MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Tal Chaimi, mkazi wa Kibbutz Nir Yitzhak, na Joshua Luito Mollel, mkazi wa Kibbutz Nahal Oz , waliuawa wakati wakishikiliwa mateka na Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Miili yao yote miwili bado inashikiliwa na Hamas. Chaimi aliaminika kutekwa nyara lakini, ushahidi mpya ulionyesha aliuawa Oktoba 7 na mwili wake ulichukuliwa na Hamas hadi Gaza.
Chaimi alikuwa sehemu ya kikosi cha dharura ambacho kilitumwa kusimamisha shambulio la Hamas hadi waweze kuongezewa nguvu.
Chaimi aliondoka asubuhi hiyo baada ya kubainika kuwa Hamas wamejipenyeza Israel na kuwaacha mkewe na watoto nyumbani.
Waliporejea kikosini, Chaimi hakuwa miongoni mwao. Kikosi hakikuweza kumwambia mkewe mahali alipokuwa.
Chaimi alikuwa mkazi wa kizazi cha tatu wa Nir Yitzhak na mzao wa waanzilishi wake. Ameacha mke na watoto watatu.
Kumbukumbu yao iwe baraka
Mollel mwanafunzi wa Kitanzania wa kilimo alikuwa amewasili Israel wiki mbili tu kabla ya Mauaji ya Oktoba 7.
Mollel alikuwa akifanya kazi huko Nahal Oz kama mfugaji wa ng'ombe wa maziwa na alikuwa kazini siku ya mauaji hayo.
Baba yake alijulishwa usiku wa kuamkia leo juu ya hatma ya mtoto wake, inasemekana haamini na ameuliza chanzo cha habari hiyo.
Babake Mollel anawasili Israel usiku huu akiandamana na wawakilishi wa wizara ya mambo ya nje, kwa mujibu wa Kituo cha Wahamiaji na Wakimbizi.
UPDATE:
Kupitia Mtandao wa X, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amethibitisha taarifa hii.
Makamba ameandika “Tumejulishwa na Serikali ya Israel kwamba Joshua Mollel, kijana wa Kitanzania aliyekuwa anasoma chini Israel, na ambaye tulipoteza naye mawasiliano tangu tarehe 7 Oktoba 2023, na ambaye Serikali imekuwa inafanya jitihada kubwa kupata taarifa zake tangu wakati huo, aliuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la Hamas mnamo tarehe 7 Oktoba 2023. Nimeongea na Mzee Mollel, baba mzazi wa Joshua, kuhusu ujumbe huo wa Serikali ya Israel.
Tunaendelea na mpango wa awali wa kuwapeleka Mzee Mollel na manafamilia mwingine pamoja na Afisa wa Serikali nchini Israel, kuungana na Balozi wetu na maafisa waliopo huko, kukutana na kuzungumza na mamlaka za nchi hiyo ili kupata taarifa za ziada. Kwa ridhaa ya familia, na itakapobidi, tutatoa taarifa za ziada katika siku zijazo.”