Mikasa/vituko vya lodge

Mikasa/vituko vya lodge

Kama kuna mtu anapata safari ya Ruangwa Mjini kuna hotel inaitwa Green View vyumba 25k(fan) na 30k(ac) hii hotel ipo vizuri saaaana kwenye usafi changamoto ni kubalance maji ya moto na baridi labda na vile Visabuni vya Eva basi lakini kuhusu usafi nawapa kongole, Nimelala apo mwaka jana na mwaka huu pia.
Na ni mwendo wa dk 2 kwenda stendi...pazuri sana,ila kama bajeti yako nzuri unaeza enda Kidia napo ni pazuri sana
 
kuna guest nishawahi ingia nilisikia kelele tu muda mwingi wanazagamuana hadi saa 9 ikaacha ikaanza tena 11 niliwahi sana kwenda stand ile siku na nililala sana kwenye basi sitasahau
Hiyo ilinipata mwaka Jana, nilienda mwanza kwenye rock city marathon, nikalala mtaa wa kirumba maana sio mbali na rock city Moore tunapoanzia mbio. Aisee vyumba vyote vya hiyo guest ilikua ni kelele tupu, nje ukutani ni kelele, kelele kila mahali watu wanapigana mashine. Sikulala Hadi asubuhi
 
Musoma mara,mwaka 2008,siwezi kusahau ile siku tarehe na mwez nimesahau ila siwezi kusahau,nimefika nikitokea Mwanza nilale asubuhi niende zangu dar kupitia sirari kipindi hicho njia ukiwa bukoba unapitia kampala kwa basi,ukiwa mwanza unapitia sirari,daaah nikachukua lodge,hapo hapo kulikuwa na bar,nikatoka enzi hizo balimi tamu balaa nikaanza kupiga balimi zangu ghafla akaja mshkaj akawa anamzingua muhudumu ambae anahusika na upande wa lodge na kaunta ya vinywa daaaah baada ya muda jamaa kaanguka kafa pale pale,cha kushangaza hakuna mlevi wala muhudumu aliostuka wakawa wanasema tu kiburi kimemponza,polisi wakaja wakachukua maiti bila kusema chochote na sisi tuliopo pale,palepale nikapata stor kuwa aliwekewa sumu ya mamba,usiku nimerudi chumbani maji yakawa hayatoki nikatoka kumgongea yule dada muhudumu,kwanza hakuitika ila aliuza nan wewe nikasema mm mpangaji wa chumba flan akauliza unataka nini,nikamwambia maji hakuna,akaniuliza kwahiyo[emoji3] daah nilipokumbuka tukio la yule jamaa aliokufa,nikamjibu hakuna kitu dada nimeuliza tu labda yatarudi na mabomba yapo wazi hivyo yatamwagika[emoji3][emoji16]
 
kuna guest nishawahi ingia nilisikia kelele tu muda mwingi wanazagamuana hadi saa 9 ikaacha ikaanza tena 11 niliwahi sana kwenda stand ile siku na nililala sana kwenye basi sitasahau
Hiyo ilinikuta gesti moja Shinyanga stendi
 
Morogoro nimekutana na Mwalimu tukawa tunaangalia promo ya heineken, nikamnunulia bucket 🪣 mbili mara kaanza kukata mauno na yeye kama wacheza shoo, tumefika chumbani katapikia mashuka yote, nikabeba kibegi changu nikasepa, sijui nini kiliendelea,uzuri huwa naandika majina na no za simu za uongo.
 
Hiyo ilinipata mwaka Jana, nilienda mwanza kwenye rock city marathon, nikalala mtaa wa kirumba maana sio mbali na rock city Moore tunapoanzia mbio. Aisee vyumba vyote vya hiyo guest ilikua ni kelele tupu, nje ukutani ni kelele, kelele kila mahali watu wanapigana mashine. Sikulala Hadi asubuhi
Walikuwa ni washiriki wenzio wa marathoni maana ni njia mpya ya kufanya umalaya na ukahaba. Hakuna lolote la maana huko kwenye hizo marathoni zaidi ya hiyo. Mungu atusaidie kwa kweli.
 
Miaka miwili nilienda vwawa mbozi kuna guest house ipo karibu na shell ya ilasi inaitwa mkulima guest house,chumba chenye choo,tv,maji ya moto ya heater,kitanda 6x6,wali maharage bure,nguo zisizidi 2 unafuliwa na viatu unabrashiwa kwa sh 10,000/=!!kwa kweli nilistaajabu na wengi hawaamini nikiwahidithia!
Vitu vyote hivyo kwa elfu 10000 ?
 
Back
Top Bottom