Mikataba ya $300 ya kuwa Housegirl Uarabuni haina tija kwa nchi

Mikataba ya $300 ya kuwa Housegirl Uarabuni haina tija kwa nchi

$300 ni kama $10 kwa siku, hiyo ni kama 25000 tsh kwa siku hapa Bongo..

Hivi Serikali imeshindwa kuwatengenezea uwezo watu wake na kipato kikawa 25000k kwa siku hapa Tanzania? namaanisha pato la mtanzania liwe 25000k kwa siku tena huyo ni yuke mvivu mvivu ila akikomaa awe na uwezo wa kuingiza hata 50k to 100k kwa mwezi.

Watanzania wangekuwa na vipato vizuri basi hata huo uhouse girl madada wangeufanyia hapahapa Bongo land na kama kwenda ughaibuni basi wangeenda wale wenye competency kwenye proffesional jobs nk, hawa competent na proffesional wakienda inakuwa na faida zaidi kwenye nchi.

Viongozi wa Serikali waache kukimbia majukumu yao na kukimbilia vitu rahisirahisi ili kupata political mileage ilihali vinakwenda kuumiza utu wa raia wao.

Serikali iboreshe mfumo wa elimu na kuhakikisha watanzania wengi wanaipata hiyo elimu, Serikali iwekeze kwa watu wake kwa kuhakikisha wengi wanapata soft skills zinazoendana na kasi ya dunia, serikali ikuze uwekezaji na biashara mitaani huko ili vijana wengi wapate ajira na vipato rasmi..

Viongozi wetu wengi wanawaza kirahisi rahisi sana na kuishia kuja na majibu mepesi kwenye issues ngumu zinazohitaji akili na uelewa mpana.
Naamini watu wenye taalum zinazotambulika wakienda huko ndio inaweza kuwa na faida zaidi kwa Taifa, ni vyema tukawa na watu weengi wenye taalum zaidi wanaoweza kupatikana hapa kuliko kuendekeza haya.
 
Ingekua kwa wazungu walau mmh hawa wengine kigugumizi kidogo mie siwaelewi
Hao waarabu wenyewe wanakimbilia ulaya na America kila siku kutafuta unafuu wa maisha na kukwepa sheria kali za nchi zilizounganishwa na dini.
 
Serikali inatia aibu wakati mwingine.

Imejikita kuwasaidia madada wa Tanzania kuwa housegirls huko Uarabuni badala ya kuwasaidia diaspora ambao wanafanya kazi za maana na wenye uwezo wa kusaidia nchi kama sheria zikiwekwa sawa. Hatutaweza kuendelea kwa $300 kwa mwezi!

Na unyanyasaji na ubaguzi kwa ndugu zetu huko uarabuni badala yake tusaidie wasomi na wafanyabiashara wetu.

Nchi nyingine wanapeleka Manesi na wanalipwa $70,00-$100,000 kwa mwaka na madaktari wanaingiza zaidi ya $100,000 kwa mwaka na wasomi wengine mmablimbali mfano India inapeleka kwa mikataba wataalamu wa computer engineering. Sisi tunaenda ku sign mikataba ya mahaouse girl kwa $300 kwa mwezi? Kwanini kama ni marafiki zetu wasichukuwe wataalamu wengine?

Wito ni kwa serikali kuweka sheria rafiki kwa diaspora ili waweze kuchangia kama diaspora wengine mfano Kenya badala ya kujishusha na kutegemea wafanyakazi wa ndani!
Inasikitisha sana. Nimemsikia balozi yaani jitu zima limesomeshwa na serikali linapigia upatu wenzake kwenda kuwa watumwa!!!!!! Sijawahi ona nchi ikiendelea kwa kuwatuma raia wake waende kuwa housgirl. Ni sawa waende lakini haipaswi kuwa kipaumbele cha mapaka balozi eti anafanya matangazo. Kuna watanzania wangapi wasomi wapo nje ya nchi wenye ujuzi wa kusaidia nchi hata serikali iko kimya tu. Kwa ufupi hili jambo ni la kijinga sana. Hata nikifika uarabuni ni aibu yaani tunaenda kuwa watumwa dahhh hapa Makonda aingilie kati. Na kwa taarifa yake huyu balozi hiyo kondoa imejaa waislamu wenye itikadi kali sana ya ule uislam wa kuua na unaweza kuta wanarudi kuwa magaidi hapa Tanzania. Tena hakuna kitu kibaya kama huyo balazo atakuja kuumbuka kama hao wanaoenda uarabuni kuja kugundulika wanafundishwa uislamu wa itikadi kali.
 
