Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Labda nirudi kukufundisha Sarf (صرف) na nikuelekeze kuwa tuna مفرد (mufrad) pia tuna مُثَنَّى (muthanna) na tuna جمع (jamaa)...
Umejifaragua unifundishe Swarf, hiyo Swarf siioni hapo kwenye maelezo yako zaidi ya kutaja majina tu.

Hili achana nalo halina nafasi hapo.
 
Ila acha kwanza nikuache na hii aya ya 113 ...
Huyu ni Mwanachuoni Kutoka Lamu ndyo aliyetafsiri na kufanya Comentary kwenye hii apps vipi unasemaje mkuu..

Kaandika Biblia hapo kwenye Al kitaba...
Huyu muongo hii maana haipo popote pale.

Anaitwa nani huyo Mwanachioni ?
 
Ukisoma challenge nyingi za hakuna Mungu na kuchallenge maandiko hakika utapotea,utakua nao na utakiri Mungu hayupo...
Amini nakwambia yupo mkuu kutuzidi sisi japo dini nyingi zinapotosha.

Nimeamua kutokusoma nyuzi kama hizi tena,mana nimekaripia kupotoka.
Hata hii nyuzi nimesoma kichwa cha habari tu,sijasoma comments hata moja,ushawishi na doughs ni nyingi.
MUNGU YUPO NA NI MKUU SIKU ZOTE,
alamsikii
 
Sio Pekee yake kuna wanchuoni wengi sana wa kuaminika wana Tafsiri hiyo..
Unataka nikutajie..

1..Abdullah Yusuf Ali
Screenshot_20231213_071533_Adobe Acrobat.jpg

Anaposema same book anamaanisha kilikuwepo kitabu kimoja Kati yao au kitabu kimoja kilichofana...

BTW wako wengi sana wanachuoni na wanakubaliana kwamba kulikuwa na kitabu kimoja kilichohusisha vtabu Vilivyotajwa torah na zaburi na vingine..
 
Hii kanuni umeipata wapi kijana ?
huwa nafurah kuitwa kijana inanikumbusha miaka hiyo!

Mkuu ntapuuza ulichoandika maana ninaamini wewe umesema Ni mtu unayejua angalau kanuni chache za ki Sarf (صرف)..

kinachonishangaza ni wewe kutokujua matumizi ya Neno Al..
Sidhani kama hapa ni sehemu sahihi ya kufundishana kiarabu..

Ila kwakuwa umetaka kanuni nitakupa Uende ukasome baadhi ya vitabu

TAfuta vitabu kama lughat-ul-Arabia au Arabic Course cha Madina islamic University kilichoandikwa na Dr Abdul Rahim..Kitakusaidia naamini viko vitabu mpaka version 3 (Na uhakika utajifunza vizuri kiarabu)..

Pia kuna vitabu vya Darasa la kwanza mpaka la saba vya kujifunza Arabic and Islamic Grade one up to grade 6 of islamic study viluvyoandikwa na Abdul Malik Mujahid pamoja na Dr molvi Abdul Aziz..
Anza na hivyo kwanza humo kuna kanuni zote utazikuta ambazo nilisoma miaka hiyo mingi...
 
Wakuu habari zenu?binafsi nimekuwa nikifuatilia mijadala mingi sana kuhusu mikanganyiko(contradiction) katika vitabu vya dini.

Nimekuwa nikifatilia nyuzi nyingi za kiranga kuhusu kupinga uwepo wa mungu, tukitoa mihemko tukajenga hoja kwa mantiki (logical) character ya mungu mwenye nguvu zote, mwenye upendo wote na ajuaye yote hayupo na haiwezi kufit kwenye mizani ya mantiki.

Nimekuwa nikisoma Biblia na imekuwa ikijikanganya yenyewe na bado ikidai kwamba mungu huwa hakosei. Leo nitaonyesha baadhi ya mikanganyiko hiyo ambayo hata kiranga amekuwa akiiweka.hizi ni baadhi ya verse zenye mikanganyo👇

Mwanzo 1:3-5 BHN
Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa. Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza, mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.

Mwanzo 1:14 BHN
Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka

Mwanzo 1:11-13 BHN
Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu.

Mwanzo 2:4-9 BHN
Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa. Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia, Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima. Hata hivyo, maji yalitoka ardhini yakainywesha ardhi yote. Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai. Kisha Mwenyezi-Mungu akapanda bustani huko Edeni,

Mwanzo 1:26-27 BHN
Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. Hapa mungu aliumba mwanamume na mwamke.

