Mifumo ya kidunia ilishaamua mwanaume aishi kwa kukandamizwa na kufanyiwa ulaghai/ udanganyifu

Mkuu hayo yote yanafahamika.
Huko sie hatupingi,tunapopapinga sisi ni wanawake kujitegeza na kuplay victim kisa wao wamepewa kipaumbele.
Embu mchukulie mfano mke wa Ashraf Hakimi,hakuna sababu ya kudai talaka kadai talaka na kutaka mgawanyo wa mali.
Mwanamke kisa yeye kapewa kipaumbele ya kutetewa basi ule utetezi huutumia vibaya.
Kuna kisa kimoja ngojea nikupe kusadikisha hili.

Kuna siku nilienda serikali za mitaa Kigamboni Kisiwani nikakuta kesi ya dawati la jinsia.Yule binti akikua anadai mwanaume kamzalisha na hamuhudumii yeye na mtoto,jamaa aliitwa hakubishana akakubali kutoa matumizi kila siku akipeleka 10k ya matumizi.

Jamaa chumba alimuachia mwanamke maana maelewano yalikatika akarudi kwa mamaake.
Binti kuona kaachiwa chumba akaanza kuishi na bwana wake mwingine huku bado akidai matumizi.
Jamaa akaona hapana sio kweli,aliamua awe anamchukua mtoto anampeleka kwa mama ake anashinda na kula kesha anamrudisha kwa yule binti akiwa na 3k ya chai tu asubuhi.
Binti karudi dawati la jinsia akidai mwanaume haleti matumizi anamuacha mtoto na njaa ilhali hapo hapo KAACHIWA CHUMBA AKAAMUA KULETA BWANA NDANI.
Hii wewe unaichukuliaje???

Achana na hiyo,kuna jamaa alisafiri kurudi akakuta mkewe kaingiza mchepuko.Jamaa kapaniki na kuanzisha varangati,mkewe imagine mkewe kamuitia jamaa mwizi watu wakaanza kumpiga tena vingunguti,bahati nzuri wakatokea wanaomjua na kusema huyo anaepigwa ndio mume halisi sio mwizi.
Ukitizama hii mifano miwili utakuja kugundua WANAWAKE MASHEITWANI YA KUKUBUHU.
TENA YANAWEZA KUKUANGAMIZA HUKU YANACHEKA KWA KUJIFICHA NYUMA YA MGONGO WA HAKI SAWA KWA WOTE.
Yani hata kama mkosaji ni yeye akienda kulia mahakamani umemuonea BABA HAUSIKILIZWI UNAHUKUMIWA DIRECTLY.

Ndio maana mimi nimekosa huruma kwa hawa viumbe,waliokutana na mimi wanajuta kunifanyia ujinga maana NILIWASULUBU KWA KUWAACHIA KOVU LA MAISHA.
 
MKUU 💯 shida ni wanaume kujitoa kupita maelezo ndiyo ina pelekea anguko letu.
 
Bro ukatili wa mwanaume uko wazi na unaeleweka na pia wanaume wamewajibishwa ipasavyo.
Pia tunafurahi mwanamke kutetewa na kupewa kipaumbele na mfumo dume kupigwa vita.
Ila hiyo nafasi ambayo mwanamke anapewa aitumie vizuri basi,asitumie kufanya ujinga na uzandiki kisa eti anasikilizwa.
Yani wanawake wa sasahivi ni sawa na kiongozi anayetumia madaraka vibaya(dictator).

-Yani kisa mwanamke eti akizaa nje kitanda hakizai haram mie nilee??
Mbona sie wanaume tukizalisha nje tunaitwa WAHUNI,MALAYA,WALETA MAGONJWA n.k n.k?
-Haki sawa kwa wote mbona tukitalikiana mali ya mwanamke marufuku kugawanywa ila ya mwanaume lazima kugawanywa hata kama mali mwanaume katafuta peke yake??
Ukiuliza eti sababu mke alikua akikufunulia chupi,kwani raha akiwa hapati nikiwa napata pekeangu?
Ukiuliza eti alikua anahudumu familia nyumbani wewe ukawa wapata utulivu,ilhali WANAWAKE WA SIKU HIZI WANAKWAMBIA "MIE MKE SIO HOUSEGIRL UTAFUTE HOUSEGIRL HUNIFANYISHI MIKAZI YA NYUMBANI".
-Kisa yeye mwanamke kwanini aplay victim ya ukandamizaji??
Bro leo hii mpandishie sauti kidogo mkeo akienda polisi akishtaki akidai umempiga aisee hatopimwa wala kudaiwa ushahidi utaswekwa ndani na virungu juu ilhali hujamfanya chochote.
Kuna jamaa yangu mkewe ndio kamkosea kumfokea mke akaondoka kilio na kusema jamaa kamuomba ndogo mke kakataa jamaa kampiga.Jamaa hakusikilizwa kawekwa ndani na kipigo na faini juu.

