Kama inavyofahamika kuwa SImba Jumapili wanakipiga na Asec Mimosas ya Code vore na tayari walishatangaza viingilio vya mechi hiyo ambapo kiingilio cha chini kabisa kilikuwa ni shilingi 5,000. Jana Mwenyekiti wa Heshima wa Club hiyo akizungumza na wachezaji alipowatembelea kambini kuwatia hamasa, aliamua kushusha viingilio vya mechi hiyo kutoka 5,000 hadi 3,000. Nimemsikia mchambuzi mmoja wa Wasafi mda si mrefu akihoji mustakabari wa wale washabiki ambao wameshanunua Ticket za 5,000 kama watarudishiwa chenji ama lah!.. Kama ningekuwa kiongozi wa wa vipindi wa redio leo ndio ingekuwa mwisho wake wa kufanya uchambuzi wa soka..kwani ameonyesha uwezo mdogo saana wa kufikiria na tena kwa kiwango kisichovumilika .aisee hawa wachambuzi wetu wameshajiona wao ni wakupinga kila kitu hata bila kutumia akili...