Mikoa hii haina vyuo vikuu kabisa wala mpango wa kuvijenga. Serikali iwajibike kuisaidia haraka

MUHIMU: Ni Kwa level ya vyuo vinavyotoa degree, Open University kipo kila mkoa na wanatoa degree lakini ni maalum zaidi kwajili ya waajiriwa, hawaingii madarasani wanajisomea kivyao, huwa wanaenda kufanya mitihani tu.

Kuna mikoa ni kama imesahaulika kabisa kwenye miradi ya kielimu, Mikoa mipya tunaweza kuelewa lakini kuna mikoa kongwe mpaka leo haina vyuo, NI AIBU !!!

  • MARA (Kuna chuo kilianzishwa 2010 kumuenzi Nyerere kijijini Butiama lakini hadi leo hakijakamilika)
  • RUVUMA
  • PWANI (Kuna shule ya uongozi wa siasa, kile sio chuo )
  • MANYARA (Kuna IAA lakini hawajafika level za kutoa degree)
  • SONGWE
Mikoa hii haina vyuo ila vinajengwa
  • KAGERA - Kuna tawi la UDSM linajengwa
  • LINDI - Matawi mawili ya UDSM yanajengwa
  • NJOMBE - Kuna Tawi la UDOM linajengwa
mikoa hii mnaweza kudhani hakuna vyuo ngazi ya degree ila vipo
  • KATAVI - Kuna tawi la SUA
  • RUKWA - Kuna tawi la MUST
  • KIGOMA - Kuna tawi la TIA
  • SINGIDA - Kuna tawi la TIA
  • SIMIYU - Kuna tawi la IFM
USHAURI:

Ni aibu makao makuu ya baadhi ya mikoa kukosa hata chuo kimoja, hali inayowalazimu watu kusafiri kwenda mikoa mingine kutafuta elimu ya juu. Vyuo vilivyopo vinapaswa kuondoa hali hii kwa kufungua matawi kwenye mikoa isiyo na vyuo. Mfano TIA wameonesha mfano mzuri kwa kufungua matawi mikoa ambayo haikuwahi kuwa na vyuo, ni zamu ya vyuo vingine sasa. napendekeza kuona matawi kama DIT Manyara, Mzumbe Mara, UDOM Geita, IFM Songwe, na UDSM Pwani. Serikali isimamishe kwanza mipango ya kujenga vyuo mikoa ambayo tayari imejitosheleza, waweke kipaumbele mikoa isiyo na vyuo ama kuna vyuo vichache, Lengo ni kujaribu kupata usawa kielimu kitaifa, mikoa yote Tanzania inayolipa kodi ina haki ya huduma hii muhimu ya kijamii.

Kujaza vyuo baadhi ya mikoa inaweza pia kuwa ni mbegu ya kustawisha ukabila na ukanda, vyuo vinatoa output ya wahitimu wenye sifa za kuajiriwa kwenye system, balance isipokuwepo kunakuwa na hatari ya kuruhusu makundi flani yajae kwa kiasi kikubwa kwenye system.

PDF - ORODHA YA VYUO VINAVYOTOA DEGREE
Wakati unaandika hivi inabidi ujiulize...

Je mahitaji ya vyuo vikuu nchini ni kiasi gani?

Vilivyopo vimeelemewa?

Mikoa hiyo inazalisha wanafunzi kiasi gani kuingia chuo kikuu?

Je unengaji holela wa vyuo ndio ongezeko la elimu? Au mnataka kuua ubora wa vyuo kama ilivyo elimu ya msingi na o level?

Ujenge chuo kila mkoa wafundishaji wapo? Au unafikiri chuo ni majengo tu?
 
👍
 
Kuna watu walikuwa na mawazo kama yako wakidhani vyuo vikijengwa Singida, Kigoma, Mtwara, Sumbawanga, n.k. havitapata wanafunzi, hivyo vyuo vimejengwa vimejaa na bado watu wanajitaji vya ziada.

Nakupa taarifa kwamba uhitaji wa vyuo ni mkubwa sana, kama unabisha fuatilia vyuo vya Dsm, Arusha, Mwanza, Mbeya, n.k. watu wanatoka mbali sana kwenda kusoma kwasababu kwao hakuna vyuo,

kama mkoa wako kulikuwa na vyuo na ukawa na option utachukulia poa sana lakini hali ni tofauti.

Pia elimu ni huduma ya kijamii, ni jambo la kulitimiza bila kujali profitability bali kuongeza accesibility kwenye jamii
 
Kuna watu walikuwa na mawazo kama yako wakidhani vyuo vikijengwa Singida, Kigoma, Mtwara, Sumbawanga, n.k. havitapata wanafunzi, hivyo vyuo vimejengwa vimejaa na bado watu wanajitaji vya ziada.

Nakupa taarifa kwamba uhitaji wa vyuo ni mkubwa sana, kama unabisha fuatilia vyuo vya Dsm, Arusha, Mwanza, Mbeya, n.k. watu wanatoka mbali sana kwenda kusoma kwasababu kwao hakuna vyuo,
Twende kwa namba mkuu tusiongee maneno tupu.

Nipe idadi ya wanafunzi wanaohitaji vyuo vs uwezo wa vyuo vya sasa.....

Mfano 2024 hali ilikuaje?
 
wahitimu wengi wanaomaliza diploma pamoja na wanafunzi wengi sana waliomaliza form 6 Necta wana sifa za kwenda vyuoni lakini wanakosa vyuo vya kwenda degree.

Kuna wanafunzi mpaka wanabadilisha kozi za kusoma kwasababu kozi walizochagua vyuo vimejaa

Kuna watu hawawezi kwenda kusoma vyuo mikoani kwasababu ni walemavu, hawawezi kulipia gharama za hostel na chakula inafaa zaidi wasomee wakiwa nyumbani, n.k.

Ndio maana inaitwa huduma ya kijamii, its way beyond even profitability, Ni kusaidia watu wapate accesibility kirahisi
 
Kwahiyo suluhisho ni Serikali kuongeza wanufaika wa mikopo, pia waboreshe miundombinu kwa ajili ya walemavu.
 
Huyo mwehu tu huko Mtwara TEC walilalamikia chuo kukosa wanafunzi
Huwezi kuongea kama mtu ulieelimika in a civilized manner bila kutukana ?

Ni chuo gani hicho mtwara walilalamika kukosa wanafunzi wa degree ?

Mtwara kuna chuo cha TIA hawajawahi kulalamika kukosa wanafunzi.

Halafu kitu kingine vyuo vya serikali ndivyo vina demand kubwa, hivi vyuo vya private vingine vimejaa uswahili na upigaji ndio maana watu hawaendi, vingi sana vilifungiwa na Ndalichako
 
wahitimu wengi wanaomaliza diploma pamoja na wanafunzi wengi sana waliomaliza form 6 Necta wana sifa za kwenda vyuoni lakini wanakosa vyuo vya kwenda degree.

Kuna wanafunzi mpaka wanabadilisha kozi za kusoma kwasababu kozi walizochagua vyuo vimejaa

Kuna watu hawawezi kwenda kusoma vyuo mikoani kwasababu ni walemavu, hawawezi kulipia gharama za hostel na chakula inafaa zaidi wasomee wakiwa nyumbani, n.k.

Ndio maana inaitwa huduma ya kijamii, its way beyond even profitability, Ni kusaidia watu wapate accesibility kirahisi
Mkuu nimekuomba namba umekimbia.

Kwa mwaka 2024 idadi ya wanafunzi waliopata ufaulu kidato cha 6 ni 102,000. Sawa na asilimia 96 na zaidi.

Uwezo wa vyuo ni kudahili wanafunzi 180,000/= na zaidi.