KUNA MAHALI MWANAUME ALIWAHI PLAY VICTIM?????
MWANAMKE NI SHETANI ANAEONEKANA NARUDIA TENA MWANAMKE NI SHETANI ANAEONEKANA.
 
Hii ni karma ya wale babu zetu walikokua wanawanyanyasa wanawake, nature huwa inatunza kumbukumbu na kulipa kwa wakati ,wanawake na nao wasipo utumia huu wakati kwa hekima baadae na wao watakuja lalama tena .
 
Akuna anae onewa zaidi ya mtoa mada mkuu.
 
Tatizo imeshaonekana haiwezekani kusikiliza pande zote mbili kwa sababu kila upande unataka lake, lakini ukiangalia hali halisi kuna upande ambao ni kweli unaonewa na kuna upande ambao wenyewe unaona ni haki yao kufanya makosa, kikubwa ni kutenda haki na kuhakikisha kila upande unakuwa na furaha na siyo upande mmoja ulazimishwe kusacrifice furaha yake kwa ajili ya furaha ya upande mwingine
 
Utafika muda na mwanaume atachoka nae atajibu mapigo, na hii haipo mbali, mjadala huu ni ishara kuwa wanaume wameanza kuelewa lengo sio 50/50 ila ni kumzalilisha mwanaume.
Wala hakuna anayewadhalilisha ila ni inferiority complex yenu au naweza kusema mnajidhalilisha wenyewe tu yani haiwezekani kosa ni lako halafu unayemkosea akichoka kuvumilia unamlaumu, kama unajua kusoma alama za nyakati basi utagundua njia wanayoitumia wanawake kujibu mapigo ni kutafuta namna ya kuwa na furaha bila ndoa, sasa ninyi mtakapojibu mapigo sijajua mtakuwa mnamkomoa nani hapo maana zile fimbo zote mlizokuwa mnawachapia wanawake taratibu wameanza kuzikata
 
Mkuu hivi kwa kuangalia uhalisia tu toka enzi na enzi kati ya mwanaume na mwanamke ni nani anayetumia nafasi aliyopewa vibaya, je siyo ninyi mnaowasaliti na kuwanyanyasa wake zenu kwa kisingizio kwamba mnawahudumia na huku ikionekana ni kawaida kwa wanaume, hebu soma tena ulichoandika hivi leo hii mwanaume na mwanamke wakichepuka au wakichelewa kuingia kwenye ndoa au wakiachika kwenye ndoa au wakipata watoto nje ya ndoa nani anayeitwa malaya
 
Mkuu unaenda nje ya mada aisee.
HIlo halipingiki usemalo.
Kiufupi ni wanawake ku play victim.
Labda nikuulize maswali matatu:
1)Hivi ni sahihi mwanamke akipata mtoto wa nje mwanaume kwake afunike kombe mwanaharam apite(kitanda hakizai haram),wakati huo huo mwanaume akizaa nje ya ndoa anaitwa MZINZI,MVUNJA FAMILIA NA MLETA MARADHI NA MALAYA??Je hii ni sahihi??
2)Kuna age or era yeyote wanaume tuliwahi play victim na kuwa wazandiki?
3)Je ni sahihi kumhukumu mwanaume directly kwa kusikia malalamiko ya mwanamke pasi na kuthibitisha??

Kama ni 50/50 haki itendeke kote na wanawake waache ku play victim.
Mwanaume mfumo dume wake ulikua directly na easy to tackle,ila mwanamke sawa na sumu baridi yani anakufanyia unyama akidai kuwa ni haki.

Hii mada ya leo imenifanya niongee kimihemko sana kwasababu hawa viumbe hawa aisee basi tuu.
Wanaweza kukuharibia maisha kwa namna ambayo huwenda usiinuke tena maisha yako yote.
 