Hata u housegirl nao ni kazi
Hivi unafikiri Uarabuni hakuna wasomi?
mtoa mada usidharau kada hii watu wote hawawezi kuwa ma dr,engineer, kwa kule uarabuni hawana shida nao wapo wengi tu kada hii ya housegirl ndio hawana.

Amini usiamini ukiona mtanzania kaenda kusoma USA au Canada kajenga kwao na ana gari kali aliyoyafanya huko ni siri yake pengine nitoke siri wengine wanafanya kazi kuosha vyombo mahotelini,ulinzi usiku,kuosha wazee,kupiga rangi nyumba,kifyeka majani n.k

Nina dada yangu alikuwa USA hapa nchini aliondoka kama Nesi lakini kufika kule kupata kazi ikawa shida ikabidi aende kwenye vituo vinavyotunza wazee akawa kazi yake ni kuwaosha na tena wengine wakijiharishia.

Ninapoongea muda huu ameshusha bonge moja ya li mansion nikitumia nyumba nakosea na ana gari kali mno na amefungua miradi mingi familia nzima tunamuangalia yeye.

Wewe kaa na tai yako by the way nahisi unatokea ule mkoa wa majivuno no money in pocket too much sheria na ubishi

Mjengo wa sister huo hapo hapo kwenye mpapai hapa hapa bongo.Mungu ambariki aendelee kubaki huko huko akizeeka akirudi atakuwa anapeta Mansion.PNG
 
Kwenye hizo kazi kuna kazi gani umesikia ya professional? Jana ameongea balozi anajigamba watu kutengeneza $300 kwa mwezi tena katoa mpaka statistics kwamba wengi wanatoka wilaya ya kondoa🤔

Ukisikia Mtanzania ana kazi ya professional Uarabuni kapata mwenyewe na sio kwenye mikataba ya nchi. Hawa jamaa hawatuthamini kwa kazi za professional wanatuona sisi ni wa kuwa housegirls na kazi na namna hiyo huo ndiyo ukweli.
Unafikiri Watanzania wote waliopo huko ni mahausigeli?

Wengi wa hao mahausigeli wanafanya kazi jwa Watanzania "skilled" waliopo huko.

Tuulize tuliofika nchi hizo tukufahamishe.
 
Serikali mngejuwa wanayofanyiwa hawa dada zetu na waarabu,,

Basi msingeingia mkataba wa kitumwa kama huo wa Saudi Arabia..

Kwa kifupi,

Mwanamke wa kiafrika akifika huko anakuwa ni mtumwa wa ngono kwa wanaume wa karibu,
Mbaya Zaidi wanaingiliwa bila ridhaa yao.

Nasikitika Sana..

Kwann hamthamini utu wa mwafrika?

Kama kwl.mnataka kusaidia watanzania basi chukueni vijana wa kiume,,
Zipo fursa nyingi sn kwa vijana wa kiume kuliko kuleta wasichana na kugeuzwa watumwa wa ngono.

Mkipuuza hili,,,mtakuja kukumbuka hii comment wakati ishakuwa majuto kwa mabinti na dada zetu.

Inchi Salama ya kupeleka wasichana Ni Dubai au Qatar na sio Saudi Arabia wala Oman.
nani kakudanganya? tuna ndugu zetu huko Saudia wa kike kila siku tunaongea nao kwenye simu na video call tunaona maisha wanayoishi, hakuna ubaguzi wowote na wana mabalozi wa tanzania huko wana mawasiliano nao ya karibu. Unaongea kitu usichokijua.
 
MADANGURU YAPO DAR VIPI HAPO ?
Madanguro yapo kila mahali duniani Lakin wanafanya kwa ridhaa yao,na kujipatia kipato,
Na wala sio ya kuingiliwa kwa nguvu na baba na family nzima.

