So unataka nikuamini kwa porojo!? Yaani maneno matupu unataka niyaamini mbele ya takwimu rasmi!? Hiyo michezo ya vijiwe vya kahawa usiilete hapa JF.
Sijataka uniamini, wala sijasema nilichosema mimi ndiyo ukweli.
Sitaki kuamini, nataka kujua.
Nimeeleza shaka kuhusu data.
Kama unaelewa the scientific process, utajua kuwa kuna peer review.
Peer review huanza kwa mtu kusema "wait a minute, something does not seem to be right here. I could be right or I could be wrong, but something seems off here".
Na katika point hii, mtu hahitaji data kusema hivyo, hahitaji takwimu.
Kwa sababu, huo ndiyo mwanzo wa kutafuta takwimu.
Inawezekana mkoa wa Kigoma umepiga hatua kubwa katika kupunguza idadi ya watu kutoka 2.4% mpaka 1.5% kutoka sensa ya 2012 mpaka data za 2022. Na data hizi ni sahihi. Nitafurahi sana ikiwa hilo ni kweli.
Inawezekana mkoa wa Kigoma umegawanywa na mimi sijui na hivyo mkoa wa Kigoma wa awali si sawa na wa sasa.
Inawezekana ukusanyaji wa data una matatizo, watu wengi wa Kigoma si raia wa Tanzania na hivyo hawataki kuhesabiwa wala ku interact na serikali.
Sasa mimi niki raise concern ya data integrity, kitu ambacho ndicho kinaanzisha uhakiki, kwa nini unataka kulazimisha lazima nije na data?
Kama data za sasa zina walakini, na tunaweza kupata mtu wa kutupa muktadha mzuri zaidi, na data sahihi hazipo je?