Migogoro ya kimahusiano: Janga kwa Wanawake Tanzania

Migogoro ya kimahusiano: Janga kwa Wanawake Tanzania

Kwenye takwimu hapo umeona wapi vifo vingi vikisababishwa na tamaa ?

Kama sio wivu wa kijinga unalia unasalitiwa huku mwenyewe unakuta unanuka umalayer

Acheni u selfish dadeki zenu

Sawa tunanuka umalayer lakini hatuli vyenu. Nikuhudimie mimi bado ukampe mwingine utelezi? Can you imagine that? Mtakufa wengi.
 
Kwenye takwimu hapo umeona wapi vifo vingi vikisababishwa na tamaa ?

Kama sio wivu wa kijinga unalia unasalitiwa huku mwenyewe unakuta unanuka umalayer

Acheni u selfish dadeki zenu
Nyinyi si mnasema mmeumbwa na uvumilivu na hivyo mnaweza kustahimili? Mafahali wawili hawawezi kuishi zizi moja ,ukiona mme ni KITO-MBEE kwanini ukae naye? Dawa ya mwanamme Kito-mbee siyo na wewe kwenda kukitembeza ,dawa ni kumuacha ukisema na wewe ufanye hakika Pyupyuuu au nchakali ikuhusu kwasababu ME hawezi kuvumilia hayo mambo.
 
*Kutekeleza majukumu yake ya msingi ya Kila siku
*Haruhusiwi kufanya chochote lakin ngoja nikueke sawa
SISI ni waafrika na syo wazungu kikubwa zaidi tuna tamaduni zetu kama watanzania
*mwanamke ndye anaemuandalia mwanamke chakula na mambo mengne mengi
Kuna kitu kinaitwa hasira ( hapa Kuna utofauti wa Mimi,yeye au yule ) MAAMUZI hutegemea kiwango Cha mtu yalimfika
All in all

Wanaume tusiue ,,kataa kuua .ishinde nafsi
Suala la ajali za barabarani na ukatili wa kijinsia unapaswa kujadiliwa kwa hati ya dharura bungeni. Wanaume pia wana malalamiko yao wayaseme.
 
Na nyie wanawake mjichunge sana kama hamuwezi kupimana afya ya akili basi angalau uwe na clue, ukiona mtu mmepishana kidogo amebadilika uso na macho au amekuzaba kibao kimbiaaaaa huyo mshenzi kuna siku atakuua, usivumilie kipigo wala udhalilishaji, mwisho wa siku utazikwa mapema
Siku kikitoka kipimo cha afya ya akili cha fasta fasta kama kile cha HIV wanaume wengi tutakuwa single.
 
Mabinti wengi wa mjini wa Tanzania wanapenda sana kitonga na kuishi maisha yaliyo juu ya uwezo wao kwa mbali sana. Binti hana kipato chochote, ni mwanafunzi au ni secretary tu anayelipwa laki saba kwa mwezi lakini anataka aishi nyumba ya laki mbili kwa mwezi, amiliki iPhone 19 pro, mawigi ya laki laki, cosmetics zote ghali na awe anakula kuku kienyeji nusu kila siku.
And somehow wapata hivyo vyote, Unadhani kuna mtu atamshauri huyu mtu asikie?

Kuuana kunakuja baada ya kutapeliana au kukiuka makubaliano?

Nafikiri kwa jinsi ilivyo kila mwanamke anafurahia kupokea, suala linakuja nani anapokea nini, kwa nani na kwa makubaliano gani.

Wanaume pia hawajawahi kuacha kutoa, Hapa nazungumzia mambo ya mahusiano sio ndoa maana ndoa story iko tofauti. (Mke na mume wote wanapaswa kujenga familia yao, ni obligation sio ombi wala favor)
 
Nyinyi si mnasema mmeumbwa na uvumilivu na hivyo mnaweza kustahimili? Mafahali wawili hawawezi kuishi zizi moja ,ukiona mme ni KITO-MBEE kwanini ukae naye? Dawa ya mwanamme Kito-mbee siyo na wewe kwenda kukitembeza ,dawa ni kumuacha ukisema na wewe ufanye hakika Pyupyuuu au nchakali ikuhusu kwasababu ME hawezi kuvumilia hayo mambo.
Nani alisema mwanamke ameumbwa kuvumilia ushenzi wa mwanaume

Mbona mwanamke mwingine akishindwa akaamua kuondoka mnaanza tena lawama

Aibu yenu nyie wanaume wabinafsi
 
Angalizo msomaji wangu bandiko ni refu kidogo
Naomba uwe mvumikivu katika usomaji wako
Karibu sana kwenye mada 😊

Hello Great Thinkers 🫡

Katika pita pita zangu huko IG nimekuta kuna dada mmoja amepost kuhusu vifo vinavyotokana na migogoro ya kimahusiano hapa Tanzania 🇹🇿

Nimekuwa shocked baada ya kuona takwimu zinaogopesha na kushangaza
Ikanisukuma niende kwenye mtandao ku search na nione hali ilivyo kwa kujihakikishia mimi tomaso nimeshtushwa
Sikujua hali ni mbaya kwa ukubwa huu!