Wewe unaonaje mfano Dada yako au mama yako aingiliwe na wanaume tofauti bila ridhaa yake? Sababu tu ni mfanyakazi wa ndani,,

Mwarabu kwake imeshuka Dini tu ,,lakini nje ya hapo ni mshenzi Sana na katili Sana especially Kwa mtu mweusi
.
 
Inasikitisha sana. Nimemsikia balozi yaani jitu zima limesomeshwa na serikali linapigia upatu wenzake kwenda kuwa watumwa!!!!!! Sijawahi ona nchi ikiendelea kwa kuwatuma raia wake waende kuwa housgirl. Ni sawa waende lakini haipaswi kuwa kipaumbele cha mapaka balozi eti anafanya matangazo. Kuna watanzania wangapi wasomi wapo nje ya nchi wenye ujuzi wa kusaidia nchi hata serikali iko kimya tu. Kwa ufupi hili jambo ni la kijinga sana. Hata nikifika uarabuni ni aibu yaani tunaenda kuwa watumwa dahhh hapa Makonda aingilie kati. Na kwa taarifa yake huyu balozi hiyo kondoa imejaa waislamu wenye itikadi kali sana ya ule uislam wa kuua na unaweza kuta wanarudi kuwa magaidi hapa Tanzania. Tena hakuna kitu kibaya kama huyo balazo atakuja kuumbuka kama hao wanaoenda uarabuni kuja kugundulika wanafundishwa uislamu wa itikadi kali.
we fala kweli ungejua Uarabuni watanzania walivyo wengi wala usingeongea, Adu Dhabi kuna mtaa unaitwa Zanzibar, wamejaa watanzania kila kona ni kiswahili tu kinaongelewa hapo toka miaka ya 80s uko. Kwa taarifa yako Watanzania walioko Uarabuni ni wengi kupita walioko huko ulaya na marekani, na wanafuata sheria zote za dini, kama hupendi kunywa sumu na wataenddlea kwenda
 
Madanguro yapo kila mahali duniani Lakin wanafanya kwa ridhaa yao,na kujipatia kipato,
Na wala sio ya kuingiliwa kwa nguvu na baba na family nzima.

Wewe unaonaje mfano Dada yako au mama yako aingiliwe na wanaume tofauti bila ridhaa yake? Sababu tu ni mfanyakazi wa ndani,,

Mwarabu kwake imeshuka Dini tu ,,lakini nje ya hapo ni mshenzi Sana na katili Sana especially Kwa mtu mweusi
.
Umashawahi kufika Dubai, mbona uarabuni tunaenda kila siku hatuoni huo ushenzi? Mbona watanzania wengi sana tuko nao Abu Dhabi sijaona wakilalamika
 
Wasaidie manesi wa Tanzania pia wakafanye nje pia kama Kenya
 
nani kakudanganya? tuna ndugu zetu huko Saudia wa kike kila siku tunaongea nao kwenye simu na video call tunaona maisha wanayoishi, hakuna ubaguzi wowote na wana mabalozi wa tanzania huko wana mawasiliano nao ya karibu. Unaongea kitu usichokijua.
Ndugu yako hawezi akakwambiya anayopitia,,Ila Kwa kifupi ni chombo cha starehe cha waarabu.

Umeshawahi kujiuliza kwa nn wanawake wa kiarabu ndy wanaongoza kuwafanyia ukatili wasichana wa kiafrika kuliko mwanaume wa kiarabu kumfanyia ukatili Dada wa kiafrika,

Je imeshajuwa chanzo nn?

Chanzo ni wivu wa mapenzi ambao wamama wa kiarabu wanajuwa kila kitu kinachofanywa na waume zao kwa hawa dada zetu.

Ktk inchi za kiarabu ambazo mwanamke ataishi kwa amani ni Dubai na Qatar lakini sio Saudi Arabia wala Oman.,, Saudi Arabia na Oman huwezi fanya zinaa hovyo mitaani wala Hakuna madanguro.

Qatar na Dubai wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba wapo wengi mitaani,

Saudi na Oman wanawake wa zinaa hovyo hakuna,,Zaidi ya kuwageuza hawa house girls wa ndani kwako kujipooza kwa ngono..

Kama hutaki sikulazimishi..
 
Umashawahi kufika Dubai, mbona uarabuni tunaenda kila siku hatuoni huo ushenzi? Mbona watanzania wengi sana tuko nao Abu Dhabi sijaona wakilalamika
Nimekwambiya Saudi Arabia na Oman sio sehem ya kupeleka wasichana wa Kazi..

