USHAURI:-
Ikifika hivyo basi upo kwenye athari kubwa mnoo kiafya na kiakili.
CHIDI Benz alikuwa anatamani mnoo kuwa kama Snoopy Dogy Dogy, hatimae mwenzie anavuta Bangi anakula vizuri yeye anavuta Bangi anakula mama Lishe kitaa,hatimae Umeme umehack ubongo.
Kuna kitu unakiforce au umesoma machapisho ya waliofanikiwa kwa kubet,na unaishi na ndoto zako unazolazimolisha ziwe kweli,na hapo Tayari kichwani una nyumba,magari na mambo teleee.Mbaya sana.
Epuka kucheza Mechi za South,Central and Northern America ambazo zinacheza almost usiku mzima mpaka Alfajir.
Pili,Usiwaze kubet Ili utoboe kimaisha,hapo ndio utapotea mazimaaaa.Ba Jingine kubwa usibet kisa fulani unaemjua kala milioni kumi,muulize alicholiwa.
Usibet huuku ukowaza shida zako na familia Yako.
Humu tunaoBET Matren woote ukipasia vichwa vyetu kujua tunawaza nini unaweza kucheka mpaka ukazimia.
Muhim,usiwe mtumwa wa KAMARI
Sie wengine ni waajiriwa but pesa ya Familia usiiguse kabisa kwenye KAMARI,Laana ya kuadhirika familia yako haitakuacha salama Mdau,Amini hilo.
Mostly bet from other extra sources ambazo unazitengeneza,Mie out ajira nina banda la Chakula Nimetenga Mzigo Faida yake niBET tuu.Yaani unakuwa relaxed mnoo.
Ila kama Mshahara is less than 700,000 ukabetia,baba unajimaliza.Utakuwa unaomba advanced Salary kila mwezi.Unless uwe under 25 hapo kidogo but age goes up.
Pole Sana but try to change mzuka of betting..
Nakula siri iliyo dhahiri na ushuhuda:-
TunaoBET wengi wetu hatuna muda wa kukaa na kupanga Maisha na wenza wetu,hata kutamaniana ni kwa muda mfupi mnoo.We are very busy kufuatilia Mechi.
TunaoBET wengi hata Dem wako akichepuka basi wala huwazi,yaani wivu umetupotea mazimaaaa,maana Maisha ya kuchepuka ndio tumeozea huku kwenye Betting,ukiangalia Dem wangu Fc Porto nilimuambia na kachepuka,Kula Tanga Dem wangu Man City kachukuliwa na Bodaboda.
Sasa tupo so neutral
Hapa tu nakuambia kwa Mechi za leo,kuna Jamaa hapa mtaani anauza TV akiamini leo pesa Ipo.
Hapo ndio tumepofikia.Ukifuatilia akili inavyomtuma,ni kwamba leo mechi laini na atatoboa na atanunu zaidi ya ile.
Bodaboda asilimia 90 wameingia huku,na wengi wao mpira hawajui wanategemea mikeka ya kupeana wao kwa wao.Mfano wale wa CHANIKA- DAR mnanielewa maana huku ni Janga,kila siku matajiri wanachukua bodaboda zao mrejesho hakuna.
PESA ipo on Betting but tuBet kiuungwana na Tuliinde mnoo familia zetu na tutenge muda na Wake zetu hasa watoto wetu.Kipato cha Kula Familia yako usiingie kwenye Betting Laana ya aibu na kuadhirika familia yako haitakuacha salama.