KWA WAPAMBANAJI WOTE WA BETTING.
Ndugu zangu,ni siku kadhaa sasa tangu kufanyiwa marekebisho( kama si kuondolewa) kwa huduma ya kudepost pesa kwa njia ya simu kutoka kwa kampuni pwendwa katika Uzi huu ya 1xbet.com,
Kuna mashaka ama wasi wasi kwa kila mmoja wetu, hususani Mimi.
Kwa kawaida, popote pale unapokuta mzungu kawekeza na watu wanafanya kazi kila kuchapo, ujue mahala hapo, huduma zake in za uhakika kabisa kwa kigezo tu kuwa Mzungu amekaa pale.
Mzungu hawezi kusimamisha kazi kizembe tena kwa siku nyingi tu, wakati anajua dhahiri kwamba yupo kwaajiri ya kupiga pesa.
Vyovyote vile atahakikisha kwamba anapambana kurejesha huduma ndani ya masaa 24 na si zaidi ya hapo,kwani anajua ya kuwa akiendelea kupoteza muda na ndivyo anavyozidi kupoteza pesa ambapo jambo hilo halikubaliki hata kidogo.
Nimezungumza haya kwani ni zaidi ya siku tatu sasa, kampuni ya 1XBET, haina huduma ya malipo kwa njia ya simu ambapo hii huduma ni mashuhuri kwa walio wengi kutokana na urahisi wake katika masuala ya miamala.Hivyo kwa upande wa hapa Tanzania huduma hii inavyosemekana inafanyiwa ukarabati na wataalamu.
Swali, “hivi kweli wataalamu wanafanya maboresho gani mpaka yachukue siku zote hizi?”
“Au kuna jambo gani limeshinda ama limeshindikana kurejesha huduma hii ndani ama nje ya masaa 24?”
Siku kadhaa sasa watu hawabeti kupitia kampuni hii, ni dhahiri kwamba hata wao mapato yamepungua kutoka hapa Tanzania.
Hii inatokana na kwamba karibu 85% za makadirio ndio idadi kubwa ya watu wanaorumia huduma hii mbali na wale wanaorumia njia zingine za kibenk kama PayPal, Smart Cash, na huduma kama hizo.
Leo Uzi huu haueleweki watu hakuna jipya tena ni kimya kimya, nimepita jioni kucheki ni nani angalau kaandika, “ In play” chaajabu ni mtu mmoja tu ndo kafanya vile, nadhani hata yeye alikuwa na masalia katika account yake na pengine anamalizia tu ili sote tuwe sawa.
Watu tumekuwa kama wakiwa kwa huyu 1XBET alikuwa mkombozi wetu mkubwa, kutokana na uwanja wake wa masoko ya kubetia kuwa mpana na rahisi katika machaguzi na kupelekea watu kutandaza mikeka yao kwa kujinaafasi kabisa na uhakika wa kula ni mkubwa mno, kulingana na makampuni uchwara ya hapa Bongo.
Watu hawana hela tena, umasikini unanyatia kwa kasi kwani angalau kwa siku watu tulikuwa tunamnyatia bwana Putin na tunafanikiwa kuchukua vijisenti vyake.
Lengo maalumu la makala hii ni,
Kama tumeweza kubashiri timu A kufunga na kweli inaifunga timu B,
Ni dhahiri shahiri kwamba hata Mimi ninabashiri kwamba hii kampuni, huenda imenyanyua virago vyake hapa Tanzania kutokana na figisufigisu za wabongo wasiopenda Maendeleo.
Ndugu zangu wapambanaji wa Betting, Nchi yetu Tanzania,
Hivi karibuni imeingia katika sakata ama sekeseke la kusitishiwa mambo makubwa na muhimu na mataifa makubwa ki dola kama Marekani, Ulaya na Europe.
Mambo hayo ni kama misaada ya hisani, mikopo na uwekezaji.
Eidha, nchi yetu Tanzania, imekumbwa na tatizo la kibiashara hususani biashara za kimataifa,hali iliyopelekea baadhi ya nchi zimesusia kuja kufanya biashara hapa Tanzania, kwa kigezo cha ugumu wa biashara.
Baadhi ya nchi mpaka sasa zimesusa kuja kufanya biashara Tanzania.
Na makampuni makubwa yameanza kuondoka na biashara kubwa za mataifa niliyoyataja pale tayari zimeshadungwa.
Nchi yetu imetengwa na mataifa hayo.Kampuni hii ya 1XBET inatoka Ulaya katika nchi ya Urusi.
Sasa kutokana na matatizo haya,huenda wamefanyiwa figisu na mataifa hayo ili wasifanye biashara hapa Tanzania.
Kwahiyo kuna uwezekano mkubwa wa kubakia na programu tumishi tu katika simu zetu ama tarakilishi zetu tu na hakuna huduma ya kubeti tena.
Furaha kwa wale wanaotumia huduma za kibenki.
Lakini kama si shinikizo la mataifa hayo makubwa, basi huenda Serikali imewafigisu kwani wanatoa huduma zao kwa wateja wao pasina kukatwa kodi, jambo ambalo kwa Serikali ya sasa ni kama uhujumu uchumi na magendo.
Mimi na wewe hatujui kama kuna mazungumzo na Serikali ama wameshindwa masharti ya hapa Tanzania.
Huduma ikirejea basi fresh,lakini isiporejea tutambue kuwa kuna tatizo kubwa sana.
Ndugu zangu wapambanaji wa betting, hayo ni maoni yangu, ruksa kunikosoa ama kuchangia.
Ni Mimi mpambanaji wenzenu,
Kazetela
mnakugerald@gmail.com