Mikataba anayoingia Waziri Makamba ina mkono wa mkuu wa nchi? Kwanini hatusikii akiikemea? Wananchi wanabakia kunung'unika Taifa lao kufisadiwa

Wenye kamba zao ndefu shingoni, si mchezo.
 
Nadhani kila mtu angetakiwa kusoma ,umeeleza vizuri mnooo
 
Kwa namna hiyo bora hao wanasheria wa nje watusimamaie tu kwaenye masilahi ya nishati yetu. Wanasheria wa ndani ni hawa eti Kibatala na Lisu,Malya yaani kesi tu ya kuku hawajawahi kushinda.
 
Kwa ufahamu wangu hutoi tu ushauri ila una toa ushauri kuhusu gesi asilia, uwekezaji wa tr 70 una hitaji ushauri kwa mtu mzoefu
 
UKWELI UTABAKI PALEPALE KUA TZ HAMNA SOFTWARE DEVELOPERS AMBAO NI TALLENTED wanachoweza ni copy na bandika basi. Hala
Sasa hiyo sofware ya kihindi mbona ndiyo imevuruga kabisa performance ya tanesco? Performance ya tanesco watumiaji wa umeme tunaipima kupitia uwepo wa umeme tunapouhitaji.

Sasa toka 70 bil zisainiwe kulipwa kwa ajili ya software, sasa limekuwa jambo la kawaida kukosekana umeme zaidi ya masaa 48. Na ukirudi, tanesco wanaukata na kukatua zaidi ya mara tano ndani ya saa moja?

Waseme wanachohitaji kihalali tuwape sisi tunahitaji umeme.
 
Nadhani mtoa mada yeye focus yake kubwa ni "uzalendo na uzawa". Yaani anataka mtanzania ndio awe mshauri, hata kama uzoefu katika masuala ya negotiations za uwekezaji wa gesi, apewe tu hii advisory role.

Hoja zake za msingi ni zifuatazo:
1. Unajua mazungumzo haya yapo kwenye hatua gani na hata mshauri atafutwe wakati huu...
2. Je, TPDC hakuna wataalam wa gesi
3. Matusi na makasiriko kwa wachangiaji wenye mtazamo tofauti nayeye.

Nadhani hii kazi ya ushauri tumpe mtoa mada Idugunde (kwa sababu yeye ni mtanzania mwenzetu) atashirikiana na Joni Boko pamoja na Harmonize.
 
Chifu usinichekeshe...

Hawa jamaa sio kwa sababu wapo serikalini bali kwa sababu SISI WATANZANIA NI WATU WA OVYO MNO!! Hivi wakati Nimrod Mkono anatupiga na makesi yasiyoisha ya TANESCO, kwani alikuwa ameajiriwa serikalini?!

Tena Mungu anisamehe kama namsingizia Mkono na kampuni yake! Something tells me Mkono & Company Advocates walikuwa wanatengeneza mazingira ya TANESCO kufungua mikesi mingi mingi kwa sababu zile kesi za TANESCO zilimaanisha ni pesa kwa Mkono & Company Advocates!!

Matokeo yake, kesi nyingi tuliangukia pua huku Mkono & Company Advocates wakiwa wameshavuta chao!! I'm sorry man kama nawe upo kwenye private legal sector lakini hoja yangu sio watu wa legal sector peke yake bali Watanzania kwa ujumla wetu ni watu wa ovyo, wabinafsi, wala rushwa, na wezi tusio hata na aibu!!

Wewe leo hii pata kazi TRA halafu uwe na maisha ya kawaida kwa sababu unategemea tu mshahara! Wa kwanza kukuona fa'la ni ndugu zako mwenywe kwamba how come uwe TRA halafu usiwe na maisha mazuri huku wakifahamu vema wanamaanisha nini suala la wewe kuwa na maisha mazuri!!
Ukipitia tovuti za Firm mbalimbali za Sheria kama FB Attorneys, Lex Attorneys, IMMMA nk wamejipambanua vyema kuwa wanatoa ushauri kwa mambo ya biashara za kimataifa, mambo ya madini nk hata hao kweli wameshindwa kuwapa kazi??
Bongo hivi sasa tunao Mining Lawyers. Nadhani hata Zitto Kabwe kwa kupenda kwake alisoma mining law. Hawa watu tunao kwa sababu mining sector ipo chini kwa muda mrefu sasa lakini Oil & Gas Industry hata huko kuanza, tupo bado!

Na kama utakumbuka, back in 2014 ndipo nchi mbalimbali including China na Algeria zikatoa scholarship kwa vijana wetu wakasome Bachelor za Oil and Gas Engineering! Kumbe hata kwenye core sector, hatukuwa na watalaamu kwa sababu mahali kama UDSM back in the days wasingeweza kutoa hizo kozi ambazo zisingekuwa na soko! Hata hiyo TPDC yenyewe ilikuwa more of oil business company na sio oil engineering company!!
Man, unajua wakati namzungumzia Mkono hapo juu, sikufahamu kwamba hapa chini ulimzungumzia!

