la mwanamke ni kazi za nyumbani, halafu unadharau hizo pesa anazotafuta mwanaume nahuku tunahudumia familia tatu, ya mke wangu, familia niliyotoka, pamoja na familia ya mke wangu mizinga napigiwa? Unahesabia mke tu?

Kwahiyo kwenye ndoa mwanaume hana mchango wowote mpaka mali zake zipokonywe na asipate fidia yoyote pale wanapoachana? Narudia tena usirejee sheria za kitapeli ambazo ni kandamizi kwa wanaume, ongea uhalisia, eti mwanamke anakazi kubwa kubeba mimba na kulea, kwahiyo ukitaka mwanaume ndo abebe mimba? Si ni asili Mungu kaumba watu hivyo?

Maswali hayo mawili kuhusu mantiki ya kumlipa mwanamke kisa kazi za ndani nahuku ndo jukumu lake ni lipi? Mchango wa mwanaume kwenye ndoa kwanini hauhesabiki? Aya hii ya mwisho ndo summary ya maswali niliyouliza tangu jana unakwepa hujibu, jibu sasa bila kuandika gazeti ambalo halina hoja za msingi.
 
Ni kweli. Hapa solution ni kukataa ndoa tu.
 
We are challenging those stereotypes, nikutengee chakula maana yake nitoe vyombo nioshe. , don't you know this is TIME??? Kwa nini mnakataa mtu asilipwe 50 baada ya huu utumwa????? ..kubali hizo gender role zinamkandamiza mwanamke, and recognising this hence malipo ya 50/50 yanawekwa in place sasa ndio useme sasa ulitumia muda lini kufukuza mwizi na mara ngapi katika mahusiano yenu....

Anyway ulisema mwanamke kumtii mwanaume ni gender role nakuuliza ulikua unamaanisha nini, maana nilidhani umemaanisha wanawake ni weaker beings ila ukanirudisha ni respect nikakwambia ni reciprocal sasa hivi naona unanirudisha kwenye tamaduni za kiafrica, hizi zinazokandamiza wanawake all in the name of gender roles...????? Please ulikua unamaanisha nini unaposema mwanamke kumtii mwanaume ni gender role ili twende sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…