Mikataba ya $300 ya kuwa Housegirl Uarabuni haina tija kwa nchi

Mikataba ya $300 ya kuwa Housegirl Uarabuni haina tija kwa nchi

Serikali inatia aibu wakati mwingine.

Imejikita kuwasaidia madada wa Tanzania kuwa housegirls huko Uarabuni badala ya kuwasaidia diaspora ambao wanafanya kazi za maana na wenye uwezo wa kusaidia nchi kama sheria zikiwekwa sawa. Hatutaweza kuendelea kwa $300 kwa mwezi!

Na unyanyasaji na ubaguzi kwa ndugu zetu huko uarabuni badala yake tusaidie wasomi na wafanyabiashara wetu.

Nchi nyingine wanapeleka Manesi na wanalipwa $70,00-$100,000 kwa mwaka na madaktari wanaingiza zaidi ya $100,000 kwa mwaka na wasomi wengine mmablimbali mfano India inapeleka kwa mikataba wataalamu wa computer engineering. Sisi tunaenda ku sign mikataba ya mahaouse girl kwa $300 kwa mwezi? Kwanini kama ni marafiki zetu wasichukuwe wataalamu wengine?

Wito ni kwa serikali kuweka sheria rafiki kwa diaspora ili waweze kuchangia kama diaspora wengine mfano Kenya badala ya kujishusha na kutegemea wafanyakazi wa ndani!
Kazi aina zote zipo na za viwango vyote zinapatikana Uarabuni, hiyo iliyotajwa ndiyo lowest katika malipo ya kazi zilizopo.

Kama wewe haikufai wapo inayowafaa na wanajenga makwao.

Maafisa wengine hawawezi ku save hizo Tanzania hii.

Kumbuka hizo ni net, kula kulala ni gharama za mwajiri.
 
bongo elimu haina ishu, watu wenye degree tuko nai kwenye boda boda, si bora huo uhausigeli una maokoto ya maana.
Wenye digrii na waliojiongeza kwa kuitumia hiyo degree wako mbali, kuna madogo wamemaliza veterinary SUA wako kitaa pale Morogoro wanatoa huduma mbalimbali kwa wenye mifugo kama mbwa, mbuzi, ng'ombe mpaka kuku..

Nikiwa na shida kwa mifugo yangu nawapigia wanatoa huduma nawalipa. Kuna mwingine ni afisa kilimo watu wanamtafuta kwenye mashamba yao anaenda kutoa huduma na analipwa. Sasa wewe unayesubiria ajira Serikalini endelea kusubiri..
 
Kazi zilizopo huko ni hizo za mahausigeli, hizo kazi zako za wenye elimu haziko, unsdhani huko hakuna wasomi? Wanatakiwa mahausigel huki kwa sababu wazawa wa huko hawazitaki hizi kazi, wanataka hizo za dola 3,000/, kama umeshawahi kuishi nje utaelewa ugumu wa kupata kazi huko, Nenda Marekani na masters yako kutoka UDSM ksma utapata kazi ya maana. Kwanza elimu za Afrika hawazitambui!
USA hatambui elimu ya nchi yeyote nje ya elimu yake, ukienda lazima ufanye recertification.
 
Hapana ukienda kihalali ni ajira nzuri tu, kuna daycare hata huishi kwa boss, na hata ukikaa na boss kama upo official na unapokea Mshahara unaokubalika na Nchi utaenda kwa mtu anaejielewa
Kwani hao walioenda mwanzo, walienda kiwizi wizi, no walikuwa na passport na viza.
 
kwani hao walioenda mwanzo, walienda kiwizi wizi, no walikuwa na passport na viza.
Madalali wanatumia asilimia kubwa.

Mfano Nchi kama UAE ina Watu milioni 10 lakini raia kabisa wa UAE ni kama milioni 1 then kuna Expat wenye hela wachache, unapoenda kuajiriwa Nchi kama hizo una target hao raia na watu wenye hela, na huwezi kuajiriwa nao kama haupo official.

Hawa wanaoingia kwa Njia za Panya wanaishia kwa masikini wenzao wanaanza kuja kulalamika huku.
 
Kenya imemwaga manesi Uingereza kila hospitali, hizo kazi za waarabu za ndani zinafikirisha Sana Sana. Sie sijui tunakwama wapi.
 
Kazi aina zote zipo na za viwango vyote zinapatikana Uarabuni, hiyo iliyotajwa ndiyo lowest katika malipo ya kazi zilizopo.

Kama wewe haikufai wapo inayowafaa na wanajenga makwao.

Maafisa wengine hawawezi ku save hizo Tanzania hii.

Kumbuka hizo ni net, kula kulala ni gharama za mwajiri.

Kwenye hizo kazi kuna kazi gani umesikia ya professional? Jana ameongea balozi anajigamba watu kutengeneza $300 kwa mwezi tena katoa mpaka statistics kwamba wengi wanatoka wilaya ya kondoa🤔

Ukisikia Mtanzania ana kazi ya professional Uarabuni kapata mwenyewe na sio kwenye mikataba ya nchi. Hawa jamaa hawatuthamini kwa kazi za professional wanatuona sisi ni wa kuwa housegirls na kazi na namna hiyo huo ndiyo ukweli.
 
Viongozi wetu ni waoga sana wakiona tunataka kufanikiwa kwa maana tukifanikiwa itakua ngumu kututawala.

Ndio maana kazi nzuri zote wanawapa watoto na ndugu zao.

Sisi ndio kama hivi wanatutafutia uyaya.
 
Kwenye hizo kazi kuna kazi gani umesikia ya professional? Jana ameongea balozi anajigamba watu kutengeneza $300 kwa mwezi tena katoa mpaka statistics kwamba wengi wanatoka wilaya ya kondoa🤔

Ukisikia Mtanzania ana kazi ya professional Uarabuni kapata mwenyewe na sio kwenye mikataba ya nchi. Hawa jamaa hawatuthamini kwa kazi za professional wanatuona sisi ni wa kuwa housegirls na kazi na namna hiyo huo ndiyo ukweli.
sio uarabuni tu, hata ulaya watanzania wanafanya kazi za ovyo ovyo kubeba maboksi, kuogesha vibibi vya kizungu, kuosha barsbara, kufanya usafi migahawani n.k. kupata kazi proffessional nje ni ngumu
 
sio uarabuni tu, hata ulaya watanzania wanafanya kazi za ovyo ovyo kubeba maboksi, kuogesha vibibi vya kizungu, kuosha barsbara, kufanya usafi migahawani n.k. kupata kazi proffessional nje ni ngumu

Acha uongo boss, Hizo kazi wanafanya watu ambao hawana vibali na watu ambao ni wanafunzi, huwezi kaa ulaya miaka 4 legally ukawa unafanya hizo

By the way hizo kazi pia zinapesa ndefu kuliko mishahara ya TZ

Kwa mwezi $2500 ni ndogo??
 
najua ninachoongea, hizo ndio kazi wanaofanya waafrika, tena wanaoishi legally, kama huna makaratasi hata hizo huzipati, mgeni huwezi kupata kazi ya maana ulaya kirahisi, wako lakini ni wachache sana, wengi wao wanaishia kuogesha vibibi vya kizungu na kuosha masufuria migahawani
 
Back
Top Bottom