Tatizo huwa mnasoma halafu hamtaki kuelewa kilichoandikwa.
Ukisoma vizuri kwenya andiko langu nimeandika suala la Rotation kwa wachezaji.
Na Wala sijaandika kuwa hao wachezaji waingie kipindi Cha michuano ya Kimataifa.
Unaweza UKANIAMBIA sureboy Mara ya mwisho kucheza ni lini??
KIbwana Shomari Mara ya mwisho kucheza ni lini?
Oky Jesus Moloko Kuna za chini chini kuwa dirisha dogo ataachwa lakini ndiyo Supersub ya Gamond tazama mechi ya coastal union.
Moloko alifanya nini??
Soma vizuri andiko langu Kisha uje kujenga hoja.
Ndio maana nikakwambia mnaandika ujinga na upumbavu.
"Unataka wachezaji waingie tu kwenye rotation eti sijaandika kuwa waingie kwenye klabu bingwa", sasa kama hukuandika kuwa waingie kwenye klabu bingwa kwanini huu uzi uutoe baada ya mechi ya klabu bingwa kuisha? Kwanini hukusubiri mechi ya tarehe 16 kati ya Yanga na Mtibwa iishe ndio uandike? Kwenye hiyo mechi ndio ungejua Gamondi atafanya nini kwenye rotation. Usijitetee kwenye hilo, wewe na wenzio msiojua mpira mlitaka Gamond afanye rotation kwenye mechi ya klabu bingwa ndio maana baada ya mechi ya Medeama nyuzi zimekuwa nyingi na wajinga wenzio wakakuunga mkono.
Tukija kwenye ligi kuu,
Yanga kacheza michezo 9 na katika michezo hiyo, Yanga imecheza michezo minne mfululizo kwa timu ngumu ( vs Azam, vs Singida, vs Simba, vs Coastal union)hapa kocha anazihitaji alama 12 na dhidi ya timu ngumu na mechi zinazofuatana, ni ngumu sana kupanga kikosi nje ya first eleven yake labda itokee kuna majeruhi.
Sureboy mara ya mwisho kucheza ni dhidi ya Ihefu tarehe 4 mwezi wa 10 mechi ambayo Yanga walipoteza.
Baada ya hiyo mechi, Yanga ilicheza mechi moja tu ambayo ni nyepesi nayo ilikuwa sio nyepesi kihivyo kwasababu walikuwa away dhidi ya Geita.
Baada ya Geita ikafuata Azam, Singida, Simba, na Coastal. Je ulitaka hapo Gamond acheze kamari kwa kuharibu first eleven yake dhidi ya timu ipi hapo?
Kuhusu Moloko, ndio super sub wa Gamond sikatai je vipi kuhusu quality yake inaridhisha? Vipi kama wameamua kumchukua winger zaidi ya Moloko je ni jambo baya?