Mikoa hii haina vyuo vikuu kabisa wala mpango wa kuvijenga. Serikali iwajibike kuisaidia haraka

Mikoa hii haina vyuo vikuu kabisa wala mpango wa kuvijenga. Serikali iwajibike kuisaidia haraka

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
933
Reaction score
3,051
MUHIMU: Ni Kwa vyuo vya kodi zetu / vya serikali, level ya vyuo / taasisi zinazotoa degree, Open University kipo kila mkoa lakini ni maalum zaidi kwajili ya waajiriwa, hawaingii madarasani wanajisomea kivyao, wanaenda kufanya mitihani tu.

Kuna mikoa ni kama imesahaulika kabisa kwenye miradi ya kielimu, Mikoa mipya tunaweza kuelewa lakini kuna mikoa kongwe mpaka leo haina vyuo, NI AIBU !!!

  • MARA - Kuna chuo kilianzishwa 2010 kumuenzi Nyerere kijijini Butiama lakini, kila mwaka story ni ile ile "ujenzi unaendelea"
  • RUVUMA
  • PWANI - Kipo chuo Bahamoyo ila sio cha serikali, ni chuo cha kanisa katoliki tawi dogo la Saut, pia kuna shule ya uongozi watu wengi judhani ni chuo ila hawatoi diploma wala degree.
  • MANYARA - Kuna IAA lakini hawajafika level za kutoa degree
  • SONGWE
Mikoa hii haina vyuo ila vinajengwa
Panapo majaliwa vinaweza malizika visiishie kuwa story
  • KAGERA - Kuna tawi la UDSM linajengwa
  • LINDI - Matawi mawili ya UDSM yanajengwa
  • NJOMBE - Kuna Tawi la UDOM linajengwa
mikoa hii mnaweza kudhani hakuna vyuo ngazi ya degree ila vipo
  • KATAVI - Kuna tawi la SUA
  • RUKWA - Kuna tawi la MUST
  • KIGOMA - Kuna tawi la TIA
  • SINGIDA - Kuna tawi la TIA
  • SIMIYU - Kuna tawi la IFM
USHAURI:

Ni aibu makao makuu ya baadhi ya mikoa kukosa hata chuo kimoja, hali inayowalazimu watu kusafiri kwenda mikoa mingine kutafuta elimu ya juu. Vyuo vilivyopo vinapaswa kuondoa hali hii kwa kufungua matawi kwenye mikoa isiyo na vyuo. Mfano TIA wameonesha mfano mzuri kwa kufungua matawi mikoa ambayo haikuwahi kuwa na vyuo, ni zamu ya vyuo vingine sasa. napendekeza kuona matawi kama DIT Manyara, Mzumbe Mara, UDOM Geita, IFM Songwe, na UDSM Pwani. Pia mpaka leo haiingii akilini jiji la pili nchini tangu zamani Mwanza hakuna chuo kikuu, hii sio sawa kabisa serikali inabidi ijenge chuo kikuu huko. Serikali isimamishe kwanza mipango ya kujenga vyuo mikoa ambayo tayari imejitosheleza, waweke kipaumbele mikoa isiyo na vyuo ama kuna vyuo vichache, Lengo ni kujaribu kupata usawa kielimu kitaifa, mikoa yote Tanzania inayolipa kodi ina haki ya huduma hii muhimu ya kijamii.

Kujaza vyuo baadhi ya mikoa inaweza pia kuwa ni mbegu ya kustawisha ukabila na ukanda, vyuo vinatoa output ya wahitimu wenye sifa za kuajiriwa kwenye system, balance isipokuwepo kunakuwa na hatari ya kuruhusu makundi flani yajae kwa kiasi kikubwa kwenye system.

Hizi ni faida za mkoa kuwa na chuo.
  • Gharama za kusoma vyuo zinaweza kupunguzwa, wanafunzi wenye uchumi mdogo wanaweza kula au / na kuishi nyumbani kwao, pia hawaingii gharama za usafiri.
  • Chuo ni huduma muhimu ya kijamii, Kila mkoa unaochangia kodi una haki ya kupata huduma hii.
  • Makundi maalum na watu wasiojiweza inakuwa rahisi kupata elimu kwa usimamizi wa karibu na mazingira waliyozoea.
  • Vyuo vinaleta fursa kwa vijana kupata ajira, ni kweli ajira ni chache lakini zipo na inabidi zijazwe mfano wanasheria, walimu, wahandisi, HR, n.k.
  • Vyuo vinachochea uchumi mfano vyumba vya kupanga, migahawa, mitumba, mabanda ya mpira, n.k.
  • serikali husukumwa kuboresha barabara, umeme, maji, na huduma za afya karibu na vyuo.