Sehem Salama Ni Dubai na Qatar.

Dubai na Qatar madanguro ya kuuza mwili kibao mitaani..
Mwarabu Hana time na house girl wa ndani kwake.

Lakini Saudi Arabia na Oman hesabu mnapeleka watumwa wa ngono kwenye majumba ya waarabu.
 
Kazi aina zote zipo na za viwango vyote zinapatikana Uarabuni, hiyo iliyotajwa ndiyo lowest katika malipo ya kazi zilizopo.

Kama wewe haikufai wapo inayowafaa na wanajenga makwao.

Maafisa wengine hawawezi ku save hizo Tanzania hii.

Kumbuka hizo ni net, kula kulala ni gharama za mwajiri.
Furaha yake angesikia wanaenda kuwa ma-house girl israel au vatcan
 
Ndugu yako hawezi akakwambiya anayopitia,,Ila Kwa kifupi ni chombo cha starehe cha waarabu.

Umeshawahi kujiuliza kwa nn wanawake wa kiarabu ndy wanaongoza kuwafanyia ukatili wasichana wa kiafrika kuliko mwanaume wa kiarabu kumfanyia ukatili Dada wa kiafrika,

Je imeshajuwa chanzo nn?

Mimi naishi nao mkuu siongei kitu cha kusikia..
Chanzo ni wivu wa mapenzi ambao wamama wa kiarabu wanajuwa kila kitu kinachofanywa na waume zao kwa hawa dada zetu.

Ktk inchi za kiarabu ambazo mwanamke ataishi kwa amani ni Dubai na Qatar lakini sio Saudi Arabia wala Oman.,, Saudi Arabia na Oman huwezi fanya zinaa hovyo mitaani wala Hakuna madanguro.

Qatar na Dubai wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba wapo wengi mitaani,

Saudi na Oman wanawake Hakuna,,Zaidi ya kuwageuza house girls wa ndani kwako kujipooza kwa ngono..

Kama hutaki sikulazimishi..
Acha uongo, nimeishi Oman, usijidanganye, kwa taarifa yako mama yangu mkubwa ameolewa na mwarabu wa Oman, nina ndugu zangu ni waarabu, nimeishi nao nyumba moja,kwanza waarabu wanazaliana sana, na idadi ya wanawake ni kubwa kuliko wanaume, na waarabu wanawahi kuoa mapema sana, asilimia kubwa wengi wanaoa btn 16 and 20s years old, tena wakishaoa wanaendelea kuishi kwa wazazi wao, nawajua vizuri, unaposema wanawake hakuna unamaanianisha nini? sema malaya hakuna hapo nitakuelewa, kuna watanzania zaidi ya 12,000 wa kike wanaofanya kazi huko, niambie kati ya hao ni wangapi wamerushwa gorofani? ingawa ni kweli kuna wachache wenye tabia mbaya wanaweza kutembea na waajiri wao, na hapa tanzania wapo
 
Kwani umekatazwa kwenda kuwa hausigeli wa wazungu?

Ikiwa waarabu upo nao mpaka uswazi huwajui, hao wazungu ndiyo unawajuwa?
Faiza hivi nawe huwa ni mwarabu? Wakiongelewa waarabu lazma uibuke
 
we fala kweli ungejua Uarabuni watanzania walivyo wengi wala usingeongea, Adu Dhabi kuna mtaa unaitwa Zanzibar, wamejaa watanzania kila kona ni kiswahili tu kinaongelewa hapo toka miaka ya 80s uko. Kwa taarifa yako Watanzania walioko Uarabuni ni wengi kupita walioko huko ulaya na marekani, na wanafuata sheria zote za dini, kama hupendi kunywa sumu na wataenddlea kwenda
Ujinga mtupu, hapo lazima tupingane sana. Waarabu Tanzania hawatakiwi kabisa maana ni washenzi sana, wali wahasi babu zetu. Nyie wenyewe ukienda uarabuni ni nyani tu hata kama uvae hizo nguo zao utaendelea kubaki nyani na mtumwa. Ni sawa na hilo li balozi linalosisitiza utumwa kwa watanzania.
 
Back
Top Bottom