IRAN wana mifumo bora ya ulinzi shambulizi la ISRAEL limefeli pakubwa!!
Yaani hata nzi hajafa, hakuna majeruhi wala uharibifu wowote hakuna raia alokwenda kwenda mahandaki
Hakuna nchi iloenda kumsaidia Iran kama ambavyo Israel alisaidiwa na nchi 30 kuyatungua makombora ya Iran siku zilizopita
Hili shambulizi la Israel limeonyesha udhaifu mkubwa kwa dola la Israel dhidi ya Iran
We imagine Iran katumia mfumo mmoja tu wa Bavar 373 kuzuia makombora yote jamaa wametungua yote 99.99%
Kamlipuko kadogo kalionekana karibu na barabara baada ya kombora la mfumo wa ulinzi wa makombora ya Iran kufail na kulipuka.
Nimeshangazwa na Waajemi, kweli hawa sio waarabu kabisa pamoja na vikwazo vyote lakini wameprove kuwa wana mifumo bora ya ulinzi kabisa!!
Sote tunafahamu mashambulizi ya Israel huwaga ni makubwa na yenye kuleta madhara, Gharama ya kutuma ndege 100 kwenda kupiga tehran iko wapi?Maana wameishia kurusha makombora tu yakadakwa yote na Iran
Halafu hamna raia wa Iran alokwenda kwenye mahandaki hata mmoja tehran walikua walikua tuli wamelala zao!! Wakati huko Israel huwa watu hawalali ni kukaa kwenye mahandaki tu.
Hili tumejifunza nini kama taifa la Tanzania!! Hili shambulizi la Israel limejidhihirisha na kuonyesha Israel level zake na Palestina na Lebanon tu na siyo level za Iran
Gharama walotumia Israel kuishambulia Iran wangeitumia kulipua kambi za Iran huko Syria ingeleta ufanisi, lakini kitendo cha kwenda Iran na kushambulia na kutoka kapa ni aibu kubwa
My take: Iran haijaribiwi, shambulizi la Israel limefeli pakubwa, nakumbuka iran ilivyoshambulia Israel April 2024 Israel ilijibu kwa kutuma drone mbili huko Isfahan na zikaishia kutunguliwa.Israel kwa muajemi bado sana ana miaka mingine 200 ya kujipanga kumfikia muajemi!!
View: https://x.com/Nadira_ali12/status/1850005156286390481?t=tmz64j7ABD3MsCsLHC-nxg&s=19