Hivi ndugu yangu kuna cha kujivunia kutoka kwa Wanasheria waliofanya kazi na TANESCO?! Hivi ni mara ngapi umesikia "TANESCO WAANGUKIA PUA, WAAMRIWA KULIPA BILION XYZ"! Mara ngapi umesikia hayo?
 
Sasa hii Taasisi ya Pura ina manufaa gani ?? Si waivunje tu.
 
Kijana huu mradi umesimamiwa na Tpdc kwa muda mrefu. Tangu utafiti, kulipa fidia wananchi na sasa unatakiwa kutekelezwa.

Unataka kusema Tpdc hawana watalaamu? Kama ni ishu ya kupata makampuni na utalaamu toka nje kwani hatuna nchi marafiki zikatupa msaanda ni kampuni gani zinafaa? Mabalozi huko nje wanafanya nini?

Naomba mtambue hapa kuna upigaji.
 
Tena basi angalau hiyo ingekuwa ndio focus yake ningesema ni mtetezi wa "Made in Tanzania" lakini kimsingi hiyo wala sio focus yake!! Na ndo maana hapo juu kuna mtu nikamuuliza kumbe hii mada ni kwa ajili ya legacy protection....
 
Tony Blair ali seal hii deal.

Kimsingi "hiring" kampuni kama hizi sio shida,. Ni big project inahitaji big firm pia kuishauri serikali sio hawa akina Kabudi.

Hawana hata experience.

Kikubwa na good faith kulinda maslahi ya nchi kwa tozo watakazolipwa.

Shida ni wanasiasa pengine kulazimisha vitu vifanyike kwa maslahi yao katk mazingira ya kushauriwa.
 
Nilisikia Bibi mmoja akisema kila mtu ale kutokana na urefu wa kamba yake.
Ile video watu hawakuangalia yote context ilikua per diem, kwamba mawaziri wasiwanyime manaibu wao kwenda semina na wao wachukue fursa zote. Yani kila mtu aende semina na kupata per diem kwa usawa. Acheni kupotosha
 
Mfumo unahusu kuingiza nguzo na mita zote za TANESCO kwenye GPS kiasi kwamba kila nguzo na kila transforma na kila mita ijulikane ilipo.Kama wataalamu wa kitanzania wapo watengeneze mfumo mbadala wapeleke proposala serikalini na ninaamini kabisa kwamba watafikiriwa.ILA TUACHE MAJUNGU kama hela kupigwa zitapigwa tu na zimepigwa sana.
Jana tena kaibuka na kulipatia mkataba kampuni la huko Uk la Barker and Bottis mkataba wa kuwa kuwa mshauri juu ya utekelezaji wa mradi wa gasi ya asili ya Lindi. Mradi ambao una gharama zaidi ya tril 70.
Kwenye eneo hili unafahamu kabisa kwama wanasheria wetu walivotuangusha kwenye issues nyingi.Uzoefu wetu katika masuala ya mikataa ya gesi na natural gas na madini unaonesha kabisa kwamba tunahitaji utaalam zaidi katika eneo hilo
 
Tulia wewe, kwani pesa imetoka kwenye mfuko wako ama. Ongea na lukuvi plus kabudi utapata majibu murua.

Kwa sasa ukiona mkataba umesainiwa manake before that umepata aprove ya hao jamaa wawili wenye kazi maalumu
 
Kuna wakati utafika yote yatakuwa hadharani!!!
 
Sasa hii Taasisi ya Pura ina manufaa gani ?? Si waivunje tu.
Soma majukumu ya PURA na utaona ni kwanini wanatakiwa kuwepo! Anyway, sikumbuki vizuri kuhusu PURA, I wish ningepitia tena upya sheria iliyounda PURA lakini kama kumbukumbu zangu zipo sawa, hawa wamepewa majukumu ya kusimamia Midstream and downstream segments of gas and oil industry.... correct me if am wrong!!

Sasa kama nipo sahihi kwamba watasimamia Midstream and downstream segments, hawa hawatahusika na Upper stream segment kwa sababu wata-deal na local contents ambayo kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta na Gas ya mwaka 2015, hiyo sector inatakiwa kuwa operated na Watanzania wenyewe, ingawaje tukifanya masihara, oil companies kama vile Total and the like, wanaweza kujipenyeza hata huku kwenye Midstream and downstream kwa sababu na kwenyewe kuna pesa sana, na kwenye nchi zingine hizi multinational companies huwa zinajiingiza hadi kwenye Midstream and downstream segments!!

Sijafuatilia hili suala la Makamba kuajiri hiyo hiyo foreign company na kwahiyo sifahamu kama ni kwa ajili ya kuishauri serikali kwenye Upper stream segment au kote kote!!
 
Mkuu kufanya survey kwa Gps au Totatl station na kutengeneza mchoro mpaka kampuni ya nje?

Wanasheria kutuangusha huyegemea na mkuu wa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…