ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
- Thread starter
-
- #161
Hakika unakuta mwanamke namlamba kamasi mwanaume maana hana optionJamii zote ambazo wanawake ni tegemezi sana kwa wanaume na ni za kidini sana, GBV iko juu, wanawake wanapigika, wanachapika haswa na kuuwawa zaidi. Iwe katika mahusiano au ndani ya ndoa kabisa.
ni muhimu na ni vizuri sana kua waaminifu, wastahilivu na wenye subra sana kwenye ndoa au mahusiano yoyote yale, vinginevyo mtajisogezea vita na mafarakano yanayoweza kupelekea mauti miongoni mwenu, kwa furaha ya muda mfupi tu.🐒Angalizo msomaji wangu bandiko ni refu kidogo
Naomba uwe mvumikivu katika usomaji wako
Karibu sana kwenye mada 😊
Hello Great Thinkers 🫡
Katika pita pita zangu huko IG nimekuta kuna dada mmoja amepost kuhusu vifo vinavyotokana na migogoro ya kimahusiano hapa Tanzania 🇹🇿
Nimekuwa shocked baada ya kuona takwimu zinaogopesha na kushangaza
Ikanisukuma niende kwenye mtandao ku search na nione hali ilivyo kwa kujihakikishia mimi tomaso nimeshtushwa
Sikujua hali ni mbaya kwa ukubwa huu!
Nimepigwa butwaa
Hali inatisha
Chanzo cha takwimu (LHRC Tanzania)
Niweke sawa hapa
Hizi takwimu ni kati ya mwaka 2019_2023
Hebu tuangalie hizi takwimu za mauaji yanayohusisha wenza wa kimapenzi Tanzania
2019: LHRC ilirekodi wanawake 12 waliouawa na waume/wenza wao ambapo 8 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
2020: LHRC ilirekodi wanawake 32 waliouawa na waume/wenza wao, ambapo 23 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
Hii ilikuwa zaidi ya mara mbili ya matukio yaliyorekodiwa mwaka 2019
2021: LHRC ilirekodi jumla ya matukio 35 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika hao, 31 walikuwa wanawake na 4 wanaume, huku wanawake wakiwa takribani 89% ya waathirika
Pia, 72% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
2022: Kulikuwa na matukio 33 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika, 31 walikuwa wanawake na 2 wanaume, wanawake wakiwa takribani 94% ya waathirika. 52% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
2023: LHRC ilirekodi matukio 50 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi, ikiwa ni ongezeko la matukio 17 ukilinganisha na mwaka 2022
Kati ya waathirika hao, 45 walikuwa wanawake na 5 wanaume, wanawake wakiwa 90% ya waathirika. Takribani 46% ya matukio yalihusishwa na wivu.
Mjumuisho 2019–2023: Jumla ya matukio 162 ya mauaji yaliyorekodiwa katika takwimu hizi. Kati ya waathirika waliotajwa, wanawake ni 151
Mjadala👇
Sitaki kusema hakuna wanawake wanaofanya ukatili
Tumeona wapo na siwezi kufumbia macho hili hata kidogo
Wanawake wenzangu JF hakuna haja ya kukatisha maisha ya mtu kwa sababu tu ya mapenzi au migogoro mbalimbali
Ukiona mzigo ni mkubwa, tafuta msaada
Usimue mtu
Huna haja ya kuua, hilo sio jukumu lako
Kwa sababu hata usipomuua, kwa nature ya mwanadamu kila mtu lazima atakufa siku yake
Nina hakika wanaofanya mauaji huishia kwenye majuto ya milele
Tuje kwa wanaume ambao ni tishio...
Enyi wanaume, acheni kuua wanawake
Hawa ni mama zenu, dada zenu, wadogo zenu
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine kwa sababu tu amesalitiwa, amevunjwa moyo au amekataliwa
Ukihisi umefika sehemu huwezi kujidhibiti, tafuta msaada
Tafuta hata wataalamu wa saikolojia
Kama umechanganyikiwa na hujui ufanye nini, ongea uponeeee
Acha kubeba uchungu peke yako. Tafuta mtu wa kuongea naye
Kama unaogopa jambo lako kutangazwa, tafuta hata mtu asiyekujua, funguka na zungumza
Usiue Please
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine
Kama unaona hakuna future kwenye mahusiano, jikatae mapema na muachane kwa amani
Niseme hili👇
Wanaume, mkubali mkatae, mna udhaifu ambao mnatakiwa kuushinda
Kujifunza kustahimili maumivu rejection usaliti na kuvunjika moyo ni sehemu ya kukomaa
Chukulieni mfano hata hapa jukwaani
Watu wanaoongoza kuwakalia kooni wengine ni wanaume nyie hapo🫵
Nasikia wengine wanapita mpaka PM wakisambaza picha za wanawake ambao hawana hata uhakika nao
Kitu ambacho ni nadra kwa wanawake kufanya
Kuweni wakomavu
Jifunzeni kustahimili
Mbona wanawake wanahangaika na maisha?
