Kwanini tuheshimu uhuru unaodidimiza maendeleo ya watu? Kwanini iwe kwenye dini tu ndo kuwe kunakuingilia uhuru na si maeneo mengine?
Swali zuri.
Kwa sababu, kwanza, maendeleo yanaendana na utashi wa watu. Hutakiwi kujichukulia wewe unachoona ni maendeleo kuwa ndicho maendeleo.
Kwa mfano, maendeleo ni lazima yaje na uhuru wa kujichagulia. Maendeleo bila uhuru wa kujichagulia ni utumwa. Sasa utawaleteaje maendeleo, kwa mfano uwajengee majumba ya maghorofa na viwanda, watu ambao nia yao ni kukaa kwenye vibanda vyao vya asili na kilimo chao cha asili?
Mwalimu Nyerere alienda Umoja wa Mataifa mwaka 1959 katika harakati za kudai uhuru. Akawa anahojiwa katika TV show moja, show ya Mama Roosevelt New York City. Video ipo Youtube. Katika ile show, Nyerere aliulizwa, wewe unataka watu wako wapewe uhuru mjitawale, lakini mbona nyie watu kama hamjafikia uwezo wa kujiendesha nchi bado? Hamna wasomi wa kutosha, hamna ujuzi wa kuendesha nchi kisasa etc. Nyerere akawajibu kifalsafa sana, kwa mfano. Akasema, ukimkuta mtu kavaa koti lake, ukamnyang'anya, ukasema hili koti hujui kuvaa, kwanza kubwa halikutoshi, nipe mimi. Baada ya muda yule mtu akaja kudai koti lake, akisema sijali kama koti kubwa, sijali kama koti halinitoshi, najali kwamba koti ni langu, nipe mwenyewe koti langu nivae.
Nyerere alikuwa anaongelea haki ya self determination, kwamba, whether mtu anajua kuutumia uhuru wake si hoja, hoja ni kwamba uhuru ni wake apewe.
Wewe unachosema ni kama kile alichoulizwa Nyerere, unasema hawa watu wanyang'anywe makoti, kwa sababu si size yao, hawajui kuvaa. Tuwafundishe. Lakini labda unavyopenda wewe si wanavyooenda wao.
The transcripts and video of the Nyerere Interview are available here
One of the key leaders in Africa's nationalist movement has implored the major nations of the world to keep from exploiting the immediate needs of new African nations in order to involve them in international politics. Julius Nyerere (en yuh RAY run), guest of Mrs. Eleanor Roosevelt on her...
americanarchive.org