Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Songea tumefikiwaaa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii ni miji kumi inayoongoza kwa vumbi nyakati za kiangazi nchini Tanzania. Ukienda huko achana na habari ya nguo nyeupe. Pendelea rangi nyeusi, brown au kijivu.

1. KARATU
2. KASULU
3. KIBONDO
4. BOMANG'OMBE, Hai
5. SONGEA
6. TUNDUMA
7. ORKESMET, Simanjiro.
8. DODOMA
9. MERERANI
10. MTO WA MBU
Mbeya Jiji saizi vumbi limepungua kidogo
 
Aloo sio mchezo karatu baba lao. Nilienda msibani kurudi wife anauliza kwani walikugeuza maksai nn maana nguo zinachafuka vumbi la maana. Lile vumbi la karatu unaweza ombea hata mkopo bank.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kasulu ni hatari. Ile vumbi sio mchezo
Nimeishi huko...Asee kiangazi vumbi la maana, masika tope ka uji wa jela.

Sasa lami waloweka lote linabadilika linakua jekundu...Yaani hata wavue viatu wanapokanyaga lami bado ni kazi bure....

Vijiji vya Kasulu sasa, mamaaa!

Ila kiboko ya vumbi na tope la Kigoma ni Kibondo! Asee palinishinda!
 
Back
Top Bottom