Mikindani Mtwara: Wafanyabiashara wadaiwa kukimbia soko lililojengwa kwa billion 5 kwa kukosa wateja

Mikindani Mtwara: Wafanyabiashara wadaiwa kukimbia soko lililojengwa kwa billion 5 kwa kukosa wateja

Wafanyabiashara hao wameamua kuondoka kutoka katika soko hilo kwa kukosa wateja hali iliyopelekea biashara kuwa ngumu.

Wafanyabiashara hao hawajui watalipa vipi madeni wanaodaiwa na taasisi mbalimbali za fedha.

Ikumbukwe soko hilo limejengwa na serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 5.
Pesa hizi ni za walipa kodi.
Serikali haijafanya uchunguzi wa eneo hili kama lina wateja wa kutosha.

Wasafi Radio.

View attachment 1962836
Watu wamepiga ndefu sana hapo
 
Shida badala watafute location katikati ya mji wawalipe watu wajenge huo mjengo wao wanatoka nje ya mji
 
Kweli Kaka Mshana...huu ni ufisadi mwingine, kwa nini serikali iko kimya? Bilioni 5 kwa soko gani? Au lina lifti?...Huu wizi...hiyo hela itarudi lini? Mkopo wa WB utarudushwa vipi?
 
Naunga mkono hoja yako mkuu Chris.Mfano mzuri soko jipya la Magomeni ,ingawa ni ghorofa zuri wateja wachache sana ukilinganish
a na soko la ndizi Mabibo.
Ni huzuni sana. Yaani wakati mwingine tuachwe tu tuishi bila mipangilio....yaani ni aibu
 
hapo bas zetu za kutokea mjin lazima zipite chuno zinazunguka ligula pale magomen mnada wa mbuz mbae ufukon mpaka mikindan.ila hata mim napendelea sana sabasaba kuliko hapo
sabasaba vitu nafuu la mjin bei ghal.karot moja 500
 
Dawa ni kuwaachia machinga masoko makubwa wafanyabiashara wakubwa waende kwenye masoko hayo ya serikali kwa bei nafuu kama ya wamachinga
Yaani iwe verse verses tuone tena machinga watakimbilia wapi
Kaaa maachingaaaa kama kupe yamganda ng'ombe ?
 
Wafanyabiashara hao wameamua kuondoka kutoka katika soko hilo kwa kukosa wateja hali iliyopelekea biashara kuwa ngumu.

Wafanyabiashara hao hawajui watalipa vipi madeni wanaodaiwa na taasisi mbalimbali za fedha.

Ikumbukwe soko hilo limejengwa na serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 5.
Pesa hizi ni za walipa kodi.
Serikali haijafanya uchunguzi wa eneo hili kama lina wateja wa kutosha.

Wasafi Radio.

View attachment 1962836
WHITE ELEPHANT
 
Ili masoko yote yafanye Kazi lazima watoeee wanaouza bidhaa barabarani popote pale ndo uhitaji utaongezeka na watu wataenda
 
Ndugu Chris mara nyingi bidhaa za wamachinga wanunuzi wake ni wapita njia au abiria,hivi inaingia akilini mtu upande ghorofani ukanunue pamba za kusafisha masikio au soksi pea moja?

Kwa kawaida hata mimi nanunua bidhaa kwa machinga pale ninapikutana nao barabarani au nikiwa kwenye stendi ya basi au foleni ya magari.

Maana vitu vingi tunavyonunua kwa machinga maamuzi tunafanya papo kwa papo na si kuwafata mae eo yao.Machinga anamfata mteja na sio mteja kumfata machinga.

Umeelezea uvivu in a very simple way!
 
Back
Top Bottom