Miji midogo midogo Tanzania ambayo ina vibe na fursa za kibiashara lakini haivumi

Miji midogo midogo Tanzania ambayo ina vibe na fursa za kibiashara lakini haivumi

Kwenu ni Songwe sehemu gani maana naona umechagua miji ya kwenu...Nyangao kinachoibeba ni iyo Hospitali tu.
Kuna vimiji Kama
Mtimbira- Moro
Igwachanya- Njombe
Gairo
Tinde Shinyanga
Vimiji vidogo dogo lkn Vibe lake la kutosha
Hahahaha, mkuu hebu nikurekebishe kidogo Mimi sio mwenyeji wala sio mzaliwa wa Mkoa wa Songwe, niliwahi kuishi Mkoa wa Songwe kikazi nikiwa katika branch la taasisi fulani. Hivyo ilinichagiza kuufuatilia Mkoa wa Songwe vizuri ili niweze kujua fursa zakee na maeneo yake pia.
Mkoa huu Hauna miji mingi mikubwa zaidi ya Tunduma angalau, Ila una miji midogomidogo mingi inayokuwa kwa kasi.
Binafsi naijua Tanzania kama robo yake hivi.. maana nimetembea/kuzunguka Mikoa 12(yaan sio kwa kupita bali ni Kwa kuzunguka Mikoa hiyo na Wilaya zake).
Hiyo Igwachanya ya Njombe naijua vizuri kumbukumbu zangu zinanikumbusha ndipo ilipo Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe, ukitokea Njombe Town kilomita kadhaa utaingia kushoto kwako barabara ya vumbi kuelekea Igwachanya.
 
Hii miji midogomidogo mingine hebu niitaje tu ili wadau wengine waweze kuifahamu na kama wanahitaji kutafuta/kufuata fursa huko basi wafuate.
• Kibaigwa
• Nanyamba
• Mahuta
• Chimala
• Ikwiriri
• Mangaka
• Nagaga
• Nangurukuru
• Ilula
• Kalenga
• Mlimba
 
Vipi kuhusu Chalinze
Chalinze ilishakuwa na sasa inazidi kujitanua, ni Mji uliobeba mamlaka ya Wilaya kwa sasa,, fursa za biashara zipo kama biashara za mananasi, machungwa n.k😃
Chalinze ndio lango la kuingilia Mikoa ya Kaskazini yaan Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na kwingineko.
Naona toka Mhe: RizOne kapewa hili Jimbo basi Chalinze inazidi kuneemeka, Sasa wamepata hadi kituo cha mabusi kizuri kabisa sio kama kile cha Wilaya ya Gairo kinachotia aibu😃

Ridhiwan Kikwete Hoyeeee
 
Hii miji midogomidogo mingine hebu niitaje tu ili wadau wengine waweze kuifahamu na kama wanahitaji kutafuta/kufuata fursa huko basi wafuate.
• Kibaigwa
• Nanyamba
• Mahuta
• Chimala
• Ikwiriri
• Mangaka
• Nagaga
• Nangurukuru
• Ilula
• Kalenga
• Mlimba
1. Ndanda
2. Matai
3. Lyanzumbi
4. Rungwa
5. Inyonga
6. Lupa Tinga Tinga
7. Dumila
8.Laela
9. Mangaka
10. Madaba
11. Makambako
12. Tinde
13. Ikwiriri
14. Tura

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Labda kama unamaanisha Mangaka, BUT Nanganga ni kijijini tu sema ni Kijiji kilichopo njia kuu ya kwenda Masasi na Lindi/Mtwara bila kusahau hapa ndipo pacha/barabara ya kuelekea Ruangwa kwa Wamwera au kwa Mh: Kassim Majaliwa(PM), barabara hii ya kutoka Nanganga to Ruangwa ipo katika matengenezo ya hali ya juu kuelekea kiwango cha lami(Trunk Road)
Ikwiriri na nanganga uko sahihi
 
Na hapo kuna machimbo ya dhahabu yanatema vizuri tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom