Mikoa hii haina vyuo vikuu kabisa wala mpango wa kuvijenga. Serikali iwajibike kuisaidia haraka

Mikoa hii haina vyuo vikuu kabisa wala mpango wa kuvijenga. Serikali iwajibike kuisaidia haraka

MUHIMU: Ni Kwa level ya vyuo vinavyotoa degree, Open University kipo kila mkoa na wanatoa degree lakini ni maalum zaidi kwajili ya waajiriwa, hawaingii madarasani wanajisomea kivyao, huwa wanaenda kufanya mitihani tu.

Kuna mikoa ni kama imesahaulika kabisa kwenye miradi ya kielimu, Mikoa mipya tunaweza kuelewa lakini kuna mikoa kongwe mpaka leo haina vyuo, NI AIBU !!!

  • MARA (Kuna chuo kilianzishwa 2010 kumuenzi Nyerere kijijini Butiama lakini hadi leo hakijakamilika)
  • RUVUMA
  • PWANI (Kuna shule ya uongozi wa siasa, kile sio chuo )
  • MANYARA (Kuna IAA lakini hawajafika level za kutoa degree)
  • SONGWE
Mikoa hii haina vyuo ila vinajengwa
Panapo majaliwa vinaweza malizika visiishie kuwa story
  • KAGERA - Kuna tawi la UDSM linajengwa
  • LINDI - Matawi mawili ya UDSM yanajengwa
  • NJOMBE - Kuna Tawi la UDOM linajengwa
mikoa hii mnaweza kudhani hakuna vyuo ngazi ya degree ila vipo
  • KATAVI - Kuna tawi la SUA
  • RUKWA - Kuna tawi la MUST
  • KIGOMA - Kuna tawi la TIA
  • SINGIDA - Kuna tawi la TIA
  • SIMIYU - Kuna tawi la IFM
USHAURI:

Ni aibu makao makuu ya baadhi ya mikoa kukosa hata chuo kimoja, hali inayowalazimu watu kusafiri kwenda mikoa mingine kutafuta elimu ya juu. Vyuo vilivyopo vinapaswa kuondoa hali hii kwa kufungua matawi kwenye mikoa isiyo na vyuo. Mfano TIA wameonesha mfano mzuri kwa kufungua matawi mikoa ambayo haikuwahi kuwa na vyuo, ni zamu ya vyuo vingine sasa. napendekeza kuona matawi kama DIT Manyara, Mzumbe Mara, UDOM Geita, IFM Songwe, na UDSM Pwani. Serikali isimamishe kwanza mipango ya kujenga vyuo mikoa ambayo tayari imejitosheleza, waweke kipaumbele mikoa isiyo na vyuo ama kuna vyuo vichache, Lengo ni kujaribu kupata usawa kielimu kitaifa, mikoa yote Tanzania inayolipa kodi ina haki ya huduma hii muhimu ya kijamii.

Kujaza vyuo baadhi ya mikoa inaweza pia kuwa ni mbegu ya kustawisha ukabila na ukanda, vyuo vinatoa output ya wahitimu wenye sifa za kuajiriwa kwenye system, balance isipokuwepo kunakuwa na hatari ya kuruhusu makundi flani yajae kwa kiasi kikubwa kwenye system.

PDF - ORODHA YA VYUO VINAVYOTOA DEGREE
Tempe mama mitano haya yanawezekana kabisa.
 
Stella Maris Mtwara university, unataka kusema hiki ni cha kiswahili??? Cha upigaji?
Hicho ni chuo cha kanisa katoliki tawi la SAUT, vyuo vya kanisa katoliki vinajitahidi huwezi linganisha na St Joseph, Teku, Kampala, n.k.

Naomba sasa turudi kwenye swali

NI CHUO GANI HICHO CHA MTWARA CHA DEGREE UNACHOSEMA WALILALAMIKA KUKOSA WANAFUNZI ?
 
Singida kuna tawi la TIA na chuo cha ushirika moshi, ni matawi ya muda mrefu sana kabla ya vyuo hivyo havijapandishwa hadhi.
 
Hicho ni chuo cha kanisa katoliki tawi la SAUT, vyuo vya kanisa katoliki vinajitahidi huwezi linganisha na St Joseph, Teku, Kampala, n.k.