Mwanzo 2:7 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai.

(Mbele kidogo mungu anaumba mwanaume)utaona jinsi gani anavyosahau kurekodi matukio katika mtiririko ulio sahihi.

Mwanzo 6:6 BHN
Mwenyezi-Mungu alisikitika sana kwa kumuumba binadamu duniani. Mwenyezi-Mungu alihuzunika sana moyoni mwake

Hesabu 23:19 BHN
Mungu si mtu, aseme uongo, wala si binadamu, abadili nia yake! Je, ataahidi kitu na asikifanye, au kusema kitu asikitimize?

Kutoka 12:13 BHN
Basi, ile damu itakuwa ishara yenu ya kuonesha nyumba mtakamokuwa. Nami nitakapoiona hiyo damu, nitawapita nyinyi, na hamtapatwa na dhara lolote wakati nitakapoipiga nchi ya Misri.

Mithali 15:3 SRUV
Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.

( kwenye kutoka mungu wa kiyahudi anatoa maagizo wapake damu kwenye vizingiti vya milango ili asije kujichanganya, lakini mungu huyo huyo anajinasibu katika mithali macho yake yapo kila mahali)

Kutoka 20:14 BHN
“Usizini.

HOSEA 1:2
2 Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana.

Karibuni tujadili bila kashfa tujadiliane, hizi ni baadhi ya mikanganyiko iliyopo katika biblia.

Kwanini mungu mkamilifu kitabu chake kiwe na mikanganyiko kiasi hiki?

Mungu anasifa zote za binadamu anasahau, anabadili mawazo yake, ana hasira, Ana wivu, katili, na tabia zingine nyingi za kibinadamu.
Mkakanganyiko upi mkuu
 
Sio Pekee yake kuna wanchuoni wengi sana wa kuaminika wana Tafsiri hiyo..
Unataka nikutajie..

1..Abdullah Yusuf Ali
View attachment 2841055

Anaposema same book anamaanisha kilikuwepo kitabu kimoja Kati yao au kitabu kimoja kilichofana...

BTW wako wengi sana wanachuoni na wanakubaliana kwamba kulikuwa na kitabu kimoja kilichohusisha vtabu Vilivyotajwa torah na zaburi na vingine..
Hili tatizo lingine kumbe hata wanachuoni huwajuo, Sasa Yusuf Ali anaaminika kwa kina nani ?

Soma Tafsiri Ibn Kathir, soma Tafsiri al-Qurtubiy, Soma Tafsiri ya Imam Sa'ad na wengine katika wanazuoni wa Tafsiri uone kama Kuna Biblia hapo.
 
huwa nafurah kuitwa kijana inanikumbusha miaka hiyo!

Mkuu ntapuuza ulichoandika maana ninaamini wewe umesema Ni mtu unayejua angalau kanuni chache za ki Sarf (صرف)..

kinachonishangaza ni wewe kutokujua matumizi ya Neno Al..
Sidhani kama hapa ni sehemu sahihi ya kufundishana kiarabu..

Ila kwakuwa umetaka kanuni nitakupa Uende ukasome baadhi ya vitabu

TAfuta vitabu kama lughat-ul-Arabia au Arabic Course cha Madina islamic University kilichoandikwa na Dr Abdul Rahim..Kitakusaidia naamini viko vitabu mpaka version 3 (Na uhakika utajifunza vizuri kiarabu)..

Pia kuna vitabu vya Darasa la kwanza mpaka la saba vya kujifunza Arabic and Islamic Grade one up to grade 6 of islamic study viluvyoandikwa na Abdul Malik Mujahid pamoja na Dr molvi Abdul Aziz..
Anza na hivyo kwanza humo kuna kanuni zote utazikuta ambazo nilisoma miaka hiyo mingi...
Nimesoma hivyo vitabu vya Sheikh Fuad Abdulrahiim Allah amrehemu, amekufa mwaka huu, hakuna hiyo kanuni inayosema kwamba "Al" inaongelea umoja wa kitu, sababu "Al" ambayo siyo ziada katika neno huonyesha alama ya jina na kitu chenye kujulikana. Sababu unaweza kuwaongelea Wanaume wengi wenye kujulikana, vitabu vingi vyenye kujulikana na "Al" inakuwepo katika majina hayo.
 
