enzo1988
JF-Expert Member
- May 26, 2018
- 1,838
- 7,346
Usiku wa leo, jeshi la anga la Israel lilifanya mashambulio kwenye maeneo mbalimbali hasa maeneo ya kijeshi yakiwa ndiyo lengo kuu.Zaidi ya ndege mia moja (100) zinadaiwa kutumika kwenye mashambulio hayo!
Mara baada ya mashambulizi hayo kumalizika,taarifa mbalimbali zimeanza kutoka kupitia vyanzo mbalimbali!
Ukweli nguvu iliyotumika na madhara yake ni tofauti na ilivyotarajiwa na wengi! Madhara ni madogo mno kulinganisha maandalizi na nguvu kubwa iliyotumika! Hii imewashangaza zaidi wataalamu wa masuala ya kijeshi!
Iran ilisema mfumo wake wa ulinzi wa anga ulifanikiwa kukabiliana na mashambulizi ya Israeli kwenye maeneo yake ya kijeshi katika majimbo ya Tehran, Khuzestan, na Ilam, na kusababisha "uharibifu mdogo" katika baadhi ya maeneo.
View: https://twitter.com/worldupdates245/status/1850047504559091900
Wenyewe wametoa visingizio kama hiki kimoja wapo!
Afisa mwandamizi wa Marekani alisema kuwa Rais Joe Biden na timu yake ya usalama wamekuwa wakishirikiana na Waisraeli katika wiki za hivi karibuni kuhimiza Israel kufanya mashambulizi yenye hatari ndogo kwa raia na hicho ndicho hasa kilichotokea jioni ya leo.
Source: Reuters