Mikopo ya kausha damu ipo mtaani, tuwe makini

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Dakika kadhaa zilizopita nilikutana na maajabu hapa mtaani kwetu

Wamekuja wanaojiita maofisa wa kausha damu wako na mjumbe na mwenyekiti wa serikali za mitaa na polisi wawiili wakaingia kwenye nyumba moja ya mdada

Dada akagoma kufungua, wakaenda upande wa chumbani wakaita wakasogeza pazia wakamwona, mjumbe akaomba afungue asiwe na wasiwasi khaaa yaliyofuata yanasikitisha sana

Mdada alienda pembeni na mjumbe na kadhaa wakamsainisha makaraatasi, kilichofuata ni kuita vijana waliokuja nao wakaanza na tv ya 42, wakafuata na makochi meza ya mable sebuleni, wakamaliza sebule nzima wakaona haitoshi mdada analia tu jamani.

Wakaenda chumban kwake wakabeba kitanda, walitaka na godoro mjumbe akazuia, wakazoa kabati la mbao jamani aisee.

Hizi kampuni nani mmiliki na nani anawapa jeuri kama hizi jamani! dada kabaki na vyumba vyake viwili na godoro analia analia analia kama kafiwa na wazazi wote siku moja

Tuwe makini mnaopenda kukopa wapendwa, mikopo ndio mizuri mingine ina laana, mtaua wazazi wenu wakisikia mambo kama haya.

Rip mali za dada yangu.
 
Hii njia waliotumia kufidia deni lao imevunja sheria.
 
Kutokujua kwetu sheria ndio sababu majambazi hao wanaojiita wakopeshaji wanakuwa na nguvu.

Mtu pekee anaeruhuisiwa kuchukua samani yako ni yule aliekuuzia samani hiyo kwa mali kauli (Hire purchase) na ukashindwa kupeleka marejesho. Kinyume na hapo mdai yeyote mwingine ni sharti afuate process za kimahakama.

Alichofanyiwa huyo dada ni uvamizi, ana haki ya kufungua kesi na hata kudai fidia. Anaweza hata kusema katika vitu walivyochukuwa kulikuwa na kiaisi cha fedha.

Wabongo pia ni wavivu sana kusoma mikataba. Unapokuwa na shida ya pesa, unasaini chochote utakachopewa bila kusoma. Kumbe umesaini uhai wako kwa walaghai wa mjini.
 
Dhamana yako wakati unakopa hiyo Kausha damu ilikuwaje

Lakini pia ,iangaliwe hao wanalipa Kodi au wanawakausha tu watu damu na hakuna la mana
Upo utaratibu wa kufuata ikiwemo idhini ya mahakama na tena ikiwa mdeni atakiri hana uwezo tena wa kulipa wakati huo (huenda akaomba muda wa kulipa uongezwe na alipe kidogo kidogo kwa muda fulani).
 
buza nini??
 
Watanzania wengi ni matapeli, siku ya kukopa anakenua meno yote 32 siku za marejesho zikifika hapokei simu. Acheni kulaumu hao kausha damu au mnataka wafirisike ili muwacheke.
Mtanzania ukimchekea kwenye biashara yako unafirisika asubuhi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…