Miguna Miguna amvaa Rais Magufuli kuhusu kukamatwa kwa Tito Magoti

Miguna Miguna amvaa Rais Magufuli kuhusu kukamatwa kwa Tito Magoti

Kutetea haki za wanaoonewa nayo ni kazi yake. Kama na wewe unavyofanya kazi yako ya kutukuza wanaojivika umungu mtu wa kuamua nani aishi au nani afe au nani aozee gerezani kwa kesi uchwara. Kila mtu afanye kazi yake.
Toka lini Miguna ametetea haki za wanaonewa,kama humjui Miguna basi baki hivyo hivyo,wanaonewa nani?
 
Toka lini Miguna ametetea haki za wanaonewa,kama humjui Miguna basi baki hivyo hivyo,wanaonewa nani?
Wanaonewa na wanaowapa kesi uchwara kama kesi ya yule tajiri.wa.Yanga. Unauliza toka.lini!? Acha.kuchekesha. Haya tufanye toka leo. Una tatizo na hilo?
 
Mutanyooka tu! Dili zote kwa heri! Walikwambia wapi? Au unaamini itasaidia wamuunge mkono Mbowe? Tuache mambo ya kuimarisha na kulaani makabila ya wengine. Kwani kabila bora hapa TZ ni lipi? Kwa vigezo gani?
Unaleta arguments za kitoto sasa. Hakuna aliyelaani kabila lolote lile. After all, uko nje ya mada.
 
Biblia pia kupitia kitabu cha kwanza cha Samuel inatuambia kuwa anayeona rohoni kwa binadamu ni mmoja tu, naye ni Mungu. Sio wewe na mimi.
Biblia pia inasema Roho wa Mungu akiwa ndani yetu tutaona hata yale yasiyoonekana kwa macho ya kibinadamu.
 
SIJUI ANAUNGAMA KWA PADRE GANI!?..... Ilikuwa makosa makubwa sana kumweka msukuma Ikulu. Unajua hata kuoga hawaogi!!!... Huge mistake....
Ha ha ha ha sio wasukuma wote ni huyu tu katia doa
 
Miguna kaongea alichoona ni sahihi kwake kuongea. Kama kushangilia umezoea wewe kushangilia.unaowashingilia. Hiyo ni juu yako. Yeye kamwambia huyo anayeteka watu kwa mujibu wake yeye Miguna. Kama wewe msemaji wa serikali mjibu basi. Kila mtu afanye kazi yake.
Haki za binadamu hazizuiwi na mipaka. Ndio maana Nyerere aliongoza juhudi za kusaidia.mataifa yaliyokuwa bado kupata Uhuru. Otherwise angeweza kusema tu kila mtu abebe msalaba wake.
Haiwezekani mtu anayetaka kuvunja umoja wa kitaifa akachekewa. Kutekana tekana kijinga na kupotezana sio asili ya WATz. Hizo ni tabia za kule nchi jirani.
Imebidi nipitie baadhi ya michango yako kuona kama kuna wakati unakuwa na fahamu za kujenga hoja. Ninachokiona, uko hoi! Usijiingize kujadili ya maana. Huna uwezo.
 
SIJUI ANAUNGAMA KWA PADRE GANI!?..... Ilikuwa makosa makubwa sana kumweka msukuma Ikulu. Unajua hata kuoga hawaogi!!!... Huge mistake....
😂😂😂nothing personal against wasukuma but you made my day!
 
Waliokuwa wanaitwa Wasiojulikana, mimi nimewafahamu wawili. Wewe je!?
 
Baada ya kukopi ya Miguna, wewe unasemaje?
Sidhani kama tumefikia hatua ya kupewa ushauri na mtu ambaye ni reject wa nchi jirani.
Sasa Miguna Miguna yake yamshinda ataweza ya bongo dasalaam . Dawa ishamwingia atulie dozi ifanye kazi
 
Imebidi nipitie baadhi ya michango yako kuona kama kuna wakati unakuwa na fahamu za kujenga hoja. Ninachokiona, uko hoi! Usijiingize kujadili ya maana. Huna uwezo.
Mwenye uwezo wa kujenga hoja nani!? Ni wewe unayeunga mkono udhalimu!? Lakini haishangazi kwa kuwa hata dhalimu Idi Amini alikuwa na wafuasi waliomuabudu na kuunga mkono uzalendo uchwara.
 
nimesoma post zote, mimi naishia hapa. naogopa cyber crime. tupo pamoja[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]

Hasara Umfika Mwenye Mabezo
 
DK. MIGUNA MIGUNA WA KENYA AMVAA JPM KUKAMATWA KWA TITO MAGOTI.

Mwanasiasa na Mwanasheria machachari nchini Kenya, Dk. Miguna Miguna amemtaka Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kumwachilia huru Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Tito Magoti.

Dk. Miguna ambaye amewahi kuidhinisha kiapo cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa ni 'Rais wa Wananchi' Januari 2018, jambo lilisababisha kutimuliwa kwake nchini Kenya na kupelekwa nchini Canada ambako alidaiwa kuwa ni raia wa nchi hiyo amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Rais Magufuli anapaswa kutambua kuwa suala la kuwakatisha tamaa, kuwaogopesha na kujaribu kuwanyamazisha wakosoaji, wapinzani na wanaharakati za haki za binadamu nchini humo dhidi ya serikali yake halitafanikiwa.

Dk. Miguna ameita vitendo hivyo vya serikali dhidi ya wakosoaji, wapinzani na wanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania ni dalili ya udhaifu mkubwa wa serikali hiyo.

Tito Magoti, ambaye ni mwanasheria anayehudumu LHRC alikamatwa siku nne zilizopita na watu wasiojulikana eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam, jambo ambalo lilizua taharuki kuwa ametekwa lakini baadae jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam lilijitokeza hadharani na kukiri kumshikilia mwanaharakati Magoti, ingawa halikutaja moja kwa moja makosa yake wala kituo ambacho kinamshikilia.

Makundi mbalimbali ya wanaharakati wa haki za binadamu Tanzania na kimataifa yamelaani kitendo cha Tito Magoti kukamatwa kinyume na taratibu kitendo kinachotafsiriwa kama utekaji kutokana utata unaoligubika tukio hilo.

Wanaharakati hao pamoja na taasisi mbalimbali nchini Tanzania na zile za kimataifa zimekuwa zikishinikiza kuachiliwa huru ama kufikishwa mahakamani endapo Ofisa huyo wa LHRC kuna makosa anatuhumiwa nayo.

Jana Desemba 22, 2019 Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa leo (Desemba 23, 2019) atatoa taarifa ya kina kuhusu kushikiliwa kwa Tito Magoti.

#JusticeForTitoMagoti
Miguna kamalizana na akina Uhuru na Raila au anapambana na yasiyomhusu?
 
Back
Top Bottom