Mikoa 13 Kinara wa Kuchangia Kodi ya TRA mwaka 2023

Mikoa 13 Kinara wa Kuchangia Kodi ya TRA mwaka 2023

Ni kwamba Mwanza watu wanakwepa kulipa kodi!! Au tatzo ni nn maana imezidiwa na vimikoa vya hovyo vingi hapo juu
Mkoa wa Hovyo ni Kagera na Ile top 10 ya Maskini wenzake 🤣🤣

Jibu ni kwamba Mwanza hakuna entry/exit points kama border posts au uwanja wa Kimataifa ambazo zinaingiza pesa nyingi.

Lakini pia ni kuzidiwa tuu na Kasi ya uwekezaji eg Dodoma haina boda ila imeizidi Mwanza.
 
Kutoka kwenye takwimu za Mapato ya Kodi za TRA yaani Regional Tax Statistics za mwaka 2023/2024 zimebainisha Mikoa 13 ambayo imechangia Mapato makubwa ya Kodi Kwa mwaka 2023.

Uchambuzi wa awali nilioufanya umebainisha Mikoa 13 ambayo imechangia zaidi Mapato ya Kodi ya kuanzia Bilioni 60 na zaidi.

Orodha hiyo Kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 inasomeka kama ifuatavyo;(Figures are in "000" Million Tanzania Shillings).

1. Dar es Salaam =7,416.95
2. Arusha =356.28
3. Kilimanjaro =234.88
4. Tanga =203.28
5. Songwe = 176.81
6. Dodoma =163.17
7. Mwanza =160.66
8. Mara =143.13
9. Kagera =118.94
10. Mtwara =116.44
11. Mbeya =85.10
12. Morogoro =67.60
13. Pwani =60.60

View attachment 3063007

My Take
1.Vyanzo vya Kodi kama Utalii, Property Tax,OPMU,MTD na Large Tax Payers Sio sehemu ya takwimu za Mikoa Kwa sababu ni Kodi ya Jumla ambayo Haina mchanganuo wa Mkoa ilikokusanywa.

2.Figurrs za Mkoa wa Dar es Salaam zimehusisha Mikoa ya kikodi iliyoko Dar ambayo ni Ilala,Kinondoni,Temeke,Tegeta,Kariakoo,DSM Service Centre na JNIA.

✓Credits;TRA Regional Tax Statistics 2023/2024.

Observation
•Mapato ya Kodi Kwa Mikoa Mingi mwaka ulioisha wa 2023/2024 Yalishuka sana ukilinganisha na Mwaka 2022/2023. Huenda Mvua za El Nino zilichangia Hali hiyo na sababu zingine.Utalii na Makaa ya Mawe viliokoa jahazi.

•Mkoa wa Mtwara umefanya vizuri Sana kwenye Mapato Kwa sababu ya Bandari ya Maboresho ya Bandari ya Mtwara ,amri ya Rais kusafirisha korosho Kupitia mtwara na Kusafirisha shehena kubwa kabisa ya Makaa ya Mawe kutoka Ruvuma na Njombe.

•Mwanza inazidi kupotea kwenye Ramani ya Uchumi wa Tanzania huku nafasi yake ikichukuliwa na Mikoa mingine.Mlioko Mwanza Jiji lenu limekumbwa na nini Hadi shughuli za Uchumi zinazorota?

Mwisho.
•Pamoja kwmaba TRA ndio taasisi mama ya kukusanya Mapato ila Tanzania Ina taasisi nyingi sana zinazokusanya Mapato ya Serikali,hivyo mchango wa Mkoa kwenye Uchumi wa Nchi unapimwa sawaia Kupitia GDP.

Pia soma Mikoa 15 Inayoongoza Kuchangia Kodi za TRA Tanzania

Angalizo
•Uchambuzi huu sio rasmi hivyo uchukuliwe Kwa muktadha huo.Taasisi Zenye mamlaka husika ndio zitafanya Uchambuzi wake wa kina kama zikiona inafaa.
Tabora na ukubwa wa mkoa bado ni poor😁😁😁😁
 
Mkuu kumbka Arusha ni kinara wa utalii
Kinara wa utalii, huo utalii unawasaidia nini kuinua uchumi wenu, wazungu wanakuja arusha kushangaa masai wenye mashuka na pumbuz zikiwa wazi mnajiona wajanja, GDP ndio uchumi.
 
Arusha kwa miaka mingi imekua ikichangia mno pato la Taifa lakini huduma muhimu hawapewi.

Stendi ya mkoa tu ya maana hakuna.

Barabara za lami chache, maeneo mengi ni vumbi tu.

Wamasai ni kunyanyaswa tu kwa kufukuzwa makazi yao ya asili.
Maendeleo sasahv ni Zenji na Pwani kwanza

Nyie wa Kaskazini mlishajiendeleza wenyewe
 
Hizi takwimu zimepikwa tu hawa kilimanjaro wana nini cha ziada ukitoa huo mlima ?? Hao Tanga wana maajabu gani kwanza nyumba zao zimechoka hivyo
 
Acha kujitafutia presha yaani ka Arusha unataka kapambane na jiji lenye mandevu kama Mwanza utachekesha marehemu.
Mkuu Takwimu ndio inasema sio mimi sio unaona mapato hata nusu ya Arusha hamfiki labda ng'ombe ndio mtuzidi
 
Nyie na Kagera tofauti yenu ni ndogo sana ,wote mnategemea Mapato kwenye import/export points ambazo ni Border posts na Viwanja vya ndege nothing else
Acha kupotosha wewe hayo ni Matusi kufananisha kichwa na kalio
 
Kinara wa utalii, huo utalii unawasaidia nini kuinua uchumi wenu, wazungu wanakuja arusha kushangaa masai wenye mashuka na pumbuz zikiwa wazi mnajiona wajanja, GDP ndio uchumi.
DU- ulizaliwa au ulitolewa tumboni kwa mama yako?
 
Mkuu Takwimu ndio inasema sio mimi sio unaona mapato hata nusu ya Arusha hamfiki labda ng'ombe ndio mtuzidi
Mnafurahia kodi ndogo kama hiyo na nyie ndio mnashikilia utalii wa nchi, ina maanisha utalii umeshuka sana kutoka kukusanya 500B adi 300B ina maanisha sekta ya utalii imeporomoka sana, mapato ya ngorongoro tu ni zaidi ya 250B bado serengeti mlitakiwa mkusanye kuanzia 1T, nyie ni underdog tu kwa Mwanza ambayo mapato yote yanatokana na wananchi wenyewe wala sio pesa za watalii wa kizungu.
 
Back
Top Bottom