Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Songea tumefikiwaaa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbeya Jiji saizi vumbi limepungua kidogo
 
Aloo sio mchezo karatu baba lao. Nilienda msibani kurudi wife anauliza kwani walikugeuza maksai nn maana nguo zinachafuka vumbi la maana. Lile vumbi la karatu unaweza ombea hata mkopo bank.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kasulu ni hatari. Ile vumbi sio mchezo
Nimeishi huko...Asee kiangazi vumbi la maana, masika tope ka uji wa jela.

Sasa lami waloweka lote linabadilika linakua jekundu...Yaani hata wavue viatu wanapokanyaga lami bado ni kazi bure....

Vijiji vya Kasulu sasa, mamaaa!

Ila kiboko ya vumbi na tope la Kigoma ni Kibondo! Asee palinishinda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…