Mikasa iliyotokea kipindi wanaigiza filamu za Yesu

Hapo ndipo wanapochanganya na kuona wakristo wanakufuru wakati ni imani tofauti.

YESU NI MUNGU.


Luka 18
19 Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mwema? Hakuna mtu aliye mwema ila Mungu peke yake.
Yohana 17
3 Na huu ndio uzima wa milele: wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli, nakumfahamu Yesu Kristo ambaye umemtuma.


Hapa Yesu alikua anamzungumzia Mungu gani?
 
Subiri waje wakuulize , Mungu anazaliwa ? Mungu anakubali kufa kizembe bila kujitetea?

Yesu ni Mungu kamili ila tu alipovaa mwili wa kibinadamu akaonekana ni binadamu kamili.
Kumbe mara nyingine Mungu wenu huwa anauvaa ubinadamu na huyo huyo mwasema hafananishwi!?

Mna taabu sana waamini
 
Tunajuje kama imetizamwa zaidi bila kuuzwa zaidi?
 
Tunajuje kama imetizamwa zaidi bila kuuzwa zaidi?
Filamu ya Yesu haikutengenezwa kibiashara kwa ajili ya kuuzwa bali ilikua ni mission ya kutangaza Injili ...ndiomana huko vijijini watu huwa wanakusanyika kuangalia sinema ya Yesu free of charge
 
Hivi ni mtangazaji gani aliyetafsiri filamu ya Yesu kwa Kiswahili...jamaa alitisha sana aisee
 
Ona hiyi
 
Soma Mwanzo 1:1-14...

Hapo mwanzo kulikuwa na neno naye neno alikuwa kwa Mungu, naye neno alikuwa Mungu..
Yesu kabla ya kuja duniani alikuwepo mbinguni kama kiumbe wa roho,na yeye ndio kiumbe wa kwanza kabisa kuumbwa kabla ya kitu chochote kile,Methali(Mithali)8:22-31,baada ya Yesu kuumbwa yeye pia alikuwa anashirikishwa katika kazi ya uumbaji,kama hiyo mistari ilivyoeleza Yan alikuwa msaidizi, ndiomaana Kuna mistari inayosema "Tumfanye mtu Kwamfano wetu" hapo Mungu alikuwa anamwambia Yesu,,lakini pia Mungu hawezi kufa ila Yesu alikufa siku3,,soma hapa kidogo Yohana20:17 'Yesu akamwambia acha kuning'ang'ania,kwamaana Bado sijaoanda kwenda kwa Baba.Lakini nenda kwa ndugu zangu,nawe uwaambie,Ninapanda KWENDA KWA BABA YANGU NA BABA YENU na kwa MUNGU WANGU NA MUNGU WENU"
 
Fikiria vizuri kabla ya kumuita Yesu kuwa ni Mungu
Mungu anaukuu wa hali ya juu na hafanishwi na kitu chochote!
Andiko lipo linaloonesha yesu ni Mungu, wakiristo wamegawanyika,wapo wanaamini yesu Mungu na wapo wanaamini ni mwana wa Mungu,na wote wapo sahihi kwa mujibu wa biblia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…