Mikopo na sera mbovu za ubinafsishaji ndizo zimetufikisha hapa, Mwaka 2000 exchange rate ilikuwa(1 Usd=Tshs 803.3)

Naunga mkono hoja
 
Zaidi ya 70% ya export yetu inatokana na Madini,ambayo yanachukuliwa hapa kwenda kuuzwa huko Ulaya-kwa maana hii hizi export ni kama namba tu ambazo hazina impact yyt kiuchumi ndani ya nchi.
Kama wanunuzi wangekuwa wanakuja kununua haya madini hapa Nchini basi wangenunua kwa fedha yetu na fedha yetu ingepanda thamani.Vilvile Kama hii migodi ingekuwa inamilikiwa na Wawezekazi wa ndani hata kama wangekwenda kuuza nje basi wangerudi ndani wakileta hizo USD zinazotokana na faida na mwishowe wangepandisha uchumi na shilingi ya Nchi.

The so called uwekezaji kwenye Nchi aina ya Tanzania yenye viongozi wala rushwa na wananchi wajinga ni utahira.
 
Uchumi wa nchi unapimwa kwa uzalishaji na ufanisi wa balance of trade.
Umetumia njia ndefu Sana kufika kwenye hili hitimisho ambalo hasa ndiyo linatakiwa kuwa kiini cha mjadala huu.

Jee udhaifu wa sarafu yetu unasababishwa na sababu Gani ya kiuchumi!??

Maana uimara ama udhaifu wa sarafu ya nchi yoyote ile duniani hautokei kusikojulikana, bali huwa na chanzo chake cha kiuchumi.

China inazalisha kwa wingi bidhaa mbali mbali tena kwa gharama ndogo kwa Teknolojia ya kisasa na bora kabisa.

Sisi tunazalisha ama tunauza nini kwenye soko la kimataifa. Urari wetu wa kibiashara (balance of payment/trade) kimataifa ukoje!?

Kwa mtazamo wangu badala ya kujikita kujadili thamani ya sarafu yetu kimataifa, basi tujadili kwanza thamani ya uchumi wetu kimataifa.
 
Hii nchi inatakiwa ipate kiongozi mzalendo atakaye amua kusimamia sheria.
Nimekuja kugundua wanao ikwamisha Tanzania ni Marais hao hao tunawachagu hapa kidogo mwenye ahueni ni Nyerere.wengine wote ni chanzo cha haya matatizo yote.Na mbaya zaidi kwa mfumo wa kiutawala wa hii Nchi Rais ndio kila kitu-yani ni mfumo wa hovyo kweli.

Viongozi na wananchi wote hawawezi kufikiria na hata wakifikiria lazim fikra zao ziakisi ambacho kitampendeza Rais-hivi nchi ya namna hii inaweza kuendelea vipi?????.huyo huyo Rais na wafanya uamuzi wenzake wamejiwekea kinga ya kikatiba wasishutakiwe either wakiwepo au wasipokuwepo madarakani-viongozi wa namna hii ambao hakuna sheria ya kumwawajibisha anaanzaje kuwaza namna ya kuipeleka Nchi mbele kwa 50 yrs to come.

Yani Tanzania ni zaidi ya upumbavu.
 
Mbona nimeanza kulisema hilo awali kabisa kwa kutumia mfano hai kabisa wa China?

Kama nilivyosema awali, pesa ni bidhaa kama bidhaa nyingine, thamani yake, kimsingi, inapatikana kwa forces za demand and supply.

Sasa kama Tanzania ina import mpaka toothpicks, halafu exports zake ni chache, na hizo chache karibu zote ni unprocessed raw materials ambayo inaacha value kubwa sana kwa kuto export processed goods, currency yetu itapanda thamani vipi?

Sisi tuna import kuliko tunavyo export. Pesa zetu hazina demand sana kwa sababu watu wengi hawaji kununua vitu kwetu. Kuna wakati nilirudi New York City kutoka Tanzania, nikawa nimejisahau nimerudi na shilingi za Tanzania (nilibadili dola nyingi nikawa nimemaliza likizo kabla ya kumaliza shilingi, nikazisahau shilingi kwenye begi mpaka nikarudi nazo New York City). Kufika New York City, nikagundua nina shikingi za Tanzania, nikatafuta Bureau de Change inayoweza kuchukua shilingi za Kitanzania na kunioa dola za US, sikupata. Hela haina demand, thamani inapatikana kwenye demand, hela itapandaje thamani?
 
Mwalimu hakuwahi kuza uchumi wowote zaidi ya kutumia hazina aliyoachiwa na wakoloni akaitumia vibaya kutaka kumrejesha swahiba wake madarakani dhidi ya idi amini zingine akazitapanya kwenye ukombozi wa nchi za Africa
 
Mwalimu hakuwahi kuza uchumi wowote zaidi ya kutumia hazina aliyoachiwa na wakoloni akaitumia vibaya kutaka kumrejesha swahiba wake madarakani dhidi ya idi amini zingine akazitapanya kwenye ukombozi wa nchi za Africa
Hizi hadithi za kwenye vijiwe vya kahawa usilete kwenye mjadala wa mada makini kama hii.
 
