Tulienda ukerewe 2018 kwenye ishu flan kama group hv, bahati mbaya siku tuliyofika kulikuwa na ziara ya uncle Magu, lodge na guest zote kwa pale mjin zilikuwa zimejaa, zunguka kila sehemu holaa.
Baadae kabisa tukapata moja inaonekana ya muda mrefu sana, kuulizia bei elfu 3, ikabidi tulipie kibishi tu tukalala room moja watu watatu muhudumu alitutafutia na godoro tukaweka chini ili tutoshe, toilet ni ya nje, mlango wa kuhamisha, ukiingia unauegesha mlangon ukimaliza unauweka pembeni.
Nyingine ni Arusha, lodge inaangaliana na hospital ya selian ile ya pale town, ipo classic kabisa ina had cctv, walinishangaza tu nimeuliza bei wakaniambia ukilala mwenyewe 40k, ukilala na mtu 50k, sijawah kuikuta sehemu zote nilizotembea hyo...