Naomba sasa turudi kwenye swali

NI CHUO GANI HICHO CHA MTWARA CHA DEGREE UNACHOSEMA WALILALAMIKA KUKOSA WANAFUNZI ?
Ndio hicho nilichokitaja
 
Ndio hicho nilichokitaja
Stella Maris hii hapa

Nafasi 1000 za ualimu wa masomo ya arts,

Tatizo hii kozi imechuja sana, wahitimu wengi tangu 2016 karibia 90 % wapo kitaa

Hizo kozi nyingine hali ni mbaya zaidi labda ujiajiri

1746898240113.png

Graduation

View: https://www.youtube.com/watch?v=aUmyjfnz48I
 
Mkoa una watu wengi wenye sifa za kujiunga na vyuo wanaenda kwengine kwanini ?

Kozi inayodahili wanafunzi wengi ni Ualimu wa Arts - Nafasi 1000

Hii kozi imekuwa kama dampo, wahitimu wa uaalimu wa Arts toka 2016, 2017, 2018, 2019, 2020, 2021, 2022, 2023, 2024 hadi sasa zaidi ya 95% wapo kitaa, nani aende humo akiwa timamu ?

Solution waanzishe kozi zenye demand kama ualimu masomo ya hisabati, sayansi, biashara, n.k. watu hawapo tayari kurundika kozi ambayo tangu 2016 imejaza nyomi ya wahitimu wapo kitaa.

Lakini pia hicho ni chuo cha kanisa katoliki, imani za watu wa huko inaweza kuchangia baadhi yao kukikwepa.

Mkoa una watu wengi wenye sifa za kujiunga na vyuo wanaenda kwengine kwanini ?

Chuo kinatoa nafasi nyingi kwenye kozi moja tu ya Ualimu tena ni wa masomo ya arts tu nadhani unajua watu wanavyoikimbia, Waalimu wa Arts toka 2016, 2017, 2018, 2019, 2020, 2021, 2022, 2023 zaidi ya 95% wapo kitaa, kozi nyingine arts in Socialogy na Philosophy zina demand ya chini zaidi ni ngumu sana kupata ajira.

Solution waanzishe kozi zenye demand kama ualimu masomo ya hisabati, sayansi, biashara, n.k. watu hawapo tayari kurundika kozi ambayo tangu 2016 imejaza nyomi ya wahitimu wapo kitaa.

Lakini pia imani za watu wa huko zitakuwa zinakinzana na imani ya chuo, watu wengi wa huko ni waislam yafaa zaidi kuwekwa chuo cha kawaida cha serikali
Nikikuita yale majina unasema matusi, umeshindwa kusoma hata guidebook kabla ya kuja hapa.
Huna hoja kilaza kalale tu, hizo kada ulizotaja wanatoa.
 
Nikikuita yale majina unasema matusi, umeshindwa kusoma hata guidebook kabla ya kuja hapa.
Huna hoja kilaza kalale tu, hizo kada ulizotaja wanatoa.

Tatizo lipo kwenye kozi,

Sharbel upo tayari kumpeleka mtoto wako asome Degree ya ualimu wa masomo ya arts ? 😂

Yani tangu 2016 kuna nyomi linajikusanya tu,

Hao Stela Marias wabadilike hatupo tena enzi za Kikwete
 
Sharbel upo tayari kumpeleka mtoto wako asome Degree ya ualimu wa masomo ya arts ? 😂

Yani tangu 2016 kuna nyomi linajikusanya tu,

Hao Stela Marias wabadilike hatupo tena enzi za Kikwete
Akili huna Stella Maris wanatoa Science, law, business, economics na bado wamekosa watu.
 
Tatizo lipo kwenye kozi,

Kozi si zipo nyingi tu
 
Bachelor or Arts in Music
Bachelor of Philosiohy
Bachelor of Insurance
Bachelor of arts in socialogy
Bachelor of arts in Education

Ndizo kozi zinazojaza hapo nani aende huko sasa

Kozi muhimu kama Law, Doctor, Computer Engineering, huwezi kuta nafasi zaidi ya 3000 kwa kila kozi vyuo vyote nchi nzima

Nenda pale Stella Marius watu wamejazana kozi za maana kidogo kama law na ualimu wa sayansi tatizo nafasi chache, nafasi nyingi kwenye kozi hizo za arts watu hawataki kumwagwa kwenye hayo madampo
 
Umeanzaaa!!!! yani unageuka geuka tu hoja huna, ulianza vyuo havitoshi umekimbia unakuja mara vya Serikali umekimbia sasa ohhh wanatoa arts umekimbia ohhh wengi ni education, nenda kalale tu.
 
Back
Top Bottom