Mikese: Wanne wafariki ajali ya basi la Kibisa, 15 wajeruhiwa

Mikese: Wanne wafariki ajali ya basi la Kibisa, 15 wajeruhiwa

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Watu wanne wamefariki dunia na wengine 15 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Kibisa lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na gari la kubebea mizigo…ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika kata ya Mikese Manispaa ya Morogoro.

Kaimu Afisa Habari wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Scholastica Ndunga amadhibitisha kupokea miili ya watu wanne na majeruhi 15 na kwamba majeruhi hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospital hiyo.

#AzamTVUpdates
Habari | Theresia Mwanga
Mhariri | John Mbalamwezi
 
Watu wanne wamefarika dunia na wengine 15 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Kibisa lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na gari la kubebea mizigo…ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika kata ya Mikese Manispaa ya Morogoro.

Kaimu Afisa Habari wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Scholastica Ndunga amadhibitisha kupokea miili ya watu wanne na majeruhi 15 na kwamba majeruhi hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospital hiyo.

#AzamTVUpdates
Habari | Theresia Mwanga
Mhariri | John Mbalamwezi
N mapepo yanatuamdama ama uzembe wa manresa...
Sababu lazima itakuwa uzembe wa madereva na/au ubovu wa barabara.
Barabara zilizopo ni mbovu sana, Wala hazina ubora au viwango vinavyotakiwa. Barabara ni nyembamba Sana, Zina njia mbili tu za kupita magari (two lanes only), moja ya kwenda na nyingine ya kurudi ndio maana unaona ajali za magari kugongana uso kwa uso ni nyingi sana kupita kiasi.

Inatakiwa barabara Kuu (Trunk roads) angalau ziwe na 'lanes' nne, lanes mbili kwa kila upande, na lanes hizo zitenganishwe kwa kuweka tuta au 'concrete road blocks' katikati ya hizo lanes ili kuzitenganisha lanes za upande wa kulia na za upande wa kushoto. Hii itasaidia Sana katikà kudhibiti ajali za barabarani za magari kugongana uso kwa uso.
 
Back
Top Bottom