Unakuta mama kaachiwa watoto, anakomaa na haui mtu
Amedhulumiwa anatulia
Anamfumania mume wake kitandani, tena na house girl kwenye kitanda chake mwenyewe lakini mama anapiga moyo konde
Mnazalisha nje huko, wanawake wanapiga moyo konde
Enyi wanaume, nyie mna roho za barafu?
Wanawake wana roho za chuma?
Sitetei yeyote
Sitetei mwanamke msaliti wala mwanaume msaliti
Lakini ukiona umeshindwa kabisa kuendelea na mahusiano, achaneni kwa amani
Tatizo ni nini mpaka hali imefika hivi?
Karibu tujadili kwa pamoja
Na kuelemishana 🙏🙏
ShesRise_1 ✋️
Hakika wanaume wadhaifu ni wale wenye kichaa ambacho hakijathibishwa na daftari ndio huua wajinga kabisaMwanaume anayeua au kupiga mke wake kwasababu ya mapenz ana udhaifu fulan mwanaume kamili anayejiamini anajua atapata mwanamke mwingine muda wowotw ukichunguza utakuta either kuna matatizo ya kiuchumi au mambo mengine
Nimeweka kama hypothesis tu mkuu! You bear responsibility kwa mwanamke unayempenda, akikuzingua huwezi kufurahia, mwingine dio kama hivyo anakumaliza, mwingine anasamehe, mwingine anaondoka anakuacha hapo. Approaches tofauti tu.Mstari kama huu 👆 mwaka 47 ilikuwa ngumu kuuona, hii ni kusema hata sisi wazee sometimes tunatumia lugha ya vijana ili tueleweke kirahisi.
Cc Mzee Grahams.
Kabisa kabisa!Nimeweka kama hypothesis tu mkuu! You bear responsibility kwa mwanamke unayempenda, akikuzingua huwezi kufurahia, mwingine dio kama hivyo anakumaliza, mwingine anasamehe, mwingine anaondoka anakuacha hapo. Approaches tofauti tu.
Anajiona hana pa kwenda, kuna watu wanajua kuteka.Yaani mkuu, mtu anaedundwa halafu anabaki huwa simuelewi na sitokaa nimuelewe. Hivi ile hofu tu ya kibinadamu hawana?. Yaani unakaa nyumba moja na mtu anakudunda hadi unazimia? Tena unalala nae kitanda kimoja. Watu wana mioyo jamani.
Ni rahisi kusema hivyo ila sio rahisi sana mwanamke kumkimbia mwanaume mpigaji au mtesaji kwa sababu nyingi sana😁. Fikiria jinsi single mothers wanasimangwa kuanzia kwenye familia zao halafu ukute tayari una vifaranga viwili, una pesa zozote za kwako, huwezi kufanya shughuli za kuingiza kipato, dini haikubali talaka n.k. Wengine wanapata na good sex hawaoni pengine pa kupata hiyo mikwaju😁Wanawake na sisi hatujijali, unakuta mtu anaona kabisa mwanaume ana dalili za kumfanyia kitu kibaya , halafu anabaki,mwisho wa siku anauwawa kweli. Hata Jennifer alihisi mume wake atamuua, ila hakuchukua hatua sahihi za kujilinda. Mi kwa niliyoyaona utotoni,mwanaume akiwa na dalili tu sizielewi, natoka mbio yaani mbio siangalii nyuma. Kule kwetu wanawake wanapigwa wanauwawa na waume zao kwa sababu za kijinga na familia zinapotezea. Utakuta mwanaume anamuua mke wake kisa mtoto wao wa miaka 6 kakojoa kitandani au kisa binti yao kabeba ujauzito au sijui mara mwanamke ameenda sokoni bila ruhusa ya mume.