PDF - ORODHA YA VYUO VINAVYOTOA DEGREE
 

Attachments

Huna unalolijua kwenye mambo ya elimu.
Mara kuna chuo kikuu cha kilimo cha mwalimu nyerere.
Ficha ujinga wako
Hicho chuo hakina wanafunzi miaka 13, kilijengwa kisiasa sana kupelekwa Butiama kijijini kwa Nyerere.

Ni bora zaidi wangejenga tawi la Mzumbe, TIA, DIT, n.k. pale Musoma mjini makao makuu ya mkoa wa Mara.
 
Kwa level ya vyuo vinavyotoa degree, mikoa hii haina vyuo.

1. MANYARA
2. MARA
3. LINDI
3. KATAVI
4. RUVUMA

KAGERA - Kuna tawi la UDSM linajengwa

NJOMBE - Kuna Tawi la UDOM linajengwa

RUKWA - Kuna Tawi la chuo cha MUST

SIMIYU, KIGOMA, SINGIDA, - Kuna tawi la chuo cha TIA
Kiufupi mleta mada IQ yako ipo chini sana.
 
MUHIMU: Ni Kwa level ya vyuo vinavyotoa degree

1. MANYARA (Kuna IAA lakini wanatoa Diploma sio degree)
2. MARA (Chuo cha Butiama miaka nenda rudi hakina wanafunzi)
3. LINDI
3. KATAVI
4. RUVUMA

KAGERA - Kuna tawi la UDSM linajengwa

NJOMBE - Kuna Tawi la UDOM linajengwa

RUKWA - Kuna Tawi la chuo cha MUST

SIMIYU, KIGOMA, SINGIDA, - Kuna tawi la chuo cha TIA
Simiyu hakuna tawi la TIA Bali Kuna tawi la IFM eneo la Sapiwi
 
Kwa level ya vyuo vinavyotoa degree, mikoa hii haina vyuo.

1. MANYARA
2. MARA
3. LINDI
3. KATAVI
4. RUVUMA

KAGERA - Kuna tawi la UDSM linajengwa

NJOMBE - Kuna Tawi la UDOM linajengwa

RUKWA - Kuna Tawi la chuo cha MUST

SIMIYU, KIGOMA, SINGIDA, - Kuna tawi la chuo cha TIA
Katavi kuna Mizengo Pinda University College of Agriculture, tawi la SUA.
Lindi kuna agricultural campus ya UDSM (Coastal Agriculture and Food Technology (CoAF) initiative in Lindi Municipal), nasikia ipo na campus nyingine tena inajengwa Lindi na watu wanalalamika inakuwaje campus 2 za USDM zinajengwa hapo? Majaliwa kafanya yake pale. Manyara kuna initiative za kupeleka Nelson Mandela University Campus. Huko Mara kuna vitu kama vile;
  • Clinical Officers Training Centre Musoma
  • Imani College of Health and Allied Sciences
  • Shirati College of Health Sciences
  • Mara Zone Training College
  • Tarime College of Health Sciences
 
Katavi kuna Mizengo Pinda University College of Agriculture, tawi la SUA.
Lindi kuna agricultural campus ya UDSM (Coastal Agriculture and Food Technology (CoAF) initiative in Lindi Municipal), nasikia ipo na campus nyingine tena inajengwa Lindi na watu wanalalamika inakuwaje campus 2 za USDM zinajengwa hapo? Majaliwa kafanya yake pale. Manyara kuna initiative za kupeleka Nelson Mandela University Campus. Huko Mara kuna vitu kama vile;
  • Clinical Officers Training Centre Musoma
  • Imani College of Health and Allied Sciences
  • Shirati College of Health Sciences
  • Mara Zone Training College
  • Tarime College of Health Sciences
Nimepitia TCU Guidebook hicho chuo cha Katavi kipo ila wanatoa degree moja tu ya ufugaji wa nyuki, ila wana nafuu kuliko mikoa mingine isiyo na chochote.

Lindi ni kweli matawi ya udsm yanajengwa, mcheza kwao hutuzwa, Majaliwa kafanya yake.

Mara hivyo vyuo vyote ulivyotaja ni DIPLOMA, hakuna hata kimoja chenye DEGREE
 
Huna unalolijua kwenye mambo ya elimu.
Mara kuna chuo kikuu cha kilimo cha mwalimu nyerere.
Huko SIMIYU ni tawi la ifm sio TIA.
Ficha ujinga wako
Simiyu nimekosea kuna IFM

Mara hakuna chuo chochote kinachodahili wanafunzi degree, nimeweka pdf ya udahili wa vyuo vyote Tanzania
 
Back
Top Bottom