Uislamu huujui, Waraqah bin Nawfal hakuwa na Biblia, bali alikuwa na mabaki na elimu ya vitabu vya kale yaani Taurati na Injili, ndio maana ikawa rahisi sana kwake kuamini ya kuwa Muhammad ni Mtume ajaye. Japokuwa Kuna tofauti kwa Wanazuoni ya kuwa je Waraqah ni swahaba au la.

Tukisema Biblia kila mtu anajua inakusudiwa nini, Sasa hii ambayo ni maarufu na inayo julikana kwa watu, mnipe ushahidi kama ilikuwepo kipindi cha Mtume. Jibu hamna, Sasa msiseme kama mmejibu swali langu wakati hamjajibu, wakati huo huo mnasema Biblia ina maana Pana na maana yake ya ujumla ni mkusanyiko wa vitabu kadhaa. Halafu bado mnadai mmethibitisha ya kuwa Biblia ilikuwepo kipindi cha Mtume.

Siwezi kukulazimisha kama umeamua kubisha tu

Tatizo lako unataka ushahidi lazima utokane na vitabu vya imani yako tu

Umetajiwa mwaka ambao vitabu vya Bibilia ya kwanza kuwa compiled kama single book ni mwaka ambao Mudi alikua hajazaliwa bado...... hujalikanusha hili au kuliridhia ila bado unataka ushahidi

Kanusha kwanza hili kwa HOJA na ushahidi kuwa sio kweli
 
Hili tatizo lingine kumbe hata wanachuoni huwajuo, Sasa Yusuf Ali anaaminika kwa kina nani ?

Soma Tafsiri Ibn Kathir, soma Tafsiri al-Qurtubiy, Soma Tafsiri ya Imam Sa'ad na wengine katika wanazuoni wa Tafsiri uone kama Kuna Biblia hapo.
Mkuu wanazuoni wako wengi sana hata Tanzania tuna baraza la Ulamaa na baraza la wanazuoni pia..

Zote nimezisoma na ninazo kama softcopy walichosema Ni same book kitabu kimoja..
Japo Yusuf ally ameenda mbali na kufafanua kitabu hicho
 
Ukisoma challenge nyingi za hakuna Mungu na kuchallenge maandiko hakika utapotea,utakua nao na utakiri Mungu hayupo...
Amini nakwambia yupo mkuu kutuzidi sisi japo dini nyingi zinapotosha.

Nimeamua kutokusoma nyuzi kama hizi tena,mana nimekaripia kupotoka.
Hata hii nyuzi nimesoma kichwa cha habari tu,sijasoma comments hata moja,ushawishi na doughs ni nyingi.
MUNGU YUPO NA NI MKUU SIKU ZOTE,
alamsikii
Mungu Yuko kwenye mawazo yako Tu
 
Siwezi kukulazimisha kama umeamua kubisha tu

Tatizo lako unataka ushahidi lazima utokane na vitabu vya imani yako tu

Umetajiwa mwaka ambao vitabu vya Bibilia ya kwanza kuwa compiled kama single book ni mwaka ambao Mudi alikua hajazaliwa bado...... hujalikanusha hili au kuliridhia ila bado unataka ushahidi

Kanusha kwanza hili kwa HOJA na ushahidi kuwa sio kweli
Sijaweka hilo sharti, hii Biblia thibitisha ya kuwa ilikuwepo kipindi Mtume yupo. Popote utakapo toa huo ushahidi kama wa kweli nitaukubali.
 
Mkuu wanazuoni wako wengi sana hata Tanzania tuna baraza la Ulamaa na baraza la wanazuoni pia..

Zote nimezisoma na ninazo kama softcopy walichosema Ni same book kitabu kimoja..
Japo Yusuf ally ameenda mbali na kufafanua kitabu hicho
Hauko serious Tanzania hakuna wanazuoni, inaonekana hujui maana ya "Wanazuoni", Tanzania Kuna wanafunzi waliofaidika na ndio masheikh zetu na walimu wetu,labda huko mbeleni wake kuwepo ila kwa Sasa hakuna.

Hilo Baraza la Ulamaa ni jina tu, ila ukiwaweka kwenye mizani hakuna mwanazuoni hata mmoja, sababu Kuna sifa bainifu za wanazuoni.

Ukisoma Tafsiri zote za Qur'an za wanazuoni hapo inaongelewa Injili na Taurati, na sio Biblia. Hao wameitwa watu wa kitabu kutokana na wali teremshiwa Taurati na Injili kwa nyakati tofauti. Ila wakaachana na vitabu hivyo na kuanza kubadili maandiko kwa maana na baadhi ya wakati Matini kabisa.
 