Mi wanawake wanaovumilia wanaume wakorofi naonaga wanasubiri vifo vyao
Nonsense hii gentlemen unaua kisa usaliti ambao pengine hata hujauthibitishani muhimu na ni vizuri sana kua waaminifu, wastahilivu na wenye subra sana kwenye ndoa au mahusiano yoyote yale, vinginevyo mtajisogezea vita na mafarakano yanayoweza kupelekea mauti miongoni mwenu, kwa furaha ya muda mfupi tu.🐒
Sio mimi nasema aiseeeee bora niokote makopoNi rahisi kusema hivyo ila sio rahisi sana mwanamke kumkimbia mwanaume mpigaji au mtesaji kwa sababu nyingi sana😁. Fikiria jinsi single mothers wanasimangwa kuanzia kwenye familia zao halafu ukute tayari una vifaranga viwili, una pesa zozote za kwako, huwezi kufanya shughuli za kuingiza kipato, dini haikubali talaka n.k. Wengine wanapata na good sex hawaoni pengine pa kupata hiyo mikwaju😁
Dear nimekumbuka kuna video ya mchungaji maarufu Dar ilitrend nadhani 5 years ago , kwenye mahubiri huyo mchungaji alikuwa anawamahamisha wanaume wapige wake zao endapo wakiunguza mboga. Yule mchungaji akasema" wewe dada unampikia mume wako chakula halafu unaunguza kwanini usipigwe, lazima upigwe tu" tena anakazia. Sasa hapo unategemea nini?. Halafu huyo mchungaji ana jina la kipwani pwani ingawa kwa sura yake mi nilivyomuona nikajua tu mtu wa nyumbani huyu. Kakulia kwenye ukatili,anakuja Kanisani kuhamasisha wanaume wafanye ukatili na ajabu wanawake wanasali na kutoa sadaka kwake. Ingekuwa tunajielewa, wanawake wangeacha kwenda Kanisani kwake.Hakika unakuta mwanamke namlamba kamasi mwanaume maana hana option
Wengine wanaua kwa sababu ya 10kWanawake jiwekeni vizuri kiuchumi na mpunguze tamaa.
Hivyo vifo, huo wivu wa mapenzi unaotajwa kwa kiasi kikubwa ni ile jamaa amehudumia kwa muda mrefu mwisho anaambulia dharau au maumivu, kitu ambacho kinaepukika ikiwa mwanamke hutakua tegemezi kwa mwanaume.
Na ukiwa tegemezi sana ndio hiyo mtu anakuona kama mtumwa wake na sio mke/mpenzi.
Na mwisho mjifunze kupigana sio kila siku mnadundwa nyie tu, kwani hamli mkashiba?
Siku hizi simu janja (Smartphones) zimefanya hata sisi Wazee wa mwaka 47 kuji-tune kuendana na Kasi ya vijana 🤗Mstari kama huu 👆 mwaka 47 ilikuwa ngumu kuuona, hii ni kusema hata sisi wazee sometimes tunatumia lugha ya vijana ili tueleweke kirahisi.
Cc Mzee Grahams.
Hayajakukuta, waulize vizuri mawakili wa kesi za ndoa. Watu wanapelekana mahakamani kwa ugomvi mkubwa halafu siku ya kesi wanakuja wote mahakamani kwenye gari moja tena wamevaa mashati ya kufanana😁Sio mimi nasema aiseeeee bora niokote makopo
Mimi kabira langu mwanamke hawezi kuhudhuria KWENYE kikao Cha ukoo lakini watoto wadogo wa kiume wanaingiaKipenzi, wanaume wa hii nchi sahau kama watabadilika. Malezi wanayopewa huko majumbani, yanawafanya wao wajione miungu watu. Imagine mtu anakua kwenye utamaduni ambao mtoto mdogo wa kiume anapigiwa magoti na mwanamke mkubwa akiwa anapewa chakula. Unategemea huyu mtoto akikua mkubwa atachukulia mwanamke kama binadamu au atamuona kama ng'ombe tu??. Sisi wanawake ndo tuhamasishane kukataa ukatili. Na ukatili hua hauanzi mkubwa,unaanza kidogo kidogo. Tuwaambie mabinti zetu" ukipigwa kofi kimbia, ukitishiwa kwa maneno kimbia".uhai ndo muhimu zaidi vingine vyote vinatafutwa. Ila wanawake unakuta ndo tunaambiana" kofi tu unaondoka,bibi zetu walivumilia vipigo, wanaume wote ndo wapo hivyo". Mwisho wa siku mtu anauwawa. Unyanyasaji utakomeshwa na sisi wanawake sio kusubiri wanyanyasaji watuonee huruma.
Muwe wapole au muachane nayo.Kwamba tukae bila mahusiano? Au sijakuelewa
Ona tatizo lingine wanawake kuogopa kusema wakiogopa makombola ya wanaume wanaogopa kuitwa feministDear nimekumbuka kuna video ya mchungaji maarufu Dar ilitrend nadhani 5 years ago , kwenye mahubiri huyo mchungaji alikuwa anawamahamisha wanaume wapige wake zao endapo wakiunguza mboga. Yule mchungaji akasema" wewe dada unampikia mume wako chakula halafu unaunguza kwanini usipigwe, lazima upigwe tu" tena anakazia. Sasa hapo unategemea nini?. Halafu huyo mchungaji ana jina la kipwani pwani ingawa kwa sura yake mi nilivyomuona nikajua tu mtu wa nyumbani huyu. Kakulia kwenye ukatili,anakuja Kanisani kuhamasisha wanaume wafanye ukatili na ajabu wanawake wanasali na kutoa sadaka kwake. Ingekuwa tunajielewa, wanawake wangeacha kwenda Kanisani kwake.