Mikakati hii ya kimafia ikifanyika Simba SC itakuwa Bingwa, wasiwasi wangu uko kwa Uongozi wenye kusalitiana

Pamoja na yote yanayozungumzwa lakini tatizo kubwa la Simba lipo kwenye uongozi. Kwa mtu mwenye akili sawasawa ataliona hili tatizo. Timu ina mapungufu baadhi ya sehemu uwanjani (hasa kiungo mkabaji na mshambuliaji wa kati) unategemea wachezaji wa kuondoa hayo mapungufu wawe wamefika muda mfupi kabla dirisha la usajili halijafunguliwa ili dirisha likifunguliwa tu wawe wamesajiliw na wameshazoea mazingira ya timu na waanze kuimarisha timu. Cha ajabu mpaka leo ni Saidoo tu ndio amesajiliwa. Matokeo yake timu inaacha pointi mbili Kagera kifala kabisa. Na nafasi aliyosajiliwa Saidoo haikuwa ni tatizo kubwa sana Simba ukilinganisha na nafasi ya mshambuliaji wa kati ambayo krosi kibao za Mohamed Hussein", Sakho, Okra na Kapombe hazitumiki ipasavyo achilia mbali "assist" za Chama na Muzamiru.

Halafu watu wazima na akili zao wanakaa wanaombea Yanga apoteze michezo yake. Hata Yanga akipoteza mchezo mmoja wakati Simba yenyewe haishindi mechi zake zote mfululizo itawasaidia nini kwenye kutafuta ubingwa. Kama kuna biashara kichaa Simba wanaifanya katika kutafuta ubingwa ni kumtegemea Boko awape ubingwa. Boko kwa umri alionao sasa anatakiwa awe ni "back up" ya mshambuliaji mwingine na acheze si zaidi ya dakika 20 kwenye mechi moja. Sasa wao Simba wanamtumia kwa dakika zote 90 matokeo yake leo gari linawaka mechi ijayo gari linazima halafu mnamlaumu bure akikosa magoli ya wazi.

Mwisho Simba tafuteni mshambuliaji mwenye matumizi mazuri ya kichwa na miguu kama yule Kagere aliyetoka Gor Mahia sio huyu wa sasa aliyepo Singida mtanishukuru sana.

Ni mtizamo tu.
 
Au yule Abeid Mziba 98% ya magoli yake yalikuwa ya vichwa.
Na hiyo kasi ya mpira alioupiga kichwa unashinda mpira uliopigwa shuti.
 
Back
Top Bottom