Nimepigwa butwaa
Hali inatisha

Chanzo cha takwimu (LHRC Tanzania)

Niweke sawa hapa
Hizi takwimu ni kati ya mwaka 2019_2023

Hebu tuangalie hizi takwimu za mauaji yanayohusisha wenza wa kimapenzi Tanzania

2019: LHRC ilirekodi wanawake 12 waliouawa na waume/wenza wao ambapo 8 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu

2020: LHRC ilirekodi wanawake 32 waliouawa na waume/wenza wao, ambapo 23 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
Hii ilikuwa zaidi ya mara mbili ya matukio yaliyorekodiwa mwaka 2019

2021: LHRC ilirekodi jumla ya matukio 35 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika hao, 31 walikuwa wanawake na 4 wanaume, huku wanawake wakiwa takribani 89% ya waathirika
Pia, 72% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu

2022: Kulikuwa na matukio 33 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika, 31 walikuwa wanawake na 2 wanaume, wanawake wakiwa takribani 94% ya waathirika. 52% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu

2023: LHRC ilirekodi matukio 50 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi, ikiwa ni ongezeko la matukio 17 ukilinganisha na mwaka 2022
Kati ya waathirika hao, 45 walikuwa wanawake na 5 wanaume, wanawake wakiwa 90% ya waathirika. Takribani 46% ya matukio yalihusishwa na wivu.

Mjumuisho 2019–2023: Jumla ya matukio 162 ya mauaji yaliyorekodiwa katika takwimu hizi. Kati ya waathirika waliotajwa, wanawake ni 151

Mjadala👇

Sitaki kusema hakuna wanawake wanaofanya ukatili
Tumeona wapo na siwezi kufumbia macho hili hata kidogo

Wanawake wenzangu JF hakuna haja ya kukatisha maisha ya mtu kwa sababu tu ya mapenzi au migogoro mbalimbali
Ukiona mzigo ni mkubwa, tafuta msaada
Usimue mtu
Huna haja ya kuua, hilo sio jukumu lako

Kwa sababu hata usipomuua, kwa nature ya mwanadamu kila mtu lazima atakufa siku yake

Nina hakika wanaofanya mauaji huishia kwenye majuto ya milele

Tuje kwa wanaume ambao ni tishio...

Enyi wanaume, acheni kuua wanawake
Hawa ni mama zenu, dada zenu, wadogo zenu
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine kwa sababu tu amesalitiwa, amevunjwa moyo au amekataliwa

Ukihisi umefika sehemu huwezi kujidhibiti, tafuta msaada
Tafuta hata wataalamu wa saikolojia
Kama umechanganyikiwa na hujui ufanye nini, ongea uponeeee

Acha kubeba uchungu peke yako. Tafuta mtu wa kuongea naye
Kama unaogopa jambo lako kutangazwa, tafuta hata mtu asiyekujua, funguka na zungumza

Usiue Please
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine

Kama unaona hakuna future kwenye mahusiano, jikatae mapema na muachane kwa amani

Niseme hili👇
Wanaume, mkubali mkatae, mna udhaifu ambao mnatakiwa kuushinda
Kujifunza kustahimili maumivu rejection usaliti na kuvunjika moyo ni sehemu ya kukomaa

Chukulieni mfano hata hapa jukwaani
Watu wanaoongoza kuwakalia kooni wengine ni wanaume nyie hapo🫵
Nasikia wengine wanapita mpaka PM wakisambaza picha za wanawake ambao hawana hata uhakika nao
Kitu ambacho ni nadra kwa wanawake kufanya

Kuweni wakomavu
Jifunzeni kustahimili

Mbona wanawake wanahangaika na maisha?
Unakuta mama kaachiwa watoto, anakomaa na haui mtu
Amedhulumiwa anatulia

Anamfumania mume wake kitandani, tena na house girl kwenye kitanda chake mwenyewe lakini mama anapiga moyo konde

Mnazalisha nje huko, wanawake wanapiga moyo konde

Enyi wanaume, nyie mna roho za barafu?
Wanawake wana roho za chuma?

Sitetei yeyote
Sitetei mwanamke msaliti wala mwanaume msaliti

Lakini ukiona umeshindwa kabisa kuendelea na mahusiano, achaneni kwa amani

Tatizo ni nini mpaka hali imefika hivi?

Karibu tujadili kwa pamoja
Na kuelemishana 🙏🙏

ShesRise_1 ✋️
Roho ndogo
 
Usariti+Tamaa ni janga
Demu
Ana muuza chips
Boda boda
Boss kaziini
Bwana nyumbani
Usife kweli
Mi nadhani kuepo na mdahalo wanawake mkanyane na mshauliane

Wanaume tusiue
 
Serikali iweke ofisi za watu wa ushauri nasaha na saikolojia, kuanzia mashuleni hadi maofisini, mitaala liingizwe somo la afya ya akili, kampeni juu ya afya ya akili ziwe nyingi sio mnatangaza betting tu, kwenye kila kipindi cha radio au tv kuwe na tangazo kuhusu afya ya akili mbona enzi zile za VVU na Ukimwi mliweza? Tilieni mkazo hili suala wanawake wanateketea juu ya huyu kiumbe mwanaume
Huna haja ya kufanya hayo yote,wanawake wanatakiwa haelimishwe kutochanyanga wanaume.Kama umemchoka mumeo achana naye sio umsaliti ilihali bado unaendelea kuishi naye-hapo kifo kitakuita.
 
Aibu yenu wanaume lol
Kwanini usidai fidia kama vipi
Kuua unaona ndio njia sahihi
Badilisheni mitazamo hiyo ya hovyo ya kuana
Kipenzi, wanaume wa hii nchi sahau kama watabadilika. Malezi wanayopewa huko majumbani, yanawafanya wao wajione miungu watu. Imagine mtu anakua kwenye utamaduni ambao mtoto mdogo wa kiume anapigiwa magoti na mwanamke mkubwa akiwa anapewa chakula. Unategemea huyu mtoto akikua mkubwa atachukulia mwanamke kama binadamu au atamuona kama ng'ombe tu??. Sisi wanawake ndo tuhamasishane kukataa ukatili. Na ukatili hua hauanzi mkubwa,unaanza kidogo kidogo. Tuwaambie mabinti zetu" ukipigwa kofi kimbia, ukitishiwa kwa maneno kimbia".uhai ndo muhimu zaidi vingine vyote vinatafutwa. Ila wanawake unakuta ndo tunaambiana" kofi tu unaondoka,bibi zetu walivumilia vipigo, wanaume wote ndo wapo hivyo". Mwisho wa siku mtu anauwawa. Unyanyasaji utakomeshwa na sisi wanawake sio kusubiri wanyanyasaji watuonee huruma.
 
Na nyie wanawake mjichunge sana kama hamuwezi kupimana afya ya akili basi angalau uwe na clue, ukiona mtu mmepishana kidogo amebadilika uso na macho au amekuzaba kibao kimbiaaaaa huyo mshenzi kuna siku atakuua, usivumilie kipigo wala udhalilishaji, mwisho wa siku utazikwa mapema
Huwa wanaamini labda atabadilika, na wanapenda kubembelezwa na kudanganywa danganywa.

Jitu linamdunda ila bado kaliganda, kumbe mchana akibondwa usiku anabembelezwa na kuletewa zawadi anapoa na kusahau.

Shida kwa sisi wanaume sasa, ukinisaliti sijui uongee kingereza gani upunguze maumivu ya kuchapiwa, hatubembelezeki na mbaya zaidi sisi sio wafariji wazuri wa sisi kwa sisi, hatujui kufarijiana kwenye mahusiano.
 
Wanawake nao wanauwa wakisalitiwa ila mauwaji yao ni very strategical, inaweza kuchukua hata miaka 10, ukaja kutiliwa sumu kwenye msosi, hapo mwanaume ushasahau na ndani mnacheka vizuri tu.

wanawake wana visasi. Sisi ni papo hapo hakuna kusubiri.

Na ukinisaliti nikakuacha utaniona boya, so it's better nikumalize usije endeleza usaliti wako kwa mwanaume mwingine.

Hata tamaa ya mali ni usaliti pia.

"Msaliti auwawe"

Kwa lugha nyepesi ni kwamba wanaume wengi hawana uwezo wa kudhiti hisia zao yani ni wadhaifu.
 
Back
Top Bottom