Hujapata point yangu.
Mwanaume akifanya kosa huwa directly hufikiwa na kushurutishwa.
Mwanaume akipata mtoto nje ya ndoa kipindi ana mke ataitwa malaya,sio muaminifu tena hata ukimshitaki na kuhukumiwa anaweza hukumiwa.
Ila KWANINI mwanamke akizaa nje amafanyiwa cover up na kudai kitanda hakizai haram??
Kwanini hii kitanda hakizai haram na mwanaume asitafutiwe favor??
Mwanamke kulea mtoto wa mwanamke mwenzake unyanyasaji na dharau ila mwanaume kulea mtoto wa mwanaume mwenzake sawa??

Mwanaume toka enzi sawa katumia mabavu ila kawajibika kwa kila maamuzi.
Ila mwanamke anajitegeza sanaaa.Hayajakukuta bro ndio maana unaongea.Violence ya mwanaume inaeleweka mabavu ama utumiaji nguvu.Ila mwanamke anaweza kukufanyia jambo ukilitafakari unajiuliza awali yake nini.
Unaweza kuniambia bro sababu ya Mke wa Hakimi kudai talaka na kutaka mgawanyo wa mali pasu kwa pasu ilhali kamkuta Hakimi mali kajitafutia mwenyewe????
Hakuna sehemu mwanaume anakosa kuwajibishwa kwa makosa yake,ila cha ajabu mwanamke akitenda makosa ya mfanano huo HAWAJIBISHWI BALI ANATAFUTIWA HURUMA.
 

Mkuu mimi hata sielewi unaishi kwenye jamii gani hiyo ambayo kwenye mahusiano au ndoa mwanaume akifanya kosa anatukanwa ila mwanamke anapendelewa maana kwenye jamii za kiafrika vice versa ndio uhalisia

Je ni jamii hii hii ambayo mwanamke anaitwa single mother na kudhalilishwa na kuambiwa kuwa hafai kuolewa ila mwanaume haitwi single father na kwake ni sawa tu kuoa

Je ni jamii hii hii ambayo mwanaume kuwa na wanawake wengi inaonekana kawaida na tena unaambiwa kabisa hakuna mwanaume malaya ila mwanamke akiwa na wanaume wengi ndio malaya

Je ni jamii hii hii ambayo mwanaume akichelewa kuoa hata akifika miaka 50 hakuna anayemtukana ila mwanamke akifika miaka 30 tu bila ndoa anaonekana katumika sana na hafai kuolewa kabisa

Je ni jamii hii hii ambayo mwanaume na mwanamke wakiachana kwenye ndoa siku zote anayeonekana mbaya na ndio chanzo ni mwanamke huku mwanaume akionekana innocent

Wewe unasema wanaume hawajawahi kuplay victims kwani hiki mnachokifanya kwenye dunia ya leo ni nini kama siyo kuplay victims, siku hizi wanaume mnalalamika sana asee yani ni kama vile mmepokea mic kutoka kwa wanawake, na sasa ni zamu yenu ya kuchana mistari ya malalamiko

Hayo unayoyalalamikia wewe kwamba wanawake wanatetewa kuzaa nje ni mawazo tu ya watu binafsi siyo sheria kusema kwamba ni lazima mtu aifuate, ukiamua unaweza ukamuacha huyo mkeo na hakuna atakayekufanya kitu mbona watu wanaachana kila siku kwa sababu kama hizo, ni kama tu baadhi ya watu wanavyotetea wanaume kuchepuka na wengi husema kumuacha mume sababu ya kuchepuka ni sawa na kukimbia nchi sababu ya mvua
 
Una akili sana, tuunde chama cha kimataifa cha kutetea haki za wanaume.
 
Sasa kutafuta furaha kukataa ndoa ?!
Maana yake una enda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu aliye kuumba. Sijui kama ume elewa. Unaweza vipi tafuta furaha kwa kukataa ndoa ebu nijibu hapo ?!
 
"Tatizo imeshaonekana haiwezekani kusikiliza pande zote mbili."
Hivi ndivyo jinsi ulivyo andika, kwamba haiwezekani.

Sasa mbona hapa chini umenijibu tena kwamba lazima kutenda haki pande zote mbili

"kikubwa ni kutenda haki na kuhakikisha kila upande unakuwa na furaha na siyo upande mmoja ulazimishwe kusacrifice furaha yake kwa ajili ya furaha ya upande mwingine"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…