Jamani mimi hapa kwenye hiki kisa cha maisha yangu toka nilipoanza kusimulia tangia tukiwa Tarime sijawahi kukashifu dini za watu,sijawahi kumkashifu mtu,na kama mtakumbuka kuna wale jamaa ambao niliwaambia kwa sasa ni matajiri wakubwa hapa Dar es salaam sijawahi kuwataja majina yao maana niliona itaniletea shida,haya yule mfanyakazi wetu wakati tukiwa Tarime,jina lake halisi lilikuwa Ashura,je mlitaka nidanganye jina lake?,hilo ndilo lilikuwa jina lake.
Matendo yote niliyoyafanya kwenye maisha yangu hayo yaliyopita hakuna nilichopunguza wala nilichoongeza,isipokuwa kile kisa cha lile pedo(pederi)la baiskeli ndicho sikukimaliza kwasababu ya maneno ya watu.
Majina ya watu niliyoshiriki nao kwenye maisha ni majina halisi na wale ambao sikuwataja kuna sababu zilizofanya nisiwataje.
Mtu kama Zainati,Yusta,Scolastica,Ezekiel na Anton,hayo ni majina yao halisi.
Alama niliyowekewa mkononi na yule Malaika bado ninayo,kuna alama nilikatwa na kisu nikiwa maeneo fulani panaitwa Matemanga mkoani Ruvuma bado ninayo,kuna alama pia ninayo kidoleni ambayo nilipata ajali nikiwa kwenye gari langu kabla ya kufilisika bado ninayo,pia kidole changu kidogo cha kushoto kimepinda kabisa baada ya kusukumwa nikiwa nimelala kule Tarime.Nyumba niliyoishi nikiwa Tajiri bado ipo pale Igoma na kama mtahitaji ushahidi nipo tayari,nyumba zangu au apartment nilizojenga kule Buhongwa bado zipo kama mkihitaji ushahidi nipo tayari,nyumba yetu ya nyegezi niliyorekebisha bado ipo mkitaka ushahidi nipo tayari,Kaburi la baba yangu kule Tarime maeneo ya Ronsoti bado lipo mkitaka ushahidi nipo tayari,Kabuli la mama yangu kule kijiji cha Sumve wilaya ya Kwimba bado lipo mkitaka ushahidi nipo tayari.
Jamani kwanini watu hawataki kuamini kile ninachokisema?,nifanye nini ili muamini?,au kuyataja hayo majina yenye asili ya kiarabu kama Ashura na Zainati ndilo tatizo?,mlitaka nidanganye?,mbona hata majina ya wakristo nimeyataja?,Kinachofanya mnitupie maneno ya lawama ni nini?.
Toka mwanzo sikutaka kuupotosha uma wa kwasababu najua impact ya uongo.Hiki kisa hivi sasa ninakismulia pale Redio Free Africa kwenye kipindi chao cha SITOSAHAU,hivi nawezaje kusimulia kisa cha uongo ambacho kitafarakanisha jamii?,ninawezaje kusema uongo mbele ya serikali hii ya Tanzania?,hivi kama ninasema uongo endapo serikali ikisema nithibitishe nitaanzaje?.
Ninausema ukweli kwasababu nipo tayari hata serikali ya Tanzania iseme nithibitishe nipo tayari kuthibitisha na wala sihofii kwasababu nilipitia mimi mwenyewe haya maisha.