Handcap kiufupi ni goli/magoli ya mezani. Magoli haya ni ya ziada ukiacha yale ya uwanjani. Yanaweza kua ya kuongezea au kupunguza yale ya uwanjani.
Mfano Leicester anacheza na Southampton, wewe Unampa Southampton Cap ya goli 2 kisha unasema Leicester atashinda, means kua kwa magoli yoyote watakayofungana uwanjani ukichukua ya Southampton ukayaongezea hayo mawili ya mezani still Leicester atashinda.
Uwanjani wanatoka 7-1, lakini na goli za Cap wanakua 7-3 still Leicester mshindi unakua umeshinda mkeka.
Mfano mwengine Liverpool vs Tottenham. Labda unasema umpe cap ya goli mbili Tottenham na umpe win, means kwamba kama wataishia 2-1 ushindi wa uwanjani kwa Liverpool, ukiweka na goli za cap itakua 2-3 ushindi kwa Tottenham, so unakua umekula.
Mfano mwengine lakini hapo hapo kwenye Liverpool. Unampa cap ya goli 1 Tottenham halafu unampa win. Hapo kama mechi imeisha 2-1 uwanjani ina maana kwa Cap itakua imeisha 2-2 so ni draw, na sababu ulisema Tottenham akiwa na cap ya goli moja anakua mshindi hapa unakua umeliwa sababu matokeo with cap ni draw, sio ushindi.
Cap inatumika pia kupunguza magoli ya uwanjani, sio kuongeza tu. Labda useme Atalanta anacheza na Udinese. Kisha useme hata ukimpa Atalanta cap ya (-1) bado atashinda, means kua kwa magoli yoyote atakayofunga uwanjani Atalanta, Hata ukimpunguzia goli 1 still atakua mshindi tu.
Kama uwanjani kapiga goli 7-1, with cap ya (-1) anakua kapiga 6-1 bado ni mshindi tu unakua umekula mkeka.
Jinsi ya kucheza Hii, kama timu ni superior Sana ipe (-goli chache) ishinde, au ile timu inferior ipe (+goli nyingi) ishinde.
Nadhani Maelezo haya yatakusaidia kiasi.