Kwanza ujinga sana
Unakopa kujenga vyoo kweli ,halafu unakusanya tozo kununua VX ,si upumbavu huu jamani
Nchi hii inakera sana
 
Weka account ya dollar upige hela.
Viongozi wenyewe hawana uchungu na nchi halafu wewe ndiyo una uchungu na nchi.
Piga hela angalia maisha yako na kizazi chako
 
Kwanza ujinga sana
Unakopa kujenga vyoo kweli ,halafu unakusanya tozo kununua VX ,si upumbavu huu jamani
Nchi hii inakera sana
Badala ukope Kisha Benki zipewe pesa hizo na kupunguza interest rates Ili sekta ya Uchumi ikue,

Faida na Kodi utayopata hapo ndio ikajenge madarasa na vyoo,

RUSHWA ni tatizo kubwa Nchi hii.
 
Hutopata muwekezaji huyo
Sasa hapo atakua amefanya nini
Yaani aje na Dola 1M mathalani ,apambane apate faida halafu siku ya kuondoka aondoke na Dola 1M ile ile , we kuweza mkuu?
 
Rate ya Bank inasoma hivyo ila mtaani watu wanauziana 2882 ilikua juzi hii ukitaka kwa hiyo ya Bank hauwezi kupata kitu naona inakimbilia Tsh 3000 kwa 1 usd...
Wahusika wapo bize na campaigh. One thing nimejifunza kuna ka utamaduni, kiongozi (si wote) akijua kazingua anakaa kimya, wenyewe wanasema (upepo upite), aka mbongo asahau.
No uwajibikaji
 
Weka account ya dollar upige hela.
Viongozi wenyewe hawana uchungu na nchi halafu wewe ndiyo una uchungu na nchi.
Piga hela angalia maisha yako na kizazi chako
Ukiwa na akili za aina hiyo unaweza hata kufanya biashara haramu ya drugs,au hata kuuza viungo vya binadamu.

Kundi dogo la wezi halitakiwi kukufanya ukose Uzalendo.

Ninaipenda sana Nchi yangu nzuri Tanzania.

Tuipende Nchi yetu. Amen
 
Bado hata huko kwenye exportation bado tabu tupu
Ukiwa na maparachichi Yako unataka uyauze uingereza kupata export permit ni mzunguko
Ukiwa na mahindi Yako unataka uyapeleke Kenya au Ethiopia shughuli yake si mchezo
Ukiwa na ngozi za ng'ombe unataka uwapelekee Gucci au LV kupata kibali sahau
Kwa hiyo hata export inauliwa na hao hao wanaotorosha dhahabu sababu ya ukiritimba na roho mbaya, matokeo yake tunabakia hoi kama nchi
 
Hutopata muwekezaji huyo
Sasa hapo atakua amefanya nini
Yaani aje na Dola 1M mathalani ,apambane apate faida halafu siku ya kuondoka aondoke na Dola 1M ile ile , we kuweza mkuu?
Kama anataka kuondoka na dola basi afanye biashara ya kuingiza dola. Yaani export business. Unaalika mtu kuja kuendesha mwendokasi. Anaingiza Tsh halafu wakati wa kuondosha faida anabadilisha kuwa dola!! Mbona tunakuwa tunafanya biashara kichaa.
 
Maparachichi njia rahisi ni kuyatoa kupitia Mombasa aisee yanatoka na box za Nairobi wakati yanatoka hapo Njombe na Moshi Nchi ngumu sana hii vitu vya kuingiza fedha za kigeni kupata vibali kama sijui unatoa kitu gani wakati SA ukitaka kufanya Export yeyote kibali ni siku moja kinafanyiwa kazi na unawaambia utatoa kwa mpaka upi ili ikiwezekana upewe na agent kabisa na vitu vyote ni bure kasoro gharama ya Agent huko Mpakani nilienda na Jamaa mmoja kutoka Iringa alidhani ile huduma tuliyopewa tunalipia kumbe ni free of charge harafu jamaa wapo serious kweli..
 
Ndio hapo ,Kwa hakika sisi watanzania tuna matatizo sana
Sijui tuna laana gani ,mtu anataka ahodhi kila kitu yeye ili abaki mwenyewe kana kwamba ataweza kutosheleza mahitaji ya soko la kimataifa
Mimi naamini hizi bidhaa za kilimo zingekua msaada mkubwa kwenye kuingiza pesa za kigeni na kuwainua wakulima ,bahati mbaya wenye maamuzi hawataki iwe hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…