Mikeka: Wazee wenzangu wa kuweka mzigo, karibuni tubashiri mechi za leo

Sasa itabdi sisi wakamalia tuanze kumtenga ManCity mana katutesa sana hzi wiki kadhaa..[emoji17]
 
Me nilimpa City over 0.5 Full time nikawa na imani naye kabisa lakini wapiiii
 
Nikeshi auti 2000 nilikua nmeweka 50000 kwa city
pole mkuu mimi nilikuwa nimempa awin either half alikuwa kwenye mkeka wangu(treni) ilipofika half time tu nikacash out 48k fasta...yani second half hawakupiga shuti hata moja,inaweza ikawa ni mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa man city wakamaliza mchezo wakiwa wamepiga vishot viwili tu
 
Sema ni mara ya kwanza chini ya utawala wa Guardiola. City miaka ya nyuma ilikuwa kibonde kashuka sana daraja
 
Tena Single bets nyingi tu zimechana leo.

Porto mwenyewe kasepa na kijiji
Mimi man city kasepa na single yangu.

Ila ni uzembe wangu maana mchana tulikaa kikao na wana tukawa tunamjadili kwamba sasa hivi inabidi tusimdhamini anaruhusu sana magoli.
Sasa mimi nikaingia kichwa kichwa nikampa direct win tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…