Kuna kozi zaidi ya 800 zinatolewa Tanzania.

Sasa ukichukua idadi ya Diploma na wanaojiendeleza hawafiki 50k wanaoingia chuo kila mwaka.

Hii ni upande wa udahili.

Tuje kwenye wahadhiri. Tunao wangapi? Kutoshea kila chuo kwa kila mkoa?

Anyway it is a good idea kuwa na chuo kila mkoa.

Ila tuangalie tusije zalisha wasomi mbumbumbu kama tunavyozalisha wanafunzi mbumbumbu wasiojua kusoma darasa la 7.
 
Huwezi kuongea kama mtu ulieelimika in a civilized manner bila kutukana ?

Ni chuo gani hicho mtwara walilalamika kukosa wanafunzi wa degree ?

Mtwara kuna chuo cha TIA hawajawahi kulalamika kukosa wanafunzi.

Halafu kitu kingine vyuo vya serikali ndivyo vina demand kubwa, hivi vyuo vya private vingine vimejaa uswahili na upigaji ndio maana watu hawaendi, vingi sana vilifungiwa na Ndalichako
Kwa hiyo mkuu ishu tena sio idadi ya vyuO tu? Ni idadi ya vyuo vya serikali?
 
Kile ni diploma, cha degree bado kinajengwa fuatilieni vizuri
Vyuo vya TIA vinavyotoa degree na kudahili wanafunzi wa degree

1746896239947.png
 
Huwezi kuongea kama mtu ulieelimika in a civilized manner bila kutukana ?

Ni chuo gani hicho mtwara walilalamika kukosa wanafunzi wa degree ?

Mtwara kuna chuo cha TIA hawajawahi kulalamika kukosa wanafunzi.

Halafu kitu kingine vyuo vya serikali ndivyo vina demand kubwa, hivi vyuo vya private vingine vimejaa uswahili na upigaji ndio maana watu hawaendi, vingi sana vilifungiwa na Ndalichako
Stella Maris Mtwara university, unataka kusema hiki ni cha kiswahili??? Cha upigaji?
 
Hicho chuo hakina wanafunzi miaka 13, kilijengwa kisiasa sana kupelekwa Butiama kijijini kwa Nyerere.

Ni bora zaidi wangejenga tawi la Mzumbe, TIA, DIT, n.k. pale Musoma mjini makao makuu ya mkoa wa Mara.
Walifanya kosa la kiufundi kabisa. Ifikie mahali waache kufanya mambo kisa kiongoz fulani, wafanye maamuzi logicaly
 
Kwa hiyo mkuu ishu tena sio idadi ya vyuO tu? Ni idadi ya vyuo vya serikali?
Naomba unijibu swali nililokuuliza hapo awali

Ni chuo gani cha degree huko mtwara walilalamika kukosa wanafunzi kama ulivyosema ?

Hio vyuo vya serikali nimeweka kama extra na ni reality, wanafunzi wengi hupenda kuchagua vyuo vya serikali, wakikosa ndio wanaanza kucheki vyuo private kama Saint Joseph, Abdulrahman, Teku, Tumaini, Kampala, n.k.

Ni chuo gani cha degree huko mtwara walilalamika kukosa wanafunzi kama ulivyosema ?
 
Naomba unijibu swali nililokuuliza hapo awali

Ni chuo gani cha degree huko mtwara walilalamika kukosa wanafunzi kama ulivyosema ?

Hio vyuo vya serikali nimeweka kama extra na ni reality, wanafunzi wengi hupenda kuchagua vyuo vya serikali, wakikosa ndio wanaanza kucheki vyuo private kama Abdulrahman, Teku, Tumaini, Kampala, n.k.

Ni chuo gani cha degree huko mtwara walilalamika kukosa wanafunzi kama ulivyosema ?
Siyo huyu aliyejibu ila ni Mimi nenda kwenye post husika nimejibu, alafu uwe makini unachanganya sana.
 
Back
Top Bottom