Mikakati ya Serikali ya Rais Samia kuhusu akiba ya Chakula Nchini

Mikakati ya Serikali ya Rais Samia kuhusu akiba ya Chakula Nchini

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Leo Novemba 22,2022. Rais Samia Suluhu amezindua ghala lenye uwezo wa kuhifadhi nafaka tani 25,000 pamoja na vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 15,000 ambavyo vyote kwa pamoja vina uwezo wa kuhifadhi tani 40,000. Lengo la Serikali ni kujenga maghala mengi zaidi nchini ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula hadi kufikia tani 500,000 Desemba 2024.

Pamoja na hayo Serikali inaimarisha sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula nchini. Msimamo wa Serikali ni hakuna mtanzania atakayekufa kwa njaa. Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kununua nafaka, kuzihifadhi na kuuza kwa wananchi inapotokea bei ya nafaka imepanda zaidi.

Rais Samia Suluhu ameanza ziara ya siku 2 mkoani Manyara, Katika ziara hiyo siku ya Kesho anatarajia kuzindua hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara pamoja na kukagua ujenzi wa miundombinu, kuona hali ya utoaji Huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
 
Back
Top Bottom