Miguna Miguna amvaa Rais Magufuli kuhusu kukamatwa kwa Tito Magoti

DK. MIGUNA MIGUNA WA KENYA AMVAA JPM KUKAMATWA KWA TITO MAGOTI.

Mwanasiasa na Mwanasheria machachari nchini Kenya, Dk. Miguna Miguna amemtaka Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kumwachilia huru Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Tito Magoti.

Dk. Miguna ambaye amewahi kuidhinisha kiapo cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa ni 'Rais wa Wananchi' Januari 2018, jambo lilisababisha kutimuliwa kwake nchini Kenya na kupelekwa nchini Canada ambako alidaiwa kuwa ni raia wa nchi hiyo amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Rais Magufuli anapaswa kutambua kuwa suala la kuwakatisha tamaa, kuwaogopesha na kujaribu kuwanyamazisha wakosoaji, wapinzani na wanaharakati za haki za binadamu nchini humo dhidi ya serikali yake halitafanikiwa.

Dk. Miguna ameita vitendo hivyo vya serikali dhidi ya wakosoaji, wapinzani na wanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania ni dalili ya udhaifu mkubwa wa serikali hiyo.

Tito Magoti, ambaye ni mwanasheria anayehudumu LHRC alikamatwa siku nne zilizopita na watu wasiojulikana eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam, jambo ambalo lilizua taharuki kuwa ametekwa lakini baadae jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam lilijitokeza hadharani na kukiri kumshikilia mwanaharakati Magoti, ingawa halikutaja moja kwa moja makosa yake wala kituo ambacho kinamshikilia.

Makundi mbalimbali ya wanaharakati wa haki za binadamu Tanzania na kimataifa yamelaani kitendo cha Tito Magoti kukamatwa kinyume na taratibu kitendo kinachotafsiriwa kama utekaji kutokana utata unaoligubika tukio hilo.

Wanaharakati hao pamoja na taasisi mbalimbali nchini Tanzania na zile za kimataifa zimekuwa zikishinikiza kuachiliwa huru ama kufikishwa mahakamani endapo Ofisa huyo wa LHRC kuna makosa anatuhumiwa nayo.

Jana Desemba 22, 2019 Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa leo (Desemba 23, 2019) atatoa taarifa ya kina kuhusu kushikiliwa kwa Tito Magoti.

#JusticeForTitoMagoti
Ya kwao yanamshinda atayaweza yetu?
 
Ngoja nione kaama Miguna naye atatekwa au kupigwa risasi hadharani na mabibi zake jamaa.
 
Miguna kamshindwa UK anarukia yasiomuhusu
Haki za binadamu hazizuiwi na mipaka. Ndio maana Nyerere aliongoza juhudi za kusaidia.mataifa yaliyokuwa bado kupata Uhuru. Otherwise angeweza kusema tu kila mtu abebe msalaba wake.
 
Miguna Miguna ni fala tu mchumia tumbo hapo anataka mabwana zake huko Canada wampe prom,ahangaike na yake kwanza
Kutetea haki za wanaoonewa nayo ni kazi yake. Kama na wewe unavyofanya kazi yako ya kutukuza wanaojivika umungu mtu wa kuamua nani aishi au nani afe au nani aozee gerezani kwa kesi uchwara. Kila mtu afanye kazi yake.
 
Mi nilisikia kamanda mambo sasa ndo kamkamata sasa Miguna Miguna kaingia chaka mumtaka Magu. Ashughulikie uraia wake kwanza. Tunaoendesha nchi tunajua ndugu zetu wanavyotumika vibaya hadi kuhatarisha usalama wetu na.hasa hao wanaojiita kutetea haki wakati wanatetea matumbo ya familia zao.
Aisee! Wewe unaendeshA nchi au litumbo lako!?
 
Mimi naona kama Dr.Magufuli anaonewa vitu vingine. Nchi inaendeshwa na Mfumo jamani.Inawezekana hata Magufuli hajui hilo sakata.Haiwezekani Magufuli akawa "on top of everything" itafikia wakati hata mtu akijikwaa na kudondoka tutasema Magufuli ndiye kampiga mtama,nk,nk.Non sense.
Yeye anajua kila kitu. Alishasema hilo. Kumbuka alivyomwambia.yule askari magereza.wa.kule Butimba.
 
DK. MIGUNA MIGUNA WA KENYA AMVAA JPM KUKAMATWA KWA TITO MAGOTI.

Mwanasiasa na Mwanasheria machachari nchini Kenya, Dk. Miguna Miguna amemtaka Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kumwachilia huru Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Tito Magoti.

