Naam vitabu vyote vya Allah vilishushwa, hapa naongelea Zaburi, Taurati, Injili na Qur'an.Wanasema imeshushwaje, yaani ilidondoka kutoka juu au ni vipi! Kwa hiyo hicho kitabu hakina mwandishi?
Nini maana ya kushushwa ? Tunaposema Qur'an imeshushwa tunamaanisha ya kuwa Qur'an yote imeteremshwa Moja kwa moja toka kwa Allah kupitia Malaika wake mtukufu Jibril. Qur'an imeshushwa mpaka kukamilika kwake kwa miaka 23.
Qur'an Haina muandishi kwa maana mtunzi bali ilikusanywa na kuwekwa katika kitabu yaani kuandikwa kwenye kitabu mpaka kutufikia sisi Leo hii.