Nikushukuru kwa kujitahidi kufafanua, sasa tuachane na sheria inavyosema ambayo ni kandamizi kwa wanaume, chukulia wanandoa hawana mtoto na mke alikuwa mama wa nyumbani, tukiachana namlipa kwasababu gani? Kisa kupika na kunipa K? Nahuku ni majukumu yake kama mke, mlitaka hizo huduma nizipate wapi? Ninachoshauri ni kila mmoja aondoke na alichokuja nacho au alichonunua, haina mantiki kumlipa mtu nahuku alikuwa anatimiza majukumu yake kama mke, kama mimi nilivyokuwa natimiza majukumu yangu kama mume (ambayo unakwepa kuyazungumzia kana kwamba hayana umuhimu)Nilishakueleza sababu za mgawanyo wa mali yaweza moja kati ya hizi au zote kwa pamoja
Kuchuma mali pamoja
Kama mkeo atakuwa anafanya kazi basi maana yake utakuwa haumhudumii, na lazima kuna bills za hapa na pale alikuwa anakusaidia kwahiyo inahesabika kama mmechuma wote, hivyo mkiachana mtagawana mali kwa hicho kigezo
Mke kufanya majukumu ya nyumbani na kulea watoto
Hayo majukumu ya mke yanakuja na wajibu juu yake ya kumhudumia, kwa sababu huo muda anaoutumia kufanya hayo majukumu alitakiwa naye awe anatafuta pesa, ili siku mkiachana awe na kitu cha kuanzia maisha
Kubaki na watoto
Ndoa nyingi watu wakiachana mke ndio hubaki na watoto, ambapo ataendeleza gurudumu la malezi huku mwanaume akiwa free tu, sasa unataka huduma za watoto nani ahusike nazo
Wajibu wa mke kwa mumewe
Tamaduni zetu zinaamini kwamba mwanaume anapooa basi mke kazi yake ni kuhakikisha anamlea, anamtunza, anamliwaza na anamfariji mumewe pale anapokuwa na msongo wa mawazo, hiyo inamfanya mwanaume apate moyo na awe na juhudi zaidi ya kutafuta pesa, ambapo wanaamini mke asipofanya hayo basi mume utafutaji wake utakuwa wa kusuasusua
Sasa whether huko ndani ya ndoa mke alikuwa anatimiza hayo au hatimizi hilo haliwahusu, wenyewe wanaassume kwamba mwanamke aliyeolewa lazima anatimiza hayo majukumu ambayo kwa namna moja au nyingine, lazima tu yatamfanya awe na haki ya kugawiwa nusu ya mali zilizopatikana ndani ya ndoa
Sasa kwa mantiki hiyo wewe ulitaka ufidiwe nini hapo au labda nikuulize kama mwanamke alikuwa hatafuti pesa na alikuwa anatimiza majukumu yake, siku mmeachana hana pesa wala mali wala kazi wala biashara unategemea anapata kipi cha kufidia muda ambao alitakiwa atafute kama wewe, by the way nenda kasome sheria za ndoa na mgawanyo wa mali mimi mwenyewe siko kwenye ndoa but atleast nafuatilia baadhi ya mambo na najaribu kukuelezea katika uhalisia wake ila wewe unajadili kwa mihemko na kulazimisha assumptions zako ndio ziwe sahihi
Halafu mke akifanya kazi, pesa zake bi ngumu kupata, anatuma kwao kimya kimya, nyie wanawake hampendani hata wenyewe kwa wenyewe, itakuwa kumpenda mwanaume?