Dk. Miguna ambaye amewahi kuidhinisha kiapo cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa ni 'Rais wa Wananchi' Januari 2018, jambo lilisababisha kutimuliwa kwake nchini Kenya na kupelekwa nchini Canada ambako alidaiwa kuwa ni raia wa nchi hiyo amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Rais Magufuli anapaswa kutambua kuwa suala la kuwakatisha tamaa, kuwaogopesha na kujaribu kuwanyamazisha wakosoaji, wapinzani na wanaharakati za haki za binadamu nchini humo dhidi ya serikali yake halitafanikiwa.

Dk. Miguna ameita vitendo hivyo vya serikali dhidi ya wakosoaji, wapinzani na wanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania ni dalili ya udhaifu mkubwa wa serikali hiyo.

Tito Magoti, ambaye ni mwanasheria anayehudumu LHRC alikamatwa siku nne zilizopita na watu wasiojulikana eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam, jambo ambalo lilizua taharuki kuwa ametekwa lakini baadae jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam lilijitokeza hadharani na kukiri kumshikilia mwanaharakati Magoti, ingawa halikutaja moja kwa moja makosa yake wala kituo ambacho kinamshikilia.

Makundi mbalimbali ya wanaharakati wa haki za binadamu Tanzania na kimataifa yamelaani kitendo cha Tito Magoti kukamatwa kinyume na taratibu kitendo kinachotafsiriwa kama utekaji kutokana utata unaoligubika tukio hilo.

Wanaharakati hao pamoja na taasisi mbalimbali nchini Tanzania na zile za kimataifa zimekuwa zikishinikiza kuachiliwa huru ama kufikishwa mahakamani endapo Ofisa huyo wa LHRC kuna makosa anatuhumiwa nayo.

Jana Desemba 22, 2019 Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa leo (Desemba 23, 2019) atatoa taarifa ya kina kuhusu kushikiliwa kwa Tito Magoti.

#JusticeForTitoMagoti
Baada ya kukopi ya Miguna, wewe unasemaje?
Sidhani kama tumefikia hatua ya kupewa ushauri na mtu ambaye ni reject wa nchi jirani.
 
Wewe umepewa ushauri na nani!? Au wewe ndio Magufuli!? Yeye Miguna amemwambia yule anayeona ndiye kamteka huyo afisa wa LHRC. Unless wewe uwe ndiye uliyemteka. Kama wewe siye ujumbe utakuwa umemfikia au hata wewe mpambe wake unaweza kumwambia .
 
Huwezi ukahatarisha Maisha ya watu zaidi 55 million 50 for your own interest and your masters ukafikiri there is no Government

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Haiwezekani mtu anayetaka kuvunja umoja wa kitaifa akachekewa. Kutekana tekana kijinga na kupotezana sio asili ya WATz. Hizo ni tabia za kule nchi jirani.
 
Mimi naona kama Dr.Magufuli anaonewa vitu vingine. Nchi inaendeshwa na Mfumo jamani.Inawezekana hata Magufuli hajui hilo sakata.Haiwezekani Magufuli akawa "on top of everything" itafikia wakati hata mtu akijikwaa na kudondoka tutasema Magufuli ndiye kampiga mtama,nk,nk.Non sense.
Daaaah inawezekana uko nje ya nchi eti eeeh au hoja ya kumtetea Jiwe imekosekana kabisa safari hii
 
Yeye anajua kila kitu. Alishasema hilo. Kumbuka alivyomwambia.yule askari magereza.wa.kule Butimba.
Nadhani hujamuelewa. Huyo anatafuta namna ya kumtetea Jiwe lakini hoja inakosekana. Yaani Jiwe anatukuzwa kila sehemu mara makinikia mara kaokota mabehewa bandarini mara anatamani kuwa IGP mara korosho sijui mara kuteua wakubwa wasiotosha kwenye mihimili mingine ili waone haya kwenda kinyume, Lakini ikifika kwenye huu uhalifu wa kishamba ghafla tu Jiwe hausiki!!! daaaah weweeeee huwezi kunijibu hivyo mimi. Hii senteso hutumiwa na wehu wengi
 
Mbona kila siku anaongea akiwa kanda ya ziwa!
Wasukuma wenyewe wanamkana, wanasema kwanza hilo jina tu sio la kwao kisha hata laafudh yake kavu wanasema sio ya msukuma halisi na mwisho hata character wanadai sio compatible na ya kwao.
 
Kweli tabia sio za kisukuma kabisa ni kama za kitutsi hivi
 
Wasukuma wenyewe wanamkana, wanasema kwanza hilo jina tu sio la kwao kisha hata laafudh yake kavu wanasema sio ya msukuma halisi na mwisho hata character wanadai sio compatible na ya kwao.
Binamu yake Slim na amemkabidhi Mirerani
 
Wewe umepewa ushauri na nani!? Au wewe ndio Magufuli!? Yeye Miguna amemwambia yule anayeona ndiye kamteka huyo afisa wa LHRC. Unless wewe uwe ndiye uliyemteka. Kama wewe siye ujumbe utakuwa umemfikia au hata wewe mpambe wake unaweza kumwambia .
Kwa hiyo unaona mtu sahihi wa kushangiliwa ni Miguna? Tatizo tumekuwa tunaamini kila mtu ana jambo la kutusaidia matatizo yetu. Vichwa vimekuwa ni hardware isiyo na kitu kiasi yeyote mwenye software anaweka!! Yaani hata Miguna munashangilia eti kasema! Unategemea serikali iitikie maneno ya Miguna?
 
Wasukuma wenyewe wanamkana, wanasema kwanza hilo jina tu sio la kwao kisha hata laafudh yake kavu wanasema sio ya msukuma halisi na mwisho hata character wanadai sio compatible na ya kwao.
Mutanyooka tu! Dili zote kwa heri! Walikwambia wapi? Au unaamini itasaidia wamuunge mkono Mbowe? Tuache mambo ya kuimarisha na kulaani makabila ya wengine. Kwani kabila bora hapa TZ ni lipi? Kwa vigezo gani?
 
DK. MIGUNA MIGUNA WA KENYA AMVAA JPM KUKAMATWA KWA TITO MAGOTI.

Mwanasiasa na Mwanasheria machachari nchini Kenya, Dk. Miguna Miguna amemtaka Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kumwachilia huru Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Tito Magoti.

Dk. Miguna ambaye amewahi kuidhinisha kiapo cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa ni 'Rais wa Wananchi' Januari 2018, jambo lilisababisha kutimuliwa kwake nchini Kenya na kupelekwa nchini Canada ambako alidaiwa kuwa ni raia wa nchi hiyo amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Rais Magufuli anapaswa kutambua kuwa suala la kuwakatisha tamaa, kuwaogopesha na kujaribu kuwanyamazisha wakosoaji, wapinzani na wanaharakati za haki za binadamu nchini humo dhidi ya serikali yake halitafanikiwa.

Dk. Miguna ameita vitendo hivyo vya serikali dhidi ya wakosoaji, wapinzani na wanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania ni dalili ya udhaifu mkubwa wa serikali hiyo.

Tito Magoti, ambaye ni mwanasheria anayehudumu LHRC alikamatwa siku nne zilizopita na watu wasiojulikana eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam, jambo ambalo lilizua taharuki kuwa ametekwa lakini baadae jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam lilijitokeza hadharani na kukiri kumshikilia mwanaharakati Magoti, ingawa halikutaja moja kwa moja makosa yake wala kituo ambacho kinamshikilia.

Makundi mbalimbali ya wanaharakati wa haki za binadamu Tanzania na kimataifa yamelaani kitendo cha Tito Magoti kukamatwa kinyume na taratibu kitendo kinachotafsiriwa kama utekaji kutokana utata unaoligubika tukio hilo.

Wanaharakati hao pamoja na taasisi mbalimbali nchini Tanzania na zile za kimataifa zimekuwa zikishinikiza kuachiliwa huru ama kufikishwa mahakamani endapo Ofisa huyo wa LHRC kuna makosa anatuhumiwa nayo.

Jana Desemba 22, 2019 Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa leo (Desemba 23, 2019) atatoa taarifa ya kina kuhusu kushikiliwa kwa Tito Magoti.

#JusticeForTitoMagoti
ngoja na yeye waje wamkamate na miguna yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo unaona mtu sahihi wa kushangiliwa ni Miguna? Tatizo tumekuwa tunaamini kila mtu ana jambo la kutusaidia matatizo yetu. Vichwa vimekuwa ni hardware isiyo na kitu kiasi yeyote mwenye software anaweka!! Yaani hata Miguna munashangilia eti kasema! Unategemea serikali iitikie maneno ya Miguna?
Miguna kaongea alichoona ni sahihi kwake kuongea. Kama kushangilia umezoea wewe kushangilia.unaowashingilia. Hiyo ni juu yako. Yeye kamwambia huyo anayeteka watu kwa mujibu wake yeye Miguna. Kama wewe msemaji wa serikali mjibu basi. Kila mtu afanye kazi yake.
 
Back
Top Bottom