Kama unabisha kuhusu Mabarza ya wanazuoni Tanzania bhasi sasa sina haja ya kuendelea kubishana na wewe..

1.Tanzania kuna Baraza la ulamaa/Baraza la wanazuoni kutoka bakwata (ambaye mwenyekiti wake ni Mufti wa Tanznia Sheikh Dr. zuberi (PhD)

2.Tanzania kuna Baraza la Wanazuoni wa Kishia likiongozwa na mwenyekiti wake Sheikh Hemed Jalala Mwakindege (Maulana)

3.Tanzania kuna Baraza la wanazuoni 'Ilima' wa BASUTA (Baraza la Answar Sunna Tanzania) likiongozwa na MUDIR Sheikh Salm Barahyan (Mudir)

4.Tanzania kuna Baraza la Wanachuoni na 'Ilma' maulamaa kutoka Jumuiya ya Salafiya wakiongozwa na Sheikh kassim Mafuta

Zipo jumuiya zingine ahmadiya,Qadiriya ,Etc...

Wote Waliomo kwenye mabaraza ya ulamaa (Mabaraza ya wanazuoni)..
wana elimu ya kutosha sana..

Na Wengi Wamesoma Vyuoni vingi ikiwemo vyuo vya madina,Masri (Misri), algeria Na asilimia kubwa wana PhD katika elimu ya kiislamu na elimu zingine wengi ni ni Ma Fuqha, Muhadithiina,...

unataka kulinganisha na wewe MUQALLID..

mkuu Niambie kwenye baraza lolote la ulamaa Tanzania nani ambaye unaweza kukaribiana elimu (Kama unawajua lakini member wake)
 
Unazijua sifa za wanachuoni ?

Mimi bado mwanafunzi na naendelea kujifunza, ila tumesomeshwa sifa za Wanazuoni na walimu zetu.

Nukta ya 4 umeandika uongo wa wazi na kumzulia sheikh wetu, huyo ni katika masheikh zetu. Hakuna Jumuiya ya Salafiya Tanzania.
 
Ila kuna nini hahaha 😅😅😅
Mkuu nimeishi Tanga kwa muda mrefu sana Hili si swala la kunidanganya mimi ..

Unajua masalafi mnajidanganya sana

Najua vizuri nyinyi Masalafi hampendi kuitwa Jumuiya mnapenda kujiita Watu wa Da'awa..
Wakati kiuhalisia Ni Jumuiya 😅😅

Mkuu Kabla sijaondoka Tanga na Zanzibar Na kuja huku Kwenye nchi za Magharibi nimekaa na wanazuoni mbalimbali na nilifanikiwa kusomeshwa Nao pia..

NA masheikh Wengi miaka hiyo kama Sheikh Mafuta mwenyewe, Sheikh Uthmani maalimu (Nilisoma Tarekh kwake mbobezi sana huyu), Sheikh izudin nilifanikiwa kuonana naye tu mwaka 2016 akiwa lamu tukapiga story mbili tatu..He's very humble kwakweli Kijana ana elimu lakini si mwenye kiburi

Masheikh niliotamani kusoma kwao kipindi nikiwa mwislam ni shikh Bachu..

KWANINI NAKWAMBIA HIVYO

KWA SABABU MIMI ni moja WA watu naowaheshimu sana sana masheikh na wachungaji hata kama sifati tena njia za dini ila wataendelea kuwa Waliochangia mimi kuwa huru ..
Nilichoshangaa wewe ni kuwatukana Tena kwa kiburi masheikh wako kwamba sio wanazuoni 😁😉

NB: KWAHYO UNAMAANISHA SHEIKH MAFUTA SIO MWANAZUONI M?
 
Uislamu huujui, Waraqah bin Nawfal hakuwa na Biblia, bali alikuwa na mabaki na elimu ya vitabu vya kale yaani Taurati na Injili, ndio maana ikawa rahisi sana kwake kuamini ya kuwa Muhammad ni Mtume ajaye. Japokuwa Kuna tofauti kwa Wanazuoni ya kuwa je Waraqah ni swahaba au la.

Tukisema Biblia kila mtu anajua inakusudiwa nini, Sasa hii ambayo ni maarufu na inayo julikana kwa watu, mnipe ushahidi kama ilikuwepo kipindi cha Mtume. Jibu hamna, Sasa msiseme kama mmejibu swali langu wakati hamjajibu, wakati huo huo mnasema Biblia ina maana Pana na maana yake ya ujumla ni mkusanyiko wa vitabu kadhaa. Halafu bado mnadai mmethibitisha ya kuwa Biblia ilikuwepo kipindi cha Mtume.

Kwahiyo hoja yako ni kwamba Bibilia ilikuwepo ila SIO BIBILIA HII TUNAYO IJUA SASA? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukisoma challenge nyingi za hakuna Mungu na kuchallenge maandiko hakika utapotea,utakua nao na utakiri Mungu hayupo...
Amini nakwambia yupo mkuu kutuzidi sisi japo dini nyingi zinapotosha.

Nimeamua kutokusoma nyuzi kama hizi tena,mana nimekaripia kupotoka.
Hata hii nyuzi nimesoma kichwa cha habari tu,sijasoma comments hata moja,ushawishi na doughs ni nyingi.
MUNGU YUPO NA NI MKUU SIKU ZOTE,
alamsikii
1 Wakorintho 15:33-34
Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu.
 
Wakuu habari zenu?binafsi nimekuwa nikifuatilia mijadala mingi sana kuhusu mikanganyiko(contradiction) katika vitabu vya dini.

Nimekuwa nikifatilia nyuzi nyingi za kiranga kuhusu kupinga uwepo wa mungu, tukitoa mihemko tukajenga hoja kwa mantiki (logical) character ya mungu mwenye nguvu zote, mwenye upendo wote na ajuaye yote hayupo na haiwezi kufit kwenye mizani ya mantiki.

Nimekuwa nikisoma Biblia na imekuwa ikijikanganya yenyewe na bado ikidai kwamba mungu huwa hakosei. Leo nitaonyesha baadhi ya mikanganyiko hiyo ambayo hata kiranga amekuwa akiiweka.hizi ni baadhi ya verse zenye mikanganyo👇

Mwanzo 1:3-5 BHN
Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa. Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza, mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.

Mwanzo 1:14 BHN
Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka

Mwanzo 1:11-13 BHN
Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu.

Mwanzo 2:4-9 BHN
Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa. Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia, Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima. Hata hivyo, maji yalitoka ardhini yakainywesha ardhi yote. Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai. Kisha Mwenyezi-Mungu akapanda bustani huko Edeni,

Mwanzo 1:26-27 BHN
Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. Hapa mungu aliumba mwanamume na mwamke.

Mwanzo 2:7 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai.

(Mbele kidogo mungu anaumba mwanaume)utaona jinsi gani anavyosahau kurekodi matukio katika mtiririko ulio sahihi.

Mwanzo 2:7 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai.

Mwanzo 6:6 BHN
Mwenyezi-Mungu alisikitika sana kwa kumuumba binadamu duniani. Mwenyezi-Mungu alihuzunika sana moyoni mwake

Hesabu 23:19 BHN
Mungu si mtu, aseme uongo, wala si binadamu, abadili nia yake! Je, ataahidi kitu na asikifanye, au kusema kitu asikitimize?

Kutoka 12:13 BHN
Basi, ile damu itakuwa ishara yenu ya kuonesha nyumba mtakamokuwa. Nami nitakapoiona hiyo damu, nitawapita nyinyi, na hamtapatwa na dhara lolote wakati nitakapoipiga nchi ya Misri.

Mithali 15:3 SRUV
Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.

( kwenye kutoka mungu wa kiyahudi anatoa maagizo wapake damu kwenye vizingiti vya milango ili asije kujichanganya, lakini mungu huyo huyo anajinasibu katika mithali macho yake yapo kila mahali)

Kutoka 20:14 BHN
“Usizini.

HOSEA 1:2
2 Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana.

Karibuni tujadili bila kashfa tujadiliane, hizi ni baadhi ya mikanganyiko iliyopo katika biblia.

Kwanini mungu mkamilifu kitabu chake kiwe na mikanganyiko kiasi hiki?

Mungu anasifa zote za binadamu anasahau, anabadili mawazo yake, ana hasira, Ana wivu, katili, na tabia zingine nyingi za kibinadamu.
Biblia ina mikanganyiko mingi sana, nimekua nikpitia Biblia. Ila bado sijapata jibu kabisa nini maana ya Biblia.
 
Back
Top Bottom