Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sindano ya nyuki, njoo ufanye ufafanuzi kwa ndugu yangu Ommy50. Handcap ni ushindi wa aina gani? (+1) inapunguza ushindi kwa aliyepata ushindi?Ila hapa kwenye cap nataka darasa zaid inamana kushinda sio lazima iwe interval ya mbili au kutoa suluhu inatakiwa zilingane kwa interval ya magoli ya ngapi naomba maelezo kwa kina hapo na je zipo cap za aina ngapi
Fanya ufafanuzi wa halftime/fulltime, kwenye betting. Mfano unakuta 1/1, ×/1, 1/2, ×/2, 2/2 kwa kweli sielewi sana. Hapa ueleze ushindi kinamba mfano tena,
1- mwenyeji anaongoza mwanzo mwisho
2-
3-
4-
Naomba kufundishwa kucheza m.bet kwa voda *149*19# yaani mbinu na tahadhari ni..kwa kawaida sio handcupWatu wengi katika ulimwengu wa GAMBLING wanajikuta wakipoteza kiasi kikubwa cha pesa bila hata ya kujitambua.Ni kutokana na kutokujua au kutambua misingi kadhaa ya kushiriki katika Mchezo huu
LEO NAOMBA NIWAJULISHE WADAU WA MCHEZO JINSI AU NAMNA YA
KUSHIRIKI KIKAMILIFU NA KUFANIKIWA KUSHINDA KWA KIASI KIKUBWA.
KWA KUZINGATIA MAMBO HAYA #8 ,UTAWEZA KUFANIKIWA KUTENGENEZA FAIDA KUBWA KATIKA MCHEZO HUU.
#1 . UFANYE UWE MCHEZO,KISIWE CHANZO CHA MAPATO.
Watu wengi hufanya mchezo wa football betting kama ni kituo cha kujipatia mapato kwa ajili ya kukidhi haya mbalimbali za kimaisha kama vile
1.kulipa kodi ya nyumba,
2.Kupata ada ya watoto,
3.Kupata fedha ya kununua mali fulani i.e Pikipiki, Simu.
4. Kupata fedha ya kulipa Deni. ...na mengineyo!
Hili ni kosa kubwa sana. Unapofanya huu mchezo kama ni chanzo cha pesa kwa ajili ya suala fulani, linakupotezea nafasi ya kuweza kufanya machaguzi ya Odds
yaliyo sahihi.Watu wenye utaratibu huu ,huwa wanachagua Odds ambazo zitawaletea zao kubwa la pesa na kusahau kuwa si michezo yote katika orodha inayoweza kukupa tokeo chanya.
(Kumbuka, Mahesabu ya kina hufanywa na wenye hizi Betting Companies kuhakikisha hakuna mtu anaweza kupata kiasi kikubwa cha pesa kama matokeo ya betting(Mkeka) wake).
#2 . ZITAMBUE LIGI VIZURI.
Watu wengi hujihisisha katika huu mchezo hata bila ya kutambia mienendo (Trend) ya ligi kuu mbalimbali barani Ulaya.Kutokana na Betting Companies kuwa na aina mbali mbali za "kubet", Pia kuna baadhi ya ligi zina "facilatate successful betting" kutokana na aina ya betting.
Kwa mfano:- Ligi ya Uingereza(EPL) , inafaa sana kutumika katika kubeti katika category ya "NORMAL" kwa asilimia 80%.Hii ni kutokana na ligi kuwa na wababe wanaotabirika , Baadhi ya timu kuwa out-of-form kwa muda mrefu, Mjeruhi ya mara kwa mara.
Ligi ya Spain(LA LIGA), inafaa sana kutumika katika "NORMAL" kwa silimia 70% na "HANDCAP" kwa silimia 30%( timu za R.madrid,Barca,A.madrid)
Ligi ya Ufaransa(LIGUE 1).Kutokana na hii ligi kuto kuwa na wababe wa kueleweka , hapa ni mahali salama sana kuitumia "HANDCAP" 80% na.Pia ni ligi iliyo na idadi ndogo sana ya magoli hivyo basi "FOURTYFIVE" prediction inafaa.Hii ni kutokana na matokeo mengi ya ligi hii kuwa na tofauti ya goli moja.
Ligi kuu ya Itali (Serie A), hii ligi haina tofauti sana na ligi kuu ya Ufaransa.Baadhi ya mechi huwa na tofauti ya goli moja, na mara nyingi huwa na matokeo ya suluhu katika dakika 45 za kwanza. Hivyo "HANDCAP" ina asilimia 60% na "FOURTYFIVE" ina asilimia 40%.(Tahadhari: Hii ligi inahitaji uchambuzi wa kina katika mechi zake kabla ya kuweka bet,)
#3 . BOBEA KWENYE LIGI CHACHE TU.
Si mbaya sana ukichagua baadhi ya timu zenye nguvu kutoka ligi nyingine, bali umuhimu wa kubobea katika ligi chache ni veyma zaidi.Hii itakufanya uwe mwenye uelewa na utambuzi wa kutosha na mwenendo wa hizo ligi chache. Pia hii itakuwezesha kuweza kufanya maamuzi sahihi yaliyo na ufahamu na uelewa yakinifu.,
#4 . MARA NYINGI NI VYEMA KUFUATA HISIA.
Umeshawahi kutazama orodha ya michezo/mechi za siku husika kuanzia ya kwanza hadi ya mwisho, na katika akili yako kuna hisia/vochochezi ambavyo vina kuambia kwamba "huyu anashinda" au "huyu anafungwa" au "hii mechi suluhu"?
Basi kwa taarifa yako, hizo hisia-za-mwazo(PRESCIENCE) husadikika kuwa sahihi kwa asilimia 80%.
Hii ni kwa upande wa wale wanao-Bet katika category ya "NORMAL".
#5 . EPUKA USHABIKI.
Kuna nyakati ambazo inakuhitaji uchague mechi ambayo timu uipendayo inacheza.Hiki kimekuwa kipindi kigumu sana kwa watu wengi.Hupenda kuchagua timu zao kuwa zitashinda hata kama ukweli ni kwamba zinauwezekano mkubwa sana wa kupoteza mchezo.
Au kuwekea timu fulani ishindwe kwa mategemeo timu yake(anayoishabikia) iendelee kuongoza ligi.
Ukiona umejawa na hisia za ushabiki na huwezi shindana nazo, basi ni bora kuacha kabisa kuchagua mechi hizo.
#6 . FANYA UCHAMBUZI YAKINIFU.
Hili ni pamoja na kuzingatia aina ya mchezo unaocheza. Mfano
-NORMAL; katika hii category unashauriwa kuchagua mechi zenye timu dhaifu na imara.Hii inaleta uwezekano wa kutokea kwa matokeo yaliyo-tabiriwa.
-HANDCAP; hapa unashauriwa kuchagua mechi zenye timu ambazo zenye uwezo unaokaribia na kulingana,kwa kuwa timu moja hupewa goli la kufikirika ambayo mara nyingi huwa ni ile dhaifu basi ni vyema kuchagua matokeo ya Suluhu huku ukiamini kuwa ile timu yenye nguvu zaidi huenda ikashinda kwa tofauti isiyozidi goli 1.Yaani 2-1 au 1-0 au hata 3-2.
-FOURTYFIVE(45); hapa sasa ni mahala ambapo mechi za machaguo ya suluhu kuzingatiwa.Kutokana na mechi kuanza kwa suluhu ya bila kufungana,kuna uwezekano wa asilimia 80% ya hizo mechi kumaliza dakika 45 za kwanza bila kufungana ili uweze kuchagua suluhi ya dakika 45, inashauriwa kuchagua mechi ambazo zina upinzani mkubwa sana baina yao au mechi zenye timu zilizodhaifu sana.
#7 . JIWEKEE KIASI KATIKA KU-BET.
Huu mchezo unaathiri sana tabia-ya binadamu (Addictive).Kuna kipindi unasikia hamu ya kubet kila mara hata pale unapoona mkeka(Betting Form) umeharibika, ili tu uweze kurudisha kile kiasi cha pesa ulicholiwa.Hii hutokea kwa sababu ya kutojiwekea "kikomo".
Weka kikomo ,mfano Tsh 5000/= tu itumike ndani ya saa 72.Itakufanya uwe na kikomo katika mchezo na kukusaidia kutopoteza kiasi kikubwa cha pesa kutoka mfukoni mwako.
#8 . FUATILIA UTABIRI WA MITANDAONI.
Ni vyema kufuatilia utabili wa mitandaoni kwa sababu huwa na takwimu sinazoonyesha historia, Perfomance, na matarajio ya mechi husika.
Hakikisha una-zingatia mechi tano(5) zilizopita.
-Head-to-head ya timu hizo.
-Perfomance ya timu katika dakika 45 za kwanza
-Majeruhi walio n'je ya kikosi kikuu.
-Usajili waliofanya
-zingatia idadi ya magoli ambayo timu hizo zinafunga(score) na kufungwa(concede).
-zingatia idadi ya mechi ambazo timu imeshinda na kupoteza.
-zingatia msimamo/stance ya timu katika mechi za nyumbani na ugenini.
Kuna baadhi ya mitandao maarufu ambayo hutumika kutoa tabiri za mechi mbalimbali.
(1)windrawin.com
(2)predictZ.com
(3)soccervista.com na
(4)livescore.com tu kwa matokeo yaliyo "live" na ya mechi zilizopita.
Nakaribisha maswali na Maoni kwenye eneo lolote lisilo eleweka...!
DemiGod,
Top Handcapper in Tanzania
Naomba msaada eti kwenye primier betting Handicap odd
1(4) ina maana timu mwenyeji ishinde goli zaidi ya 1 yaani kuanzia magoli mawili kuendelea sindio?
2(5)ina maana timu mgeni ashinde pia goli zaidi ya 1 yaani kuanzia magoli mawili kuendelea
Na je X(6) ina maanisha nini??
Ushindi mdogo kwa timu zote mbili
wakuu bonas unaweza kuitoa kwel.
Hahahahaha mkuu utatoaje bonus
Kama upi??sjakupata